Wachumba wasiolingana kielimu

Ilonza

Senior Member
Jan 11, 2011
119
13
Siku hizi vijana wengi hasa walio soma ushaurina eti lazima kutafuta mwenzi aliyesoma,kwa kuangalia sababu za kiuchumi, tatizo kwangu sijaweza kuelewa kuwa na msicha unaye mpenda mpaka kuzingatie level ya elimu yako na ya mwenza au unawezafanyaje?
 
Kuwa na yule unayempenda!!!
Mapenzi ni zaidi ya Elimu na kazi!!
Ila pia ni added advantage!!!
 
sometime it help
na ni nzuri tena hasa mwanamke usimzidi mwanamue elimu
kuepuka adha za inferiorty complex
 
Elimu, Elimu, Elimu,
Kabila, Kabila, Kabila,
Kazi, Kazi, Kazi,
Dini, Dini, Dini
Utaifa, Utaifa, Utaifa

Na nini tena kimebaki kazi kwako
 
elimu ni wajibu ili kuongeza ufaham.
Katika mapenzi si jambo muhimu...ila umuhim ni maelewano katika mahusiano/ndoa yenu.
Ukiona watu wana zingatia elim basi ujue mwisho wao ni naqama(distroy).
Wapo wasomi huushia kuwasusa wake/mume zao na kutafuta watu wa kuwakidhi haja zao!
Sasa faida ya elm ipo wapi?
Elim na mapenzi ni vitu tafauti.
Labda elim na kazi.
 
Elimu ni muhimu sana . Kuna tofauti kubwa kati ya kusoma na kuelimika sasa watu wengi wanaangalia kasoma hadi level gani lakini si mtu ana uelewa gani.DINI nayo ndio msingi wa ndoa hakuna ndoa bila ya dini kwahiyo mume anaweza kufuata dini ya mke au mke akafuata dini ya mume hapo ni maelewano yao.
 
Mie nadhani Kuoa au kuolewa na mtu unayekaribiana au kulingana naye kielimu ni muhimu sana. Binafsi watu ambao nimeshakutana nao na kupiga nao story za maisha pamoja na maisha ya ndoa, Wengi wa wanaume waliooa wanawake ambao wamewazidi sana kielimu asilimia kubwa hujuta kwa kiasi fulani, na wengine hudhubutu hata kutafuta hawala wa pembeni ambaye wanalingana nae kielimu angalau kujiridhisha.

Unajua kutofautiana sana kielimu binafsi naona si vizuri kwa sababu kama familia mnatakiwa kushirikiana kwa kila kitu ikiwemo mawazo. Sasa wewe kwa mfano una pHD unaoa std 7, unadhani anaweza kukuchallenge? au wewe ndo utakuwa decision maker wa kila kitu? Si kwamba nadharau watu ambao hawajasoma lakini kuna utofauti mkubwa sana kati ya mtu aliyesoma na ambaye hajasoma. Labda kama una lengo la kuoa mtu kwa ajili ya kukuzalia tu watoto basi na wewe ndo uwe kila kitu.

Ila haya ni mawazo yangu binafsi na uzoefu nilionao.
 
mi nachukua point ya wanandoa kuelewana, pia kumuweka mungu mbele. Ndugu yangu, cha muhimu, phd na swala la ndo ni tofauti, haijalishi hajasoma kabisa, ila awe na upendo wa kweli, heshima, busara, na mwenye kuthamini utu!
 
nakuna shule/chuo cha kusomea ndoaaaaaa!!!!!!! hakuna kabisaaaaaa!!! Biblia ikasema mke mwema mtu hupewa na Mungu !!!

maswala ya elimu/rangi/kabila/umbile si kigezo cha kuwa na ndoa nzuri !!!

tazama ndoa za wasomi nyingi zimevunjika !!!
 
Nitie kama muhuri moyoni mwako,maana upendo una nguvu kuliko mauti,una wivu kuliko ahera,mwanga wake ni mkali,kuliko mwanga wa moto,Kama mtu angetoa MALI YAKE,PESA YAKE,ELIMU YAKE,Ili anunue Upendo,atakachopata ni BURE KABISA!
 
Elimu sio ishu bwana, nawafahamu watu wengine maprof na madoc lakini wameoa au kuolewa na layman na woman na ndoa zao zinadumu.

Naona cha msingi ni kuaminiana na kuheshimiana.
 
Kuwa na yule unayempenda!!!
Mapenzi ni zaidi ya Elimu na kazi!!
Ila pia ni added advantage!!!

Inaelekea unaishi dunia ya ndoto au definition yako ya mapenzi ni finyu mno! Kama unadhani utaweza kukaa na mtu kwa miaka 40 alafu kila siku asubuhi ukimwona moyo unaenda spidi kama ile mara ya kwanza utakuwa hujui maana ya mapenzi! You have to find something deeper beyond emotional feelings. You have to share more than emotions. Elimu ni moja ya viwango unaweza kuweka. Pia unaweza kuweka class ya mtu, nk...
 
Elimu, Elimu, Elimu,
Kabila, Kabila, Kabila,
Kazi, Kazi, Kazi,
Dini, Dini, Dini
Utaifa, Utaifa, Utaifa
wanene, wanene, wanene,

wembamba, wembamba,
wembamba,
wenye range rover, wenye bajaji, wenye maguta.
Kaaaaazi kwelikweli
 
Elimu mata sana stnd 7 na phd hawaendani hata kdogo mtaishia tu kuchukiana bila sababu hata knye maamuz ya kifamilia yatabaz upande mmoja!
 
Tunaposema tunawajua watu wengi wenye tofauti kubwa kielimu alafu ndoa zimedumu sipingi wapo ila katika Asilimia ngapi? Ni ndoa ngapi za namna hiyo hudumu? KUna ndoa kudumu kwa sababu tu wanandoa wameamua Kuvumiliana kwa sababu ya vitu fulani fulani lakini ndoa
zenye afya kabisa(sijamanisha sisizo na matatizo 100%) kwa mawazo yangu swala la Elimu lina mchango wake. Kunapokua na gap kubwa la kielimu kunafanya sehemu fulani kuwe na utupu wa muingiliano wa kimawazo na hata kiutendaji,swala ambalo naliona kama ni risk.
Ni mtizamo wangu tu.
 
Nimeolewa mbumbumbu form four ila yeye alikuwa msomi, kanisomesha mpaka sasa nina elimu ya juu na ninajivunia, mapenzi sio elimu ndugu zangu ukimpenda mtu kama alivyo vingine kuvipata ni kitu rahisi sana.
 
Back
Top Bottom