Wabunge wanapaswa kumuondoa spika kabla ya waziri mkuu

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
[h=3]Chanzo;mpayukaji blog[/h]
AnnaMakinda.jpg


Hakuna ubishi kuwa spika wa Bunge Anna Makinda ni changuo la mafisadi. Ushahidi ni kushindwa kujibu tuhuma hizi ziliporushwa na spika wa zamani Samuel Sitta baada ya kuenguliwa na kusimikwa Makinda. Kwa kutojibu Makinda alithibitisha ukweli wa tuhuma dhidi yake.
Makinda amekuwa kikwazo kwa heshima na uhuru wa bunge. Rejea alivyomzuia mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema alipodai kuwa waziri mkuu Mizengwe Pinda ni muongo. Si hilo tu, amekuwa akiliburuza bunge kutokana na kutokuwa na taaluma ya sheria. Karibu mabunge yote ya Afrika Mashariki isipokuwa la Tanzania, yanaendeshwa na maspika wenye taaluma ya sheria.
Ukiachia hilo, Makinda amekuwa mtu wa jazba na kiburi kiasi cha kujiona ni bora kuliko bunge. Sasa kwa kuzuia Zitto Kabwe alilete hoja ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu, kwa mara ya pili Makinda amethibitisha alivyo kibaraka wa waziri mkuu na mhimili mzima wa utawala. Kisheria mihimili mitatu ya dola yaani Utawala, Bunge na Mahakama havipaswi kuingiliana au kuzidiana mamlaka katika utendaji wake. Huu ndiyo msingi wa kwanza wa utawala bora.
Je kwanini wabunge wasimwajibishe Spika ambaye ameonyesha wazi kuwa mtetezi wa uoza, ukale na ufisadi?
 
Amefurahije Lema kuvuliwa ubunge? Tungekuwa na Spika makini PM angejiuzulu tangu wakati wa Lema.
 
Huu ni ukweli usiopingika haka kamama hebu kaondolewe kwanza halfu ndo tuje kwa mtoto wa mkulima,maana kuendelea kukakumbatia bungeni ndo maana kanazidi kuvurunda mambo makini Bungeni tuanze nako kwanza wazee.
 
Nasikia wasira amepeleka posa

jamani mi ni mgeni kwenye jamvi hli ila ukweli ni kwamba hii serikali imefikia pabaya sasa yani ni sawa ufumaniwe ukiwa uchi halafu useme sikuwa nataka kufanya lolote.. Haka kamama hta mimi kananiudhi..yani labda ampate huyo wasira otherwise hta hzo yebo yebo asuke za gold atabaki hivyo hivyo watu kabaya kama roho yake
 
mmheshuhudia wenyewe rais bingu wa mutharika marehemu sasa alivowatesa wamalawi sasa yuko wapi?
alijisahau akajiona yeye ndie Mungu mtu wa Malaw. Ghadaffi licha ua utajiri aliokuwa nao na dhuluma zote alibomoa makanisa na kujenga misikiti alinyima wakristo uhuru wa kuabudu lkn Mungu alimtia kiburi watu wake wakamwangamiza
na hata kumuanika yeye na mwanae kama mzoga ili kila mtu amshuhudie kinyume kabisa na imani ya waislam kutoruhusu maiti kutazamwa.
kwa tanzania nako mda sio mrefu kilio chetu kitasikilizwa ameshaanza kuwachanganya wao kwao
mwishoni wataangukia matumbo yao nchi itatwaliwa na wanaompendeza Mungu kwa manufaa ya watu wake
hao wanaotunyima rasilimali zetu na kulindana siku zao zimeshaanza kuhesabika
 
Huwa najiuliza hili swali hasa nikiangalia linavyoondeshwa na Makinda najiuliza hivi pamoja na kuangalia kanuni zinafuatwa na mbunge akikosea ni kama anamsubiria akosee asitelekeze alichotarajia kukifanya hasa inapokua linahusu serikali.

Bila maelekezo ya kujenga anang'ang'ania kukosoa na kukwamisha. Mimi napata taabu kweli kweli kuelewa
 
Yule bibie yuko upande wa waliomweka pale. Hakustahili ile nafasi ila kuna waliomweka pale, na hao ndio mabosi wake.
 
Back
Top Bottom