Wachina wampiga Mkuu wa Kituo cha Polisi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Wachina wampiga Mkuu wa Kituo cha Polisi

Tuesday, 21 June 2011 22:12
0diggsdigg

Joseph Lyimo, Babati
Mwananchi

VURUGU kubwa zilizuka juzi kwenye kituo cha Polisi Babati Mjini mkoani Manyara baada ya wafanyakazi wa kampuni inayojenga barabara ya Chico, raia wa China kumpiga mkuu wa kituo hicho, ASP Shaaban Minginye na mkuu wa polisi jamii mkoani humo, ASP Morris Okinda.

Tukio hilo lililodumu kwa saa mbili kati ya saa 12:30 jioni hadi saa 2:30 usiku liliwalazimisha polisi kutumia mabomu ya machozi na risasi za moto zilizorushwa hewani ambazo hata hivyo zilijibiwa na Wachina hao wakitumiia bastola nao, hali iliyoweka rehani amani mjini Babati.

Wachina hao wanadaiwa kufanya vurugu hizo na kuwashambulia ASP Mingiye na Okinda kwa madai kuwa polisi walimwachia dereva wa basi la abiria aliyelikwaruza gari lao na kusababisha ajali.

Kitendo hicho cha kuwapiga makonde viongozi hao wa polisi mkoani humo kiliamsha hasira za wananchi ambao walianza kumshambulia mmoja wa raia hao wa China.

Mwananchi ilishuhudia raia huyo wa China, Chang Charles akipigwa na wananchi hao waliochukizwa na kitendo chao cha kuwapiga polisi ambapo alijaribu kutumia mtindo wa kujihami 'kung fu' huku akitoa sauti za, 'huu, haa', lakini alipigwa ngumi iliyomjeruhi usoni

Katika tukio hilo, ASP Minginye alipigwa vibao na ngumi na raia mmoja wa China ambapo raia watatu wa China walijeruhiwa vibaya na wananchi (Hongereni sana Wabongo) na kulazwa kwenye Hospitali ya Mrara mjini Babati na hali zao zilielezwa kuendelea vizuri.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Liberatus Sabas alithibitisha jana kutokea kwa tukio hilo na kwamba raia 10 wa China wanashikiliwa kwa kuhusika na vurugu hizo.


Alisema chanzo cha vurugu hizo ni raia mmoja wa China, (Chang Charles) kumpiga mkuu wa kituo cha polisi Babati, baada ya kuliachia basi la abiria lililogonga lori linalomilikiwa na kampuni hiyo (Chico), kitendo kilichofanya wananchi kumpiga Mchina huyo.

"Hali hiyo ilijitokeza baada ya basi la abiria aina ya Scania, mali ya Kampuni ya NBS lililokuwa likitokea Kahama kwenda Arusha kukwaruzana na gari la kampuni hiyo ya Kichina lililokuwa linatumika katika ujenzi wa barabara ya Babati-Singida,"alisema.

Alisema baada dereva wa basi hilo kulikwaruza gari la kampuni ya Chico aina ya Ford, tukio hilo liliripotiwa kituo cha polisi Babati na dereva wa basi kutakiwa kuwapeleka abiria Arusha ili kesho yake arudi kituoni hapo.

“Baada ya dereva wa basi kuruhusiwa na kuondoka raia mmoja wa China alianza kurusha mawe kwenye basi hilo na kuvunja taa na kioo cha mbele na kumpiga mkuu wa kituo, ndipo abiria waliposhuka na kuanza kumshambulia Mchina huyo,” alisema Kamanda Sabas.

Alisema baada ya vurugu hizo lilizuka kundi lingine la raia wa China lilijitokeza na kuanza mapambano na wananchi na ndipo katika vurugu hizo askari polisi wakapiga risasi hewani na mabomu ya machozi ili kuwatawanya na kujaribu kusitisha vurugu hizo.

“Hadi hivi sasa Jeshi la Polisi linawashikilia raia 10 wa China wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo na tunatarajia kuwafikisha mahakamani leo (jana), ili wakajibu mashtaka ya uaribifu wa mali na kufanya vurugu,” alisema Kamanda Sabas.

Kamanda Sabas aliwataja Wachina hao wanaoshikiliwa na polisi kuwa ni Chang Charles, Luan Hiten(23), Wang Sheng(23), Sing Yun(24), Sing Jin (23), Lin Jun (37), Whang Puong(23) Lu Gang (23) na Sio Jing (23).

