Wabunge wawe at least graduates kwenye katiba mpya ya Tanzania

kama ikipita, basi sugu, mnyika, mbowe out, huena cdm wakabaki na mbunge 1
Na zile degree feki za akina Nagu, Mahanga, Nchimbi, na wengine, zichunguzwe wafikishwe mahakamani kwa forgery.
Mtoa mada be careful usije shushwa kishipa na akina Maji Marefu na Waganga wengine standard four kutoka Nyinyiem kama akina Lusinde.
 
Kikarara na Wana Jamvi

1. Hao ambao hawakupata fursa ya kuwa na Degree wapewe nafasi kwenye Serikali za Mitaa; eg Mjumbe na Diwani; ila Mwenyekiti na Meya wawe na Degree. Nina sababu za msingi sana kusema haya. Mjumbe na Diwani watawakilisha vyema hoja za hawa waliokosa fursa.
2. Ni kweli sio wote waliosoma wamefanya maamuzi ya busara. Pengine tupate utaratibu wa kuchuja wasioweza kufanya maamuzi ya maana/busara.
3. Ukaribu na Wananchi, utendaji kazi na uadilifu ni vitu muhimu sana vya kuzingatia. Ukaribu mara nyingi hupimwa kwa kura; ingawa hapa nchini hawa waheshimiwa wabunge wamekuwa wanarubuni wapiga kura kwa kuwapa vitu vidogo. Utendaji kazi na uadilifu ni vigumu kupimika kwa mtu anayeomba kura kwa mara ya kwanza, ila kwa yule anayerudia; ni muhimu kupima utekelezaji wake wa yale aliyoahidi wakati anaomba kibali cha kuingia mara ya kwanza.
4. KWELI KUFELI SHULE SIO KUFELI MAISHA AU KUKOSA SHULE SIO KUKOSA MAISHA. SS BAKHRESA, Shule hana lakini anatumikisha Maprofesa, Ma PhD, Ma Engineer; wa ndani na nje ya Nchi; from all over the world. Wazungu, Wamarekani, Wa Australia, wahindi nk. Hio point kwa hili nakubaliana 100%. Aidha, angalia Rais wa Kwanza wa Zanzibar, utendaji wake na mafanikio yake ya Miaka 8 ya utawala wake; naamini utakubaliana na mimi kwamba wakati wa utawala wa Karume (wa Kwanza) Zanzibar ilipiga hatua kuliko wakati wa Awamu 6 zote zilizomfuatia ukizijumlisha kwa pamoja. Ila napenda kukujuvya kuwa sasa nyakati zimebadilika. Dunia imekuwa na utandawazi. Mambo mengi hufanyiwa majadiliano ili kufikia muafaka. Sasa ukimpeleka kwenye majadiliano Darasa la 4 na Graduate wa Harvard, utakuwa umetafuta mechi ya Boxing Tyson na Yondani. Kuna mambo mengi yanahitaji analysis ya kisomi; kwa mfano
a) Madini;
b) Nishati (Umeme, gesi, makaa ya mawe, petroli, diesel, mafuta mazito);
c) Biashara (Katika Jumuiya za mtangamano, baina yetu na washirika wetu na jinsi za wengine zinavyotuathiri utendaji wetu);
d) Kilimo (ruzuku, NFRA, uuzaji na ukatazaji wa uuzaji wa nafaka; ghala nk);
nk, nk, nk

Sasa kwa kuzingatia hayo ndio maana nimetoa hiyo Rai.

Nimezingatia kuwa wengi hawajapata fursa ya kuwa graduates.

Na pia nimezingatia kuwa kutokuwa graduate sio kuwa failure.

Lakini kuwakilisha katika mazingira yenye changamoto nzito ni ngumu sana.

Nimetoa mfano wa Bakhresa; yeye amefanikiwa kwa kuwa anawatumia wasomi aliowaajiri vizuri, wanajadiliana ushauri, anaelewa na anatekeleza. Tatizo tulilokwisha liona la viongozi wetu (Graduates and non Graduates) huwa hawazingatii ushauri wa wa taalamu na wakishapata Title ya UHESHIMIWA, basi wanaona wamefika PEPONI

Nawakilisha


QUOTE=Kikarara78;4287546]Makame na Wana JF,
Kamanda, Mimi napingana na wewe kidogo kwa hili:
1. Utawanyima Haki Wananchi aka Watanzania ambao hawakupata fursa ya kwenda shule kwa sababu mbali mbali kama Ujinga, Uzembe wa kutambua Elimu, Kutokuwa na Ada na Karo za shule (Hapa kundi hili ni kubwa wasio kuwa na uwezo wa kwenda shule), kipato duni cha maisha.
2. Sio watu wote waliosoma, wanafanya Maamuzi ya Busara, kwa hiyo kigezo kama ni Elimu, Je hawa Wasomi, wametusaidiaje kwenye Nchi yetu ya Tanzania ???
3. Kuna mambo mengi ya Msingi tungeangalia, kama Anayetaka kuwa Kiongozi, Je yupo karibu na Wananchi wake, Utendaji wake wa kazi upoje ??? Mwadilifu ???
My Take: Kufeli shule au kukosa Elimu sio Kufeli Maisha, hapa tuangalie Uadilifu, Kujioa, Bidii ya Kazi, na mengine mengi mazuri.
Nawakilisha[/QUOTE]
 
Makame naunga mkono hoja kwa asilimia 100%,kuwa kiongozi wa wananchi katika dunia ya sasa lazima upeo wa kielimu upewe kigezo kikubwa sana!Inasikitisha sana kuwakilishwa na wabunge ambao wakiona documents zilizoandikwa kiingereza wanageuka mabubu na katika mfumo huu wa globalization kuna umuhimu gani wa kuwa na mtu wa muundo huu kuwakilisha wananchi?

