Wachina Sokoni Kariakoo, nani wa kulaumiwa?

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,772
4,054
Juzi niliweza kwenda Kariakoo kununua mahitaji ya nyumbani. Chaajabu ni hiki hapa:
garlic.bmp

Nilipo taka kununua Kitunguu swaumu, muuzaji alinipa bei mbili. Kilo moja ya Kitunguu Swaumu Kutoka Tanzania ilikuwa Shilingi 2,200 na kilo moja ya kitunguu Swaumu kutoka China ilikuwa Shilingi 1,700.

Jamani Nani wa kulaumiwa hapa? Jamani hata Vitunguu vinatoka uchina?

Flag-Pins-China-Tanzania-300x240.jpg
 
huyo muuzaji alikuwa mhuni tu!, alitaka akuuzie vitunguu vilivyokaa sikunyingi sokoni ..
 
huyo muuzaji alikuwa mhuni tu!, alitaka akuuzie vitunguu vilivyokaa sikunyingi sokoni ..

Mkuu, vile vya kutoka uchina vilikuwa vikubwa kwa umbo kuliko vya kwetu Tanzania na bei yake ni chee. Vya Tanzania ambavyo vilikuwa vidogo kwa umbo, bei yake ni kubwa 2, 200. Mkuu hali inatisha sasa. Yaani hata vitunguu tunaagiza kutoka uchina?
 
Zambia wanauza kuku wa kichina au kuku wa kizambia; Kuku wa kizambia ghali zaidi ya wa kichina

It is frighterning... they use the same process and procedures to raise chickens...

HAYA TUNAPENDA MISAADA YA KICHINA HIYO
 
Jaribuni sana kujiepusha kununua vyakula vya kichina, juzi niliona kwenye taarifa ya habari kama sikosei ilikuwa CNN au BBC kwamba Wachina wenyewe kule kwao wanaogopa kula vyakula vyao hivyo wengi wameanza ukulima mdogo mdogo wa vitu kama nyanya na mboga za majani.
 
mama yangu weeeeeeee mpaka vitunguu vinatoka china jamani wahusika mnaruhusu vipi vitunguu kutoka nje wakati vitunguu vya wakulima vinaoza lushoto kule sitaki kuamini kama ndiko tulikofikia
Juzi niliweza kwenda Kariakoo kununua mahitaji ya nyumbani. Chaajabu ni hiki hapa:
garlic.bmp

Nilipo taka kununua Kitunguu swaumu, muuzaji alinipa bei mbili. Kilo moja ya Kitunguu Swaumu Kutoka Tanzania ilikuwa Shilingi 2,200 na kilo moja ya kitunguu Swaumu kutoka China ilikuwa Shilingi 1,700.

Jamani Nani wa kulaumiwa hapa? Jamani hata Vitunguu vinatoka uchina?

Flag-Pins-China-Tanzania-300x240.jpg
 
Wakulaumiwa wa kwanza serikali legelege wapili wananchi wa TZ kwakuchagua chama na sio uwezo wa mtu
 
Back
Top Bottom