Phlagiey
JF-Expert Member
- Oct 26, 2013
- 3,487
- 1,651
Muda wingi huwa najiuliza mbona watoto wakike wanakuwa wagumu linapokuja swala la kujitegemea kimaisha kwa maana ya kupanga nyumba na kuanzisha maisha? pengine nikafikiri labda ni waoga wa maisha, lakini jibu likaja hapana maana kuna wengine unakuwa wamemaliza masomo, wanakazi nzuri mishahara safi lakini bado wanang'ang'ania kuishi majumbani mwao, sikuishia hapo nikawaza na kuwazua labda swala la umri ndiyo tatizo jibu pia nikapata hapana kwa vile wapo amboa ni wakubwa kiumri wapo mpaka wenye miaka 25-34 na kwendelea wana kazi lakini bado hawafikiri kwenda kujipangia kachumba kake.
Baada ya maswali yote hayo nikaamua kuchukua hatua ya kutafuta majibu kwa wahusika wenyewe nilizungumza na wadada kadhaa kupitia mtandao fulani fulani hivi majibu niliyopewa yalinipa wasiwasi kidogo, wengi wao walisema wana subiri kuolewa ndiyo maana wanaamua kukaa majumbani mwao pia ukiolewa kutokea nyumbini inaongeza heshima kuliko mwanaume akikukuta ukiwa umepanga, wengine wakasema mtoto wakike akijitegemea ni rahisi kushawishika na mambo ya starehe, jibu hili likanifanya nijiulize inamaana wale wadada tunaokutana nao club za starehe wote wamepanga? na kama hawajapanga huwa wanaondokaje majumbani wao.
Mwisho nikajibiwa kwamba wazazi ndiyo wanawakatalia watoto wakike kupanga basi nikauliza sababu napewa zile zile za kushawishika kujiingiza kwenye maswala ya starehe, nikamua kuachia hapo lakini majibu ya hoja zao yako wazi kabisa nikilinganisha na mazingira halisi tunayoishi kila siku, kama ilivyo ada naomba hili swala nilirudishe kwenu wadau wa jamii forums nahitaji kusikia mawazo yenu, unakifikiri ni kwanini mtoto wakike hastahili kupanga na kuanza maisha ya kujitegemea mapema? mzazi, kaka na dada mnalizungumziaje hili.
Karibuni kwa michango yenu.