Wabunge Wetu Mlioko Dodoma Jioni Hii

SolarPower

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
223
27
Tunaomba sana muanzishe kodi mpya ya Michango ya Harusi, ambapo Kiwango cha Kodi kinachopendezwa kwa Kila Harusi inayochangiwa fedha kiwe ni asilimia 99.999. Kodi Hii Mpya Inapendekezwa Kuanza Kutumika Kuanzia Kesho Asubuhi Siku ya KARUME DAY>
 
serikali inahangaika na kuongeza kodi kwenye petrol wakati vyanzo vipo vingi tu ka michango ya harusi
good idea
 
Tunaomba sana muanzishe kodi mpya ya Michango ya Harusi, ambapo Kiwango cha Kodi kinachopendezwa kwa Kila Harusi inayochangiwa fedha kiwe ni asilimia 99.999. Kodi Hii Mpya Inapendekezwa Kuanza Kutumika Kuanzia Kesho Asubuhi Siku ya KARUME DAY>

watu huchangia harusi kwa kutaka sifa
 
Mhm!Waungwana hapa napita tu maana naona nyota nyota mbele yangu.
 
sasa kodi ya harus watakusanya vp?wengine wanaoa kimya kimya.
 
Tunaomba sana muanzishe kodi mpya ya Michango ya Harusi, ambapo Kiwango cha Kodi kinachopendezwa kwa Kila Harusi inayochangiwa fedha kiwe ni asilimia 99.999. Kodi Hii Mpya Inapendekezwa Kuanza Kutumika Kuanzia Kesho Asubuhi Siku ya KARUME DAY>
Wazo zuri kwani watu wamezoea kuchangia harusi lakini hawataki kuwachangia watoto wanaokosa ada za shule.
 
Labda kama unatania ila kama unamaanisha unachokisema basi hii imepitiliza. Chezea vitu vyote ila acha mzaha na uhai wa taifa. Ni kupitia harusi (za kila aina zikiwemo zile za kimila kule kijijini) taifa huongezeka na kukua. Wakati wenzetu Uarabuni serikali zinagharamia na kutoa zawadi kwa wanaofunga harusi, wewe unaleta utani!

Vinginevyo unataka kujenga taifa la ajabu ambalo linatokana na watoto wasio na wazazi wanaoeleweka. Fikiria ni watu wangapi watashindwa kufunga harusi endapo kodi hii itaanzishwa. Nadhani una mawazo kwamba harusi ni zile za kifahari tu; hata ndoa za mikeka zina gharama zake.

Cha msingi ndoa/harusi na ziheshimiwe na watu wote na ndio mwanzo na uhai wa taifa lolote lile. Mungu katujalia rasilimali kibao ambazo mafisadi wanazivuruga kwa hasara ya wengi hili la kodi kwenye harusi hebu liachwe kwa faida ya wote na taifa bila kujali ni maskini au matajiri. Kama kuna mahali umeliona au kulisikia huko "ulaya" - sisi Tz tuna tamaduni na desturi zetu. Tuache ku-copy na ku-paste kila kitu.
 
Dudus,

Changamoto yako ni nzuri. Wazo hili ni langu mwenyewe. Labda tukubaliane kuwa kuwe na kiwango cha michango ya harusi ambacho kama kikivukwa basi michango inayozidi ndiyo inatozwa hiyo kodi ya asilimia 99.999. Binafsi sioni kwa nini harusi yoyote ile kwa gharama za sasa izidi shilingi milioni 3. Ni aibu kuona kuwa mtu kachangia shilingi 200,000 kwenye harusi lakini hayuko tayari kununua kitabu kinachouzwa kwa shilingi 35,000 tu.
 
Sawa inaweza kuwa ni aibu lakini hebu fanya utafiti kidogo kwa nini watu wanafanya hivyo (kuchangia harusi badala ya vitabu/elimu). Sidhani kama ku-imposed kodi ndio italazimisha watu kubadilika. Ni lazima kutakuwa na sababu ya msingi ya kijamii ya watu kufanya/kutokufanya hivyo na ni tafiti za kisayansi pekee zitakazotoa majibu.
 
