Wabunge wanaweza kumfukuza spika

MLO

Senior Member
Apr 2, 2012
197
84
Inaonekana kuwa spika wa bunge ANNA MAKINDA hana msaada kwa taifa leta.Amekuwa ni mlinzi wa wa masilahi ya chama chake.Kwa taarifa za kamati za bunge alitakiwa kuwa mstari wa mbele kulinda maslahi ya Taifa badala ya anachokifanya sasa.
Je yeye haoni makosa yaliyofanywa na Mawaziri?
Je kama muda hautoshi tuache Mawaziri watutafune?
Wabunge tumieni ifungu hiki cha katiba
84.-(1) Kutakuwa na Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa na
Wabunge kutoka miongoni mwa watu ambao ni Wabunge au
wenye sifa za kuwa Wabunge; atakuwa ndiye kiongozi wa Bunge
na atawakilisha Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje
ya Bunge.
(2) Waziri, Naibu Waziri au mtu mwenye madaraka ya aina
nyingine yoyote itakayotajwa na Sheria iliyotungwa na Bunge kwa
madhumuni ya ibdara hii, hataweza kuchaguliwa kuwa Spika.
(3) Mtu yeyote atakayechaguliwa kuwa Spika atatakiwa, kabla
ya kumaliza siku kumi na tano tangu kuchaguliwa kwake,
kuwasilisha kwa Rais tamko rasmi kwamba hajapoteza sifa za
uchaguzi kwa mujibu wa masharti ya aya ya (d) ya ibara ndogo ya
(2) ya ibara ya 67. Tamko hilo litatolewa kwa kutumia fomu
maalum itakayowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na
Bunge.
(4) Rais atawasilisha kwa Kamishna wa Maadili nakala moja
ya kila tamko rasmi lililowasilishwa kwake kwa mujibu wa masharti
ya ibara ndogo ya (3) ya ibara hii.
(5) Spika atatakiwa kuwasilisha kwa Rais nakala mbili za
taarifa rasmi ya maelezo ya mali ya huyo Spika na, kadri
itakavyokuwa, mali ya mke au mume wake. Spika atatoa taarifa
hiyo kwa kutumia fomu maalum iliyowekwa kwa ajili hiyo kwa
mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge na atatoa taarifa ya
namna hiyo mara kwa mara kadri itakavyoagiza sheria hiyo.
(6) Masharti ya ibara ndogo ya (2) na ya (3) ya ibara ya 70
yatatumika pia, kwa kadri itakavyowezekana, kwa taarifa ya mali
yoyote itakayotolewa na Spika, kwa mujibu wa masharti ya ibara
hii.
(7) Spika atakoma kuwa Spika na ataacha kiti cha Spika
litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo -

(a) iwapo mtu huyo alichaguliwa kutoka miongoni mwa
Wabunge, basi ikiwa atakoma kuwa Mbunge kwa
sababu yoyote ambayo haihusiki na kuvunjwa Bunge;
au
(b) ikiwa kutatokea jambo lolote ambalo, kama
asingekuwa Spika, lingemfanya mtu huyo asiwe na
sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi wa
Spika; au
(c) Bunge litakapokutana kwa mara ya kwanza baada ya
Uchaguzi Mkuu uliofanywa baada ya Bunge kuvunjwa,
lakini masharti ya aya hii yatatumika bila ya kuathiri
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
64
masharti ya ibara ndogo ya (4) ya ibara ya 90 ya
Katiba hii; au
(d) ikiwa mtu huyo ataondolewa kwenye madaraka ya
Spika kwa azimio la Bunge lililoungwa mkono na
Wabunge amabo idadi yao haipungui theluthi mbili ya
Wabunge wote; au

(e) ikiwa mtu huyo atashindwa kuwasilisha kwa Rais
tamko rasmi kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo
(5) ya ibara hii; au
(f) ikiwa mtu huyo atapatikana na hatia kwa kosa la kutoa
habari za uongo, kwa kiapo kinyume cha sheria ya
Kanuni ya jinai, kuhusu tamko rasmi lolote lililotolewa
kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) ya ibara
hii; au
(g) ikiwa mtu huyo atashindwa kuwasilisha kwa Rais
taarifa ya mali kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo
ya (5) ya ibara hii kabla ya kumalizika muda uliowekwa
kwa ajili hiyo kwa mujibu wa sheria iliotungwa na
Bunge;
(h) ikiwa itathibitika kuwa mtu huyo amevunja masharti ya
Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(8) Hakuna shughuli yoyote itakayotekelezwa katika Bunge
(isipokuwa uchaguzi wa Spika) wakati wowote ambao kiti cha
Spika kitakuwa ki wazi.
(9) Mtu yeyote ambaye si Mbunge atakayechaguliwa kuwa
Spika, atatakiwa, kabla ya kuanza kutekeleza madaraka yake,
kuapishwa katika Bunge kiapo cha uaminifu.
 
Back
Top Bottom