Wabunge waomba Bunge la Dharura kama JK asipowawajibisha mawaziri

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
Wabunge wa JMT wametoa maonu yao iwapo leo Spika wa Bunge hataipangia na kuipokea hoja ya Zitto ya kumwajibisha PM kwa dhana nzima ya uwajibikaji na kulindana.

Wameomba kuwepo na bunge la dharura kulingana na sheria na taratibu za bunge kwa sababu kuwaacha waendelee mpaka vikao vijavyo ni kuliua taifa.

Pia wabunge hao wanadai ni unafiki na uwongo kuwa rais hana taarifa ya mambo yanayojiri bungeni kama hajui iweje ajibu akiwa Malawi kama hana taarifa?
 
Kama kuna jambo la muhimu kuzungumza kama habari ya kumtoa PM, kuongeza muda wa bunge ili tusilaze gumzo hili kiporo si jambo baya.
 
Hivi Kikwete ni mwenyekiti wa kamati ya mazishi afrika? Kutokana na uzito wa matatizo ya nchi yake alitakiwa amtume mwakilishi, mbona nchi zingine zimetuma balozi zao? Kwanini iwe ngumu kwa jk?

Hawezi kukosa misiba kama huo, si unamjua hata akiwa nyumbani? Misifa apewe mwingine? Hataki rekodi yake ya kwenda misibani ivunjwe na yeyote! Anajua naye kuna siku atahitaji dunia nzima ishuhudie anavyozikwa na ili litimie lazima ajulikane kila kona ya dunia kwamba ni mtu wa wafu.
 
ni mratibu wa mazishi ya watu mashuhuri
 
ccm inashindwa kuchukua maamuzi magumu, hii inankumbusha ya gadafi. Mwalimu wangu alipenda kusema "dying without bitterness"
 
kwa hali ilipofikia kwa sasa ilibidi kuahirisha misafari isiyo na tija
 
Hawezi kukosa misiba kama huo, si unamjua hata akiwa nyumbani? Misifa apewe mwingine? Hataki rekodi yake ya kwenda misibani ivunjwe na yeyote! Anajua naye kuna siku atahitaji dunia nzima ishuhudie anavyozikwa na ili litimie lazima ajulikane kila kona ya dunia kwamba ni mtu wa wafu.
Masharti aliyopewa na mnajimu wake ni kutoshindwa kuhudhuria misiba. Hivyo wananchi muelewe si matakwa yake, ni masharti ya kiganga.
 
Wabunge wa JMT wametoa maonu yao iwapo leo Spika wa Bunge hataipangia na kuipokea hoja ya Zitto ya kumwajibisha PM kwa dhana nzima ya uwajibikaji na kulindana.

Wameomba kuwepo na bunge la dharura kulingana na sheria na taratibu za bunge kwa sababu kuwaacha waendelee mpaka vikao vijavyo ni kuliua taifa.

Pia wabunge hao wanadai ni unafiki na uwongo kuwa rais hana taarifa ya mambo yanayojiri bungeni kama hajui iweje ajibu akiwa Malawi kama hana taarifa?

Wanafiki, mbona wameogopa kusaini hati ya Zito. Hopeless people!!!
 
Hivi Kikwete ni mwenyekiti wa kamati ya mazishi afrika? Kutokana na uzito wa matatizo ya nchi yake alitakiwa amtume mwakilishi, mbona nchi zingine zimetuma balozi zao? Kwanini iwe ngumu kwa jk?

hujui kuwa hiyo ndio staili yake ya kukwepa majukumu na lawama? Anajaribu kujikipu bize kwa mambo yasiyokuwa na tija. Anajaribu kutengeneza sababu kuwa anachelea kuwawajibisi makuwadi wake huku akisikilizia upepo. Kama umemshtukia huyu jamaa huwa anaogopa kuwa wa kwanza kufanya maamuzi kutokana na uwezo wake mdogo. Kifupi ni kwamba pale IKULU hapakustahili kukaliwa na mtu Kilaza hv. Matokeo yake ndio haya tunayoshuhudia sasa.
 
Kwa wale wabunge wa ssm waliosaign basi ni mashujaa wetu wa mwezi jamani manaona je

Habari nzima ya ushujaa ni uzushi tu, waache watu wafanye kazi zao. Hata wakulima wanaokupa chakula kwa msingi huo ni mashujaa.

Tuache kuendekeza tamthiliya.
 
Amefanya vizuri bora mawaziri hao asiwatoe ili aone sisi tutamfanya nini. Hizi ni kelele za chura.........
 
Hivi Kikwete ni mwenyekiti wa kamati ya mazishi afrika? Kutokana na uzito wa matatizo ya nchi yake alitakiwa amtume mwakilishi, mbona nchi zingine zimetuma balozi zao? Kwanini iwe ngumu kwa jk?

Anaenda kuuza sura tu,huwa haoni matatizo kwenye nchi yake huyo,lakini akisikia Kenya kuna shida,atakuwa wa kwanza kufika
 
Wabunge wa JMT wametoa maonu yao iwapo leo Spika wa Bunge hataipangia na kuipokea hoja ya Zitto ya kumwajibisha PM kwa dhana nzima ya uwajibikaji na kulindana.

Wameomba kuwepo na bunge la dharura kulingana na sheria na taratibu za bunge kwa sababu kuwaacha waendelee mpaka vikao vijavyo ni kuliua taifa.

Pia wabunge hao wanadai ni unafiki na uwongo kuwa rais hana taarifa ya mambo yanayojiri bungeni kama hajui iweje ajibu akiwa Malawi kama hana taarifa?

hapo sasa nafurahia uzalendo wa wabunge wetu ila wakileta itikadi ya vyama vyao bora wananchi tukinukishe kwa maandamano tu.
 
Hivi Kikwete ni mwenyekiti wa kamati ya mazishi afrika? Kutokana na uzito wa matatizo ya nchi yake alitakiwa amtume mwakilishi, mbona nchi zingine zimetuma balozi zao? Kwanini iwe ngumu kwa jk?

Anapenda outing!!!!!
 
Back
Top Bottom