Wacha kelele, mwenzako yule pale, kimyaaa!

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,603
Ilitokea ajali ya barabarani lakini kwa bahati nzuri abiria walipata mikwaruzo tu kidogo isipokuwa mmoja ambaye alifariki hapo hapo.

Katika walioumia, mmoja aliyekwaruzika mguu na kutoka damu nyingi, alikuwa analia kwa kelele. Baada ya kuona kelele zimezidi, abiria mmoja alishindwa kustahamili na kumkabili yule majeruhi.

"Wewe ha**thi nini? Kelele tu! Yo yo yo, uwii uwii uwii! Mwangalie mwenzako yule pale, amekufa na yuko kimya, wewe kwa kuumia mguu tu kelele hatuna amani. Pumbafff!!!"
 
Kaka mfano mzuri huo na ni fumbo. CUF walishakufa zamani sana , sasa chadema wakipiga kelele serikali inasema acha kelele we si unamuona mwenzio kimyaaa. Thanks mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom