Wabunge Wetu Vihiyo; Wanatia AIBU

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
3,444
264
Hivi huyu mdudu ilipitaje bungeni.... Gharama kupitishwa kwa 1,400% bila mtu kuhoji?
Je Wabunge wetu wanajua kusoma? Lazima mtu angehoji kama kweli wanafanya kazi tunazowatuma kufanya. Bunge letu sasa siyo tu kituko ,bali halifahi kama wanaweza kupitisha madudu kama haya hapa chini

This is shameful. Shame on our MPS


By CCM-MAMA
Bunge ilipitisha kwamba wale wote wanaorenew road licence lazima walipie huduma ya moto. Hapo mwanzoni hii huduma ya moto ilikuwa Tsh 3,000/ leo hii hiyo huduma imepanda kuanzia Tsh 40,000/ kwenda juu.

Sasa hii huduma ya moto iliyopitishwa na bunge ni la nini wakati hatuna hata zima moto moja kwenye maeneo nyeti kama airport. huu mrani ni wa nani na kwa nini. TRA inatumaliza na kodi zinazowanufaisha mafisadi.

Bunge mko wapi?
 
Kwenye katiba mpya lazima kuwepo na kipengele kitakachosema kwamba mgombea ubunge ni lazima awe na degree/diploma.
 
Kwenye katiba mpya lazima kuwepo na kipengele kitakachosema kwamba mgombea ubunge ni lazima awe na degree/diploma.
Mkuu unaweza kuniambia chenge ana elimu gani? Najua una hasira, kunywa maji kidogo ndipo urudi kuandika.
Naona kama unawinda sisimizi kwa bunduki!!!!!
 
Bookish education, kwenye utendaji tanzania huwezi kutofautisha standard 7 au graduates tena ni afadhari standard7 atafanya vizuri kwa kuogoma waliosoma. Mimi huwa siwaamini kabisa wasomi wetu kipindi nikiwa cbe wakufunzi waliwaferisha wanachuo makusudi kwasababu ya kutoelewana kati yao na mkuu wa chuo.
 
Werema ana elimu gani na yeye?

mkuu Nyani Ngabu, heshima!!!!
Nia ya kuulizia elimu ya chenge ilikuwa kupata sababu za uwiano wa kusoma sana na kuwawakilisha wananchi, kwa mfano wa chenge aliyetuingiza mikenge mingi ya mikataba mibovu akiwa AG, na kujidanganya kuweka minimum requirement kumuwezesha mtu kugombea nafasi ya ubunge.

Mimi sijui elimu ya werema, namuona yupo yupo tu!!!!
Sidhani hata kama ana setifiketi ya sheria, "nimezingatia maamuzi yake ya kisheria awapo bungeni"
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom