"Wachumba huishi kwenye ikulu na wanandoa huishi kwenye nyumba halisi"Praise the lord

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,139
"Wachumba huishi kwenye ikulu na wanandoa huishi kwenye nyumba halisi"

Kabla ya kuolewa mwanamke huona matumaini yanayong’aa kwa mume wake mtarajiwa, anaona ulinzi, uimara, matumaini na upendo usio mfano na mwingine huringa na kutembea kwa madaha hata hivyo baada ya kuolewa anaanza kuona udhaifu na ndoto zote zinaanza kuyeyuka na kusinyaa kama au maridadi kwenye jua kali la ikweta, hukatishwa tamaa na yote huja ghafla kama kimbunga na anaanza kuumia na kujuta kwa kuwa mahitaji yake hayajatimizwa kama alivyokuwa anaona mwanzoni.
Haamini jinsi mume asivyomjali na kumsikiliza na kumpenda.

Hadi hapo mke anaweza kuamua kuitikia kwa:-
(i) Kwa hasira kutokana na hayo mume wake amemuonesha]
(ii) Kwa Kuwekeza kwa upendo, imani katika uwezo/uimara (strength zile anaziona kwa mume wake na kuanza kuijenga ndoa upya

Ili mambo yaenda vizuri au upendo wa kweli uzaliwa mke anatakiwa kuamini uwezo wa ndani wa mume wake alionao ( streghth siyo weakness).
Anaweza kuwekeza kwa mume halisi aliyejificha kwa mume wa nje mwenye kutojali kutimiza ndoto zake za uchumba na honeymoon.

"The secret in marriage is not finding a hero to be your husband, but finding the hero in your husband”

Mungu amempa kila mwanamke uwezo wa ajabu wa kumsaidia mume wake kukua na baada ya muda mume kuwa mcha Mungu sawa na anavyotakiwa.

Bahati mbaya ni kwamba wanawake wengi wamekatishwa tamaa sana kiasi kwamba huyu mwanaume aliyenaye leo hawezi kuwekeza chochote kwa ajili ya mume huyu atakavyokuwa kesho
 
"The secret in marriage is not finding a hero to be your husband, but finding the hero in your husband”
Many women do not know this secret. Most of them are looking for the hero in the drama, football, leadership, college, physical appearance etc but this is not what the marriage life need actually. Thats why many marriage end up in breaking away soon after the first day or whatever
 
Back
Top Bottom