Wabunge wetu wana sifa hizi???

Jakubumba

JF-Expert Member
Mar 5, 2011
1,624
500
JE NI WABUNGE WETU WANA SIFA HIZI HAPA CHINI ZA KIONGOZI BORA?
1.Kusimamia SHERIA bila kujali gharama yake
2.Mshawishi wa vitendo, uadilifu na ujasiri
3.Kiongozi bora haogopi kukosolewa
4.Kiongozi bora huthubutu
5.Asimamie maamuzi
6.Adhibiti msongo wa mawazo
7.Awe egemeo la watu
8.Afahamu kutatua matatizo
9.Asiwe mwenye majungu
10.Awe mkweli.

My take.Najua humu jf ni watu wa busara na wapenda kutangaliza maslahi ya nchi kabla ya chama. Tujiiuliza je hivo vyama,viongozi wetu tunaowashabikia wana hizo sifa za kulifikisha taifa letu mahala pazuri?
 
Wabunge wote wa Chadema wanazo hizo sifa zote ulizozitaja tatizo linakuja kwa chama cha magamba ccm kuukataa ukweli,na hata Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kulikemea hili mwaka 1993 wakati mapendekezo ya kuundwa kwa serikali tatu yalipiwasilishwa Serikalini.
 
wewe ciril

umepotea akbisa, bora ungeipsha hii mada.

mimi nasema wapo wenye uwezo huo na wapo wasio nao, pia wapo walionusu, but tuwaombee wayajue majukumu yao
 
Kwa Tanzania hii ya mgombea hakubaliki na watu wake mpaka ahonge na ikiwezekana achakachue na kura ili aweze kuwa madarakani.Kwa kiasi kikubwa wabunge wa hiki chama kinachoitwa Chukua Chako Mapema(CCM) wengi wao hawa hizo sifa;na hata hao wenye sifa bado wanaendekeza kutetea maslahi ya chama kwanza na siyo Taifa kwanza.Na hapo ndipo ugonjwa ulipo;kwa vyama vilivyobakia kwa kiasi fulani wanajitahidi sana kuwa smart katika maslahi ya Taifa na wengi wao wana hizo sifa zilizotajwa.
 
Wabunge wote wa Chadema wanazo hizo sifa zote ulizozitaja tatizo linakuja kwa chama cha magamba ccm kuukataa ukweli,na hata Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kulikemea hili mwaka 1993 wakati mapendekezo ya kuundwa kwa serikali tatu yalipiwasilishwa Serikalini.

Ndugu yangu hata mitume wa Mungu walikuwa hawana sifa zote hizo zilizotajwa, lakini wabunge wenu wa Chadema ni zaidi ya mitume, ni wazee wa upaku
 
Wabunge makini wa Chadema wapo ni wachache, Zitto Kabwe, Halima Mdee, John Mnyika, Said Arfi, hao wengine ni type ya kina Komba, na mbunge pumba Chadema ni Lema huwo ndio ukweli ata kama mnampenda
 
Haya wabunge wote wa chama cha magamba(ccm)wanazo hizo sifa,jipigie makofii mengi basi
 
Dogo ebu angalia mabandiko yangu vizuri, nimetoa mfano wa wabunge makini, mimi ni Independent Thinker sio mtumwa wa vyama vya siasa
 
Ukweli ni kwamba hakuna kiongozi yoyote tanzania mwenye hata nusu ya hizo sifa,wote ni wachumia matumbo tu.
 
Wabunge makini wa Chadema wapo ni wachache, Zitto Kabwe, Halima Mdee, John Mnyika, Said Arfi, hao wengine ni type ya kina Komba, na mbunge pumba Chadema ni Lema huwo ndio ukweli ata kama mnampenda

Wakuu hebu tuendeleze ile dhana la jamvi hili la kuwa la great thinkers. mambo ya ushabiki tuyaweke kwenye clubs, vyama n.k. Kwa kufanya hivyo tutanufaika na mawazo na fikira sahihi (si maanishi za mwenyekiti Mao, au Mwl Nyerere), nina maanisha tutapata michango iliyochambuliwa kiyakinifu badala ya kinazi(Unazi/upendeleo fulani).

Ni mapema mno kusifia wabunge bora ni wepi na wepi si bora. Leo hii Bwana Kaborou mbunge machachali wa Kigoma ambaye alikuwa CHadema watu Wachadema wanamweka kundi gani? na wengi tu siyo Chadema tu wapo kina Lamwai NCCR/CCM.

Wabunge wetu wengi hawaingii bungeni kutetea na kulinda masilahi ya nchi na raia wa majimbo yao, waliowengi wameingia kuganga njaa zao na familia zao, kulinda masilahi ya vyama vilivyo kuwa ngazi ya kuingia bungeni, na wale ambao hawakuingia kwa lengo la kuganga njaa wameingia ili kulinda biashara zao,utajiri wao ambao wakiulizwa walivyoupata mara nyingi hawana maelezo. kwani upo msemo kwa kingereza unaosema kuwa (you can be free but not famous but no man shall be famous without being free).Ni kwamba unaweza kuwa huru lakini siyo maarufu, lakini hakuna mtu ambaye atakuwa maarufu bila kuwa huru. Sasa hawa watu maarufu wanatafutaje uhuru wa kuwa maarufu? baadhi yao ni kuununua kwa gharama yoyote, kugh'agha'ania madaraka, kuhonga n.k. Hayo ndo mabo makubwa yanayo wapelekea watu kuacha taaluma zao kuingia kwenye taaluma zitakazo wapa uhuru wa kulinda masilahi.
Nahitimisha kwa kusema kwamba ni mapema sana kusema kuwa tunao wabunge wazuri na wabaya, wote mimi bado naona wako sawa tu hadi hapo tutakapo pata watu makini wanaofanya kazi walizotumwa kufanya, walio na lengo lakuacha Historia yao (Legacy) na si kuchumia tumbo,kuganga njaa, na kulinda masilahi yao.
 
Mkuu, nashukuru sana kwa Argument zako, tunapenda watu kama wewe humu JF muwe wengi lakini mpo wachache wengi humu ni Chadema-kata upeo wakuchambua mambo ni mdogo wanakubaliana kila kitu kwa sababu wote ni Chadema, mfano nadhani umeuona kwa huyo member mwenzetu anasema wabunge wote wa Chadema wanazo hizo sifa
 
wabunge wengi wa chama cha magamba hawana hizo sifa hizo, wao wapo sana sana na zidumu fikra za mwenyekiti.
 
Back
Top Bottom