Suala la kusema uongozi ni karama siyo elimu ya darasani sikatai nakubaliana na nyie,lakini kama that is the case mbona maofisini ilikuwa kiongozi kigezo cha kwanza ni elimu? Suala la kusema litabagua wengine siliungi mkono hata kidogo,katika ulimwengu wa sasa usipokuwa na elimu umeshajibagua wewe mwenyewe huwezi kuwa sawa na wenye elimu kimtazamo tusidanganyane jamani.
 
Jamani watanzania uongozi si ukubwa wa elimu, kwa mwenendo wa hawa wasomi wa tanzania hakuna tofauti na mtu ambaye amezaliwa mjini na hajasoma ndiyo maana hata mbunge kama sugu ana mchango mkubwa bungeni kuliko nchemba, au john mnyika yupo juu kabisa ya chenge au mkono kwenye michango yenye masilai kwa taifa.
 
Nchemba ana degree ya UDSM na anadai kuwa ana first class lakini duh afadhali std four wanaonyamaza kule kwa bunge lol
 
mna ugomvi na lusinde na ngonyani. Of coz kama bunge ni kutunga sheria na wewe hujawahi kukutana hata na ka com skils si ni lzm utapeleka povu bungeni? hiyo iwe ni lzm atleast graduate. Unawezaje kuwa mbunge hata computer huijui?

Umemsahau Komba kwenye hiyo list!
 
Makame naunga mkono hoja kwa asilimia 100%,kuwa kiongozi wa wananchi katika dunia ya sasa lazima upeo wa kielimu upewe kigezo kikubwa sana!Inasikitisha sana kuwakilishwa na wabunge ambao wakiona documents zilizoandikwa kiingereza wanageuka mabubu na katika mfumo huu wa globalization kuna umuhimu gani wa kuwa na mtu wa muundo huu kuwakilisha wananchi?



Suala la kusema uongozi ni karama siyo elimu ya darasani sikatai nakubaliana na nyie,lakini kama that is the case mbona maofisini ilikuwa kiongozi kigezo cha kwanza ni elimu? Suala la kusema litabagua wengine siliungi mkono hata kidogo,katika ulimwengu wa sasa usipokuwa na elimu umeshajibagua wewe mwenyewe huwezi kuwa sawa na wenye elimu kimtazamo tusidanganyane jamani.
Mkuu naunga mkono hoja kwa 100% Na iwapo kuna mtu anapinga umuhimu wa elimu ktk uongozi then such person does not appreciate the role of education as large. Juzi TASAF wametangaza nafasi za kazi na position za kawaida kabisa lakini zote zinahitaji Masters degree. Sasa ukajiulize iwapo mtu wa 1st degree hawezi kuaminika na hawa TASAF ktk kusimamia miradi ya kawaida ya jamii kwa nini mtu mwenye elimu ya ngazi ya cheti aweze kuwa mbunge ambaye anatunga sheria na kupisha miswada inayohusu mustakabali wa taifa? Kama elimu si muhimu hebu fikiri iwapo elimu hiyo ya std 7 inaweza kuendesha vyombo kama BOT, TRA NSSF nk. Na wakati huo huo hayo taasisi hizo nyeti watu wake hawalipwi vizuri kama hao wabunge ambao wengi wao sio wasomi. Sasa hata hiyo haki ipo wapi? Nina uhakika kuwa huyo mtu mwenye masters akipata kazi hapo tasaf mshahara hauwezi kuzidi mil. 4 ikilinganishwa na huyn mbunge std 7 anaelipwa 10 mil. na marupurupu kibao ikiwepo kutibiwa India.
In fact elimu ya chuo kikuu bungeni ni lazima vinginevyo tija ktk taifa haitapatikana.
 
Napenda kuwasilisha hoja

Blair
Cameroun
Obama
Orlande
Merkell
Kibaki
NI GRADUATES

Aidha

Kuna suala zima la kuwa na comfo. Imagine mbunge wa darasa la 4 anapangiwa kamati ya bunge mfano ya Serikali za mitaa. Inatokea, Kamati ya Japan ya Serikali za mitaa imetembelea TZ, Mbunge wetu wa la 4 hatougua ili kukwepa aibu? ataongea nini?
 
Sasa hapo unataka kuingia Ugomvi na Mhe Freeman Mbowe -Elimu yake Secondary, Suzan kiwanga........Na chama wanachokaa vikao kama wapo kwenye vikao vya Ukoo
 
Back
Top Bottom