Wachezaji wa Azam FC waliozamia Sweden Wasakwa na Polisi

Babuji

Senior Member
Nov 27, 2008
197
3
POLISI nchini Sweden wameapa kuwasaka wachezaji watano wa timu ya vijana ya Azam waliotokomea wakiwa nchini humo hivi karibuni.

Wiki iliyopita, wachezaji hao walitoroka na kuzamia kusikojulikana baada ya kufanyika kwa mashindano ya ‘Gothia Cup’ yaliyofanyika katika mji wa Gothenburg nchini humo.

Mtanzania anayeishi nchini humo, John Tarimo aliliambia gazeti moja la kila siku la Tanzania kwamba karibu kila sehemu kuna picha za vijana hao.

"Kila sehemu jamaa wamewekwa, kwenye televisheni, mitaani na hata magazeti. Kweli ni hatari sana na jamaa wameapa lazima wawapate na kuwarudisha huko.

"Kwa kweli ni hatari, haijulikani wako wapi lakini nahisi watawapata tu kwa kuwa ni vigumu sana kwao kwa vile picha zao ziko kila mahali," aliliambia gazeti hilo.

Lakini, Msemaji wa Polisi katika mji wa Gothenburg, Nils Lundqvist ameliambia gazeti la Göteborgs-Posten kuwa watafanya kila juhudi kuhakikisha wanawapata vijana hao na kuwarejesha Tanzania.

Source:
http://www.nifahamishe.com
 
Salama ya hao madogo ni kukimbilia nchi nyingine na kujiainisha ukimbizi wa nchi zetu majirani bila ivo wamefulia. Watarudishwa bongo na moja kwa moja Kisutu halafu Keko.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom