Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,460
- 39,928
mwingine akasema "viongozi wasijilimbikizie mali".. walichosahau ni kuwa kulikuwa na semina ya siku kumi ambapo kila mbunge alilipwa elfu 80 kwa siku kama posho!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
halafu watu wanakataa lunch ya milioni moja.. right.
halafu watu wanakataa lunch ya milioni moja.. right.
Nasubiri kwa hamu kweli kweli msimamo wa Chadema kuhusu hii inconsistence ya sera na vitendo. Kwamba wanataka kuondoa umaskini uliokithiri kwa wananchi na wakati huo huo wanatumia rasilimali za wananchi kujilimbikizia huku wakitutangazia kwamba viongozi wasijilimbikizie!
Tuache porojo za kwenye majukwaa na dhana ya "staki nataka".Wabunge wa CDM kama kweli ni Wazalendo na njaa zao haziwazibi macho wafanye yafuatayo na wathibitishie umma wa Watanzania kuwa si sawa na CCM Club:
1.Kuamua kwa kauli moja kuzikataa ama kurudisha pesa hizo kama wamekwisha chukua.
2.Kuchukua na kuzielekeza kwenye matatizo ya Wananchi (Elimu,Afya & Ajira).
3.Kuzigawa kwa wao kupata usafiri wa bei nafuu(RAV 4) na kiasi kingine kuelekeza kwa Wananchi.
Ni mbunge mmoja wa CCM(Lameck Airo) ndiye aliyetamka kubadili matumizi ya hizo fedha kwa kununua katapila ya kuchonga barabara jimboni kwake.
Tunaomba CDM watoe tamko kati ya hayo na si porojo za "ndumilakuwili".
Nimetafakari na kuona kwamba uamuzi waliofanya watu wa visiwa vya Sheli Sheli ni uamuzi wa busara sana. Wao baada ya kuona viongozi wao wanawadidimiza waliamua kuwaita Wafaransa wawe wakoloni ili mradi tu walete maendeleo. Kwangu nafikiri ni wakati mwafaka hapa kwetu pia tuwaite wakoloni waje watutawale. Hawa watu tunaowaita viongozi siyo kabisa. Hakuna wanachofanya kabisa.
Mfano badala ya kununua magari 300 kwa bei ya shilingi milioni 90 wakanunua mitambo ya umeme tunaweza kutibu kabisa tatizo la mgao wa umeme hapa Tanzania. Kwani thamani ya hela zote ni dola za Kimarekani milioni 18. Nimefanya utafiti wa generator na nimeona kwamba kuna generator yenye uwezo wa kuzalisha MW 307 inauzwa $ milioni 18. Tukipata generator hii tutakuwa na upungufu wa umeme wa megawatt 43 tu. Tukifikiri zaidi ni kwamba kama mawaziri wangetumia magari ya bei ndogo tungeweza kutatua tatizo la umeme mwaka huu bila shaka.
Lakini hawa jamaa wametuasi. Mimi nasema viongozi wetu ni waasi, tunapaswa kuwapinga kwa namna zozote.
Power Plants and Generators - Equipment and Turnkey Installation
Hapo umesema ukweli,mkuu... mbona unaelekeza kwa CDM tuu... si kuna KAFU, NCCR na UDP ...hao huwaoni ..bado sikuelewi
lakini hlo mbona ni swala la kawaida kabisa kila baada ya uchaguzi ma MP wote hupewa?
CDM ni wachache sana zaidi ya hao wababe CCM , hivyo hata wakizikataa wale jamaa wataendelea kuzitanua tu
sasa bora kipi?
pia kumbuka kuwa hata wakizikataa hizo pesa hazitzrudishwa HAZINA ng'o zinaishia tu mikononi mwa wajanja.
hiyo ni bora zaidi ya kuzikataa, maana hazitarudi hazina.zitaishia tu mikononi mwa wanyang'anyiKweli, Lema zichukue ukaboreshe huduma za hospitali Arusha!