Wachezaji watatu wasubiri safari ya majaribio Vancouver White Caps

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
Date::4/22/2009
Wachezaji watatu wasubiri safari ya majaribio Vancouver White Caps

Na Dorice Malyaga

Mwananchi

WACHEZAJI Zahoro Pazi, Nadir Haroub 'Cannavaro' na Nizar Khalfan wameiunga mkono safari yao kwenda kwenye majaribio nchini Marekani katika klabu ya Vancouver White Caps baadaye mwaka huu.

Akizungumza na Mwananchi jijini jana wakala wa wachezaji hao, Said Tuli alisema wachezaji hao wako mbioni kujiunga na timu hiyo baada ya kukamilisha mipango yao ya safari.

Alisema wachezaji hao walichaguliwa na uongozi wa timu hiyo, Vancouver baada ya kuonyesha uwezo mkubwa wakati timu hiyo ilipokuwa ziarani nchini.

''Wachezaji hawa watajiunga na timu hiyo mara tu utaratibu utakapo kamilika.''

Wakati timu hiyo ilipokuwa nchini ilicheza na Yanga, Simba na Taifa Stars na mchezaji Zahoro Pazi alionekana baada ya kucheza vizuri akiwa kama mshambuliaji ambapo Nizar alisimama katikati kwenye kikosi cha Stars.

Mchezaji Nadir Cannavaro aliteuliwa kwenye kikosi hicho baada ya Vancouver kuvaana na Yanga mwanzo wa mwaka huku akigundulika kuwa kizuizi kikubwa kwenye kikosi chake.
 
BUBU,from the bottom of your heart,kweli,kweli unaona tanzania kuna mcheza mpira,au ni watu tu,wanaukimbiza mpira?
 
Back
Top Bottom