Wadada acheni hii tabia!

Maundumula

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
7,553
3,070
Habari,

Wadada walio wengi hupenda kufunguka sana kwenye first date. Utakuta mtu unamuangalia tu unamlia timing ili umfahamu vizuri.

Anaanza, " Unajua mimi kwanza nilikuwa na Mr A nikampenda sana ila alichonifanyia sikuamini kumbe alikuwa na gf mwingine, Nikawa na B naye akanitenda akaenda zake Ulaya hajarudi tena na mawasiliano kakata, nikawa na C naye akaja kuniacha ghafla akafunga ndoa bila kuniambia sababu......nk"

Acheni hii tabia mabinti ni suicidal, yaani unampa brother message kwamba akupige chini fasta kama walivyofanya wenzake. Pengine alikuwa hana mpango huo. Acheni hii mambo wakina mamdogo ita wa cost. Utabaki unalia kwamba huna bahati kila siku ukiwa na tabia hii.
 
heri mimi huwa namwambia mi bikra .sijamjua mwanaume bado
kumbe list chalinze mwanzaaaa......
kudadalusinde....

nao kwa mawazo yao finyu wanaona ni kweliii.....
kumbe mtu ulishajaza Yutong 4 na fuso 2......cheni bandia......pesa bandia......nani mjanja.....
kudadalusinde.....
 
mie first date sitokwambia yote hayo, usually napenda kuobserve, kusoma body movement zake, kumwangalia anavyoongea na simu na reaction kwenye kila simu......anavyotreat barmaids nk..............

Ukiniuliza mahusiano yangu ya nyuma nakutajia mmoja tu uliopita, kungwi wangu aliniambua simwambue mwanaume siri zote ambazo anaweza kuzitumia kukuumiza....
 
Hebu wadada endeleeni kufunguka, maana mkiambiwa nyie ni nyoka mnakuwa wakali ila hapo naona wote mmeji-express yourselves kwa ufasaha!
 
nao kwa mawazo yao finyu wanaona ni kweliii.....
kumbe mtu ulishajaza Yutong 4 na fuso 2......cheni bandia......pesa bandia......nani mjanja.....
kudadalusinde.....

Uzuri wake ni kwamba we unadhani unamdanganya kumbe naye anataka kula kisolokupwinyo then asepe! Wanaume huwa wanajitoa akili wanapotaka kisolokupwinyo hata mshahara atakupa sasa ukisgamegwa ndo utaona huo mshahara!
 
mie first date sitokwambia yote hayo, usually napenda kuobserve, kusoma body movement zake, kumwangalia anavyoongea na simu na reaction kwenye kila simu......anavyotreat barmaids nk..............

Ukiniuliza mahusiano yangu ya nyuma nakutajia mmoja tu uliopita, kungwi wangu aliniambua simwambue mwanaume siri zote ambazo anaweza kuzitumia kukuumiza....

ni kweli ndugu yangu umenena kuhusu hayo mengine atakuja kuyajua baadae taratibu!
 
Bora umewaambia, na kuna wengine sku ya kwanza mtu anakujia na mavyeti ya angaza. Sasa ndio iweje? kama umepima wewe tena ndio kila mtu akapime?
class bulldog kingdom mammalia nyambaaf kabisa .
 
first date nina 0%, dont have any strategy than being myself.

Yeye ni nani hadi nipretend kum-impress, atapretend yeye kuni-impress mie.
 
shkamoo lawyer.

Naona klorokwini anajivuuuuuta kuipokea !
Anaonekana huyu tangu asubuhi keshapokea nyingi ! Zimemlevya, afu mbona mi hunipaki Shkamoo ? Naambuliaga "Hi" au "Mambo?" "Hujambo?" baaas!
Au kwa vile tunajuana kwa nguo za kuogea ?
 
Last edited by a moderator:

shikamoo mme wangu! Ai lavu yu, mwaaaah!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom