Wabunge wanaotuhumiwa kwa rushwa wavuliwe nyazifa!!

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,575
8,594
Kutokana na kashifa ya wabunge kutuhumiwa na kwa kashfa za rushwa bassi hawanabudi kuachia nyadhifa zao mara moja,Kutokana wao wameaminiwa na wananchi na vyama vyao kuwawakilisha kwenye bunge tukufu la JMT,basi wameshindwa kuwatumikia sasa wanatakiwa wajiudhuru nyadhifa zao za ubunge...lasivyo vyama vyao viwavue uananachama!Kwakuwa wametia aibu kubwa kwa Bunge tukufu ambalo ni muhimili wapili nchini!Nakatika vyama wanavyotoka pia Mbunge anatakiwa kuwa msafi!asiye na ukwasu wowote!!.Hapa tulipofika nikwasababu ya hawahawa wabunge walafi kwakukiuka maadili wakati wao ndiyo wanaosimamia maadili!!Je kama wao wanayavunja je wanaowaongoza watafanya nini???..Kitu ambacho sikifahamu ni pale mbunge anapokutwa na hatia ya kula rushwa je Bunge linamchukulia hatua gani??Je bunge linao uwezo wakufukuza Mbunge mwenye kashfa ya rushwa bungeni??au kumvua ubunge?...Kama ndiyo nibora sasa bunge lifanye kazi yake, hatuwezi kuendelea kubeba msalaba mzito uliochongeshwa na wabunge walafi!!Kwakutozingatia viwango vya msalabba!!
 
Back
Top Bottom