Shida zenu msituletee hapa jamvini. Mmeishiwa mambo muhimu ya kujadili? Unashindwa hata kuishauri serikali ikusanye kodi kwa hawa wenye nyumba wanaojipangia bei ya pango watakavyo na kudai kodi ya mwaka mzima as if kuwa serkali inakulipa mshahara wa mwaka mzima in advance. Hebu acha wivu bwana kama hutaki kuchangia harusi za wenzio si unyamaze tu kwani kuna mtu alishashtakiwa kwa kushindwa kuchangia harusi? Challenge kwa serikali ni kufanya kodi iwe kwa hiari kama watu wanavyochangia harusi. Hela inayokusanywa na serikali ingeonekana inafanya nini na kwa kuzingatia vipaumbele vya nchi watu wangechangia kwa hiari tu kama wanavyochangia harusi. Acha mawazo mgando ndg yangu!!!

Wazo zuri kwani watu wamezoea kuchangia harusi lakini hawataki kuwachangia watoto wanaokosa ada za shule.
 
Shida zenu msituletee hapa jamvini. Mmeishiwa mambo muhimu ya kujadili? Unashindwa hata kuishauri serikali ikusanye kodi kwa hawa wenye nyumba wanaojipangia bei ya pango watakavyo na kudai kodi ya mwaka mzima as if kuwa serkali inakulipa mshahara wa mwaka mzima in advance. Hebu acha wivu bwana kama hutaki kuchangia harusi za wenzio si unyamaze tu kwani kuna mtu alishashtakiwa kwa kushindwa kuchangia harusi? Challenge kwa serikali ni kufanya kodi iwe kwa hiari kama watu wanavyochangia harusi. Hela inayokusanywa na serikali ingeonekana inafanya nini na kwa kuzingatia vipaumbele vya nchi watu wangechangia kwa hiari tu kama wanavyochangia harusi. Acha mawazo mgando ndg yangu!!!
Pole kama limekugusa lakini wenye nyumba wanakula kwa jasho.
 
Sawa inaweza kuwa ni aibu lakini hebu fanya utafiti kidogo kwa nini watu wanafanya hivyo (kuchangia harusi badala ya vitabu/elimu). Sidhani kama ku-imposed kodi ndio italazimisha watu kubadilika. Ni lazima kutakuwa na sababu ya msingi ya kijamii ya watu kufanya/kutokufanya hivyo na ni tafiti za kisayansi pekee zitakazotoa majibu.

Mkuu Dudus,

Sijakurupuka. Na nimefanya utafiti wa kutosha. Kwangu mimi ni ulimbukeni uliovuka mipaka kwa mtu kuchangia harusi shilingi 50,000 wakati anakataa kumnunulia mtoto wake au mtoto wa jirani yake au mtoto wa ndugu au rafiki yake VITABU VYA NEW GERENAL MATHEMATICS, BOOK 1 T0 4 AMBAVYO GHARAMA YAKE YOTE KWA HIVYO VITABU VYOTE VINNE KWA BEI YA REJAREJA NI SHILINGI ELFU 36 TU. Vitabu hivi vina idhini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kutumika katika shule zetu zote za Sekondari kwa Kidato cha Kwanza Mpaka cha NNe kwa Nchi Nzima.
 
Kweli kabisa.Kwasababu tukiwekeza katika Elimu tutakuwa tumemsaidia huyo mtoto pamoja nataifa kwa ujumla
 
kweli kabisa.kwasababu tukiwekeza katika elimu tutakuwa tumemsaidia huyo mtoto pamoja nataifa kwa ujumla

bila hisabati ni kuota ndoto za mchana. Sasa hivi pale udsm kuna matayarisho ya harusi moja yanaendelea kwa kasi ya mwanga chini ya dr. Omari .k. Mbura (0715 26 45 91). bajeti ya harusi hii ni shilingi milioni 50. ukinunua vitabu vya additional mathematics kwa ajili ya kidato cha kwanza utapata vitabu visivyopungua 5,555 kwa bei ya reja reja ya shilingi 9,000 kwa kila kitabu. hiki kitabu cha form one cha additional ndiyo kitabu pekee na cha kwanza kutungwa hapa nchini na kupata ithibati ya kutumika katika shule zetu za sekondari toka katika wizara yetu ya elimu na mafunzo ya ufundi. Kitabu hiki kimetolewa na kampuni ya gdy publications company limited (0754 32 60 61).
 
Back
Top Bottom