Alisema katika vurugu hizo, askari polisi mmoja ambaye hakumtaja jina alijeruhiwa jichoni na Wachina hao na raia watatu wa China walijeruhiwa na kulazwa Hospitali ya Mrara wakipatiwa matibabu.

Aliwataja raia hao wa China waliojeruhiwa kuwa ni Young Gris, Luan Hiten na Chang Charles ambao alisema hali zao zinaendelea vizuri, baada ya kupatiwa matibabu.



 
wachina huko washazoea kupiga wabono afu tayari kuna thread ka hii tulichangia jana mod hebu zijoin
 
Hisia za mwandishi ndizo zinazo ongoza ujumbe huu badala ya kuelezea tukio lilivyo kuwa!
Kwa aina ya tukio na uzoefu tunaouona kwenye police nachelea kusema wachina walikuwa sahii kumtia makonde mkuu wa kitu! Maelezo waliyowapa wachina ninaimani asilimia tisini titofauti na walivyo tenda!!
 
hawa polisi walimuachiaje huyo dereva bila ya kesi?sometimes polisi hua wanatia hasira sana
 
Ushabiki mwingine haufai, hata kama tunajali uataifa wetu, lakini lazima haki itendeke kwa sabau nchi yetu inaamini kuwa binadamu wote ni sawa na ndi o maana tunapiga vita ufisadi. Sasa ilkuwaje Polisi wamwachie dereva wa basi bila kuwajulisha wachina kisa cha kumwachia, kwa maana hiyo wachina waliona kama wamedharauliwa. Mkuu wa Kituo kama kiongozi alitakiwa kutumia akili yake kuwakutanisha wachina na dereva ili kutatua mgogoro huo kabla ya kumruhusu dereva wa basi kuendelea.
 
Kesi ya traffic tena ya kukwaruza gari haiwezi kumfanya dreva akae lockup wakati anaweza acha lesen yake na kuwaisha abiria
 
hawa polisi walimuachiaje huyo dereva bila ya kesi?sometimes polisi hua wanatia hasira sana
dereva anaposababisha ajali (Not Mauaji ) huachilia kwa kuiacha leseni yake kituoni na hutakiwa kufika kwa ajili ya mzozo wake nextday.Huu ni utaratibu wa kawaida kabisa.
 
Mkome kuwakaribisha Wachina,barabara yenyewe ndiyo hizo zinaumuka kama imewekwa hamira. Na bado,ingetakiwa wawachakaze wale police na wachukuwe utawale anga ile.
 
tukiendelea kuna siku tutasikia Mr. OCD apigwa mande na wawekezaji wa KICHINA.
Nakumbuka kuna mzungu arusha alimnasa vibao RPC ofisini.
 
ila hapa hawajaandika kama dereva aliachiwa kwa kuacha lesseni
dereva anaposababisha ajali (Not Mauaji ) huachilia kwa kuiacha leseni yake kituoni na hutakiwa kufika kwa ajili ya mzozo wake nextday.Huu ni utaratibu wa kawaida kabisa.
 
tukiendelea kuna siku tutasikia Mr. OCD apigwa mande na wawekezaji wa KICHINA.
Nakumbuka kuna mzungu arusha alimnasa vibao RPC ofisini.
hawachelew tutasikia spika anne kashikwa shikwa makalio..haya mambo wee utaona
 
Wanadiplomasia hii imekaaje? How do we handle and a foreign affair issue withouth being emotinally driven! This might offend our political connects!
 
Tanzania yetu inazidi kupotoka! sijui wajukuu zetu wataikuta katika khari gani!???
 
hawa polisi walimuachiaje huyo dereva bila ya kesi?sometimes polisi hua wanatia hasira sana

Nafikiri hajaelewa. Polisi hapo walitumia busara kuiruhusu gari iende Arusha ikashushe abiria kisha irudi kwa ajili ya kesi.
Kwani wangeizuia pale basi wangewaathibu abiria bure kwa njaa na mateso.
 
Hisia za mwandishi ndizo zinazo ongoza ujumbe huu badala ya kuelezea tukio lilivyo kuwa!Kwa aina ya tukio na uzoefu tunaouona kwenye police nachelea kusema wachina walikuwa sahii kumtia makonde mkuu wa kitu! Maelezo waliyowapa wachina ninaimani asilimia tisini titofauti na walivyo tenda!!
Corect.
 
Back
Top Bottom