TL. Marandu
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 3,625
- 5,807
Nimekuwa Nikijitaabisha sana Kifikira, Kutaka Kujua, Kwanini Tanzania, Utakuta Makabila Mawili au zaidi Wana lugha karibu Moja Mfano Wasukuma na Wanyamwezi Lakini Wakati huo huo, Kabila Moja katika Eneo Dogo La Kilimanjaro, Kabila la Wachagga wana Makundi madogo yenye Kutofautiana Lugha?
Warombo Kwa Mfano, Wilaya Ya Rombo Peke yake, Kuna Wamkuu, Wana lugha tofauti, Ukiendelea Kidogo Utakuta Kuna Wamrao, Ukiendelea Kidogo Utakuta Wamashati, Ukiendelea Unakuta Waseri na Tarakea.
Nilichogundua ni Kuwa Sio Swala La Ubishi, Bila Mawasiliano, Watu hawawezi Kuwa na Lugha Moja. Pia Nikagundua Huko siku za Nyuma Kulikuwa na Mvua nyingi sana Zilizotokana na Mlima Kilimanjaro Kukinga Mawingu ya Mvua.
Kutokana na Mvua Nyingi, Mito Mingi Mikubwa na Midogo Ilitiririka Kutokea Mlima Kilimanjaro, sasa Nilichogundua, Kila Unapovuka Mto, Lunga inabadilika Kidogo, Kadiri ya Ukubwa wa Mto Ndipo Upande wa Pili Lugha inatofautiana zaidi.
Mfano Rombo, Ukitokea Mkuu Ukivivuka Mto mkubwa Ungwasi Lugha Inabadili Kiasi cha Kushidwa Kuelewana, Halafu Ukiendelea, Ukavuka Mto mdogo wa Washi, Lugha inabadilika Kidogo, Ukiendelea Ukavuka Mto Maarwe Ndio mwisho wa Lugha ya Kimrao, Keni na Kimashati, Ukiendelea Ukavuka Mto Katangara na Kisha Mto Kikelelwa na Mto useri, Lugha inabadilika Kabisa Inakuwa Kiuseri.
Hivyo Hitimisho Langu Ni Kuwa Huko Nyuma, Mito ilikuwa Ni Mikubwa sana, Madraja hayakuwepo, na Kulikuwa Mahusiano ya Pande Mbili zilizotengwa na Mto yalikuwa ni Madogo, na Madogo zaidi Kadiri ya Ukubwa wa Mto. Ndio Sababu hasa ya Tofauti za Lungha lizipo sasa Kwa Wachagga. Leave it or Take it.