Wachina wanatumaliza na pikipiki ama tunajimaliza wenyewe??

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,778
Kwenu wananchi
kama mjuavyo baada ya bajaji tumeamua kuja na pikipiki usafiri wa haraka zaidi
kwa baahati mbaya wimbi hili limekuwa msiba kwa watanzania wengi jamani
ukifika kule arusha kuna wadi ya pikipiki kabisa kila siku wanaletwa kama si maiti
ICU
ukija muhimbili ni balaa tupu ...je hii ni wachina kuamua kupunguza idadi ya watanzania kuzaliana ovyo ama ni sisi tunajimaliza wapendwa??
 
Ni sisi tunajimaliza wenyewe na polisi wa usalama barabarani kwani asilimia kubwa ya hao madereva wa pikiki hawana leseni na bado wapo bararani.
 
Hili la pikipi ni sisi wenyewe yaani ajali kwa ujumla tusitafute mchawi ni sisi wenyewe. maana kila kukicha hukosi kusikia ajali iliyogharimu maisha ya watu hizo ni zile zinazotangazwa tu! je sisizotangazwa ni ngapi?
 
Kuna utafiti umefanyika unaonyesha kuwa kila siku hapa Tanzania mtu mmoja anakufa kutokana na ajali ya pikipiki

SABABU: Mimi nafikiri sababu kubwa ni waendesha pikipiki maanake wanakimbia sana halafu hawana control ya pikipiki zenyewe. Pili ni vijana wadogo waliomaliza darasa la saba ndio wanaendesha pikipiki hizi pasipo uangalifu na mafunzo sahihi

Jeshi la polisi lazima wajipange kwenye kuthibiti tatizo hili
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom