Wabunge wengi hufa mara tu baada ya kumaliza muda wao bungeni!

wanakuwa wameshapata posho ya kutosha kuishi maisha ya sayari ya 3 inawabidi waelekee sayari nyingine wakaendelee na yanayojiri huko.
 
Khaaaaa
kwanini asiseme
wanakufa sbb
posho znakatika
pamoja na magonjwa ya kidoti com?
 
Kama hawawezi ku 'manage' finances zao sasa tutawasaidiaje. Wao wamekalia kushindana. Kwanza lazima tuwakumbushe kuwa kazi ya ubunge walituomba tuwape kura. Wengine walituhonga na wengine wakatupigia magoti. Sasa wasilinganishe na kada nyingine ambazo wao waliajiriwa kwa kazi zao, ingawa pia napinga posho katika sekta zote. Kama pesa haziwatoshi ni kubwaga manyanga aje yule anayejitolea na sio kuwaongezea pesa. Wabunge wetu wengi wamelimbuka kwahio wanataka kujaribu kila wanachokiona mtaani
 
Khaaaaa
kwanini asiseme
wanakufa sbb
posho znakatika
pamoja na magonjwa ya kidoti com?

Posho zinakatika?sijakusoma please. Au unamaanisha kuwa matumizi yao ni makubwa kuweza kwenda sambamba na posho hizo? Lakini amenitisha zaidi alipodai kuwa. Mbunge anamaliza muda wake february anakata kamba. April. Ina maana kipindi hicho kifupi cha miezi miwili tu kimetosha kukwangua viji faranga vyake vyote?nna shaka! Au kuna man made issue
 
Back
Top Bottom