Wabunge wanaoamini MAGEUZI kufanya mkutano na waandishi saa tisa alasiri leo hii!

We can stop people but not time...Muda wao umefika mapema kuliko walivyodhani afadhali nao weekend zao ziwe chungu
 
Hii hoja lazima ipelekwa kufundisha watu uwajibikaji na mamlaka ya bunge, mambo ya party caucus kufanya maamuzi ya kitaifa badala ya bunge lazima yakomeshwe, wananchi hatuchagui wabunge wa vyama tunachagua wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania!
 
Zitto fanyeni kweli,4 the seek of the nation makinda kesho akikataa apigwe pale na ang'olewe kwa mabavu kama ukraine then naibu spika Ndugai..aweke hoja mezani
Makinda atakataa kwa grounds zipi, labda atumie nguvu ambayo itaonekana wazi. Kama kanuni zinavyosema kazi yake ni kupokea hoja endapo itakuwa imesainiwa kwa 20% ya wabunge waliopo. Kazi ya kutaa hoja si ya spika ni ya wabunge watakaopiga kura. Labda kinachotakiwa kama serikali inataka kuikataa hoja ijipange ili kura zisifike 50% +1.
 
tupe updates au ulikuwa unatikisa kiberiti mkuu mbona kimya ikiwezekana weka hilo tamko lenu hapa tulisome
 
On behalf of the mentioned ministers and on behalf of the Gvt,Mr. PM should be held accountable to this matter unless otherwise the respective ministers have to step out to rescue the PM

And if the ministers do not want to take actions seriously by themselves and wait for their boss to resign for their malipractices,it will be certainly taken as a total sacrifice of their boss in terms of the hierachy and seniority.

Hatuwezi kuyaacha yote2 pasipo kufanyika ila ni bora zaidi hata yote2 yakafanyika kama si mojawapo.

Watanganyika it's now dawn,hold yr breaths for the battle.
 
Zitto aje jf atamuachia nani fb na tweeter?
hatupi ushirikiano tuliouzoea, mpaka tumpekuepekue huko mitandaoni tupate cha kulumbana!!!!!!! kumbukeni magamba hawaipendi jf, kwa kumbukumbu zenu niambieni zitto kachangia mada jf mara ya mwisho lini? zitto ni mzito, mchungueni vema.
 
On behalf of the mentioned ministers and on behalf of the Gvt,Mr. PM should be held accountable to this matter unless otherwise the respective ministers have to step out to rescue the PM

And if the ministers do not want to take actions seriously by themselves and wait for their boss to resign for their malipractices,it will be certainly taken as a total sacrifice of their boss in terms of the hierachy and seniority.

Hatuwezi kuyaacha yote2 pasipo kufanyika ila ni bora zaidi hata yote2 yakafanyika kama si mojawapo.

Watanganyika it's now dawn,hold yr breaths for the battle.
 
On behalf of the mentioned ministers and on behalf of the Gvt,Mr. PM should be held accountable to this matter unless otherwise the respective ministers have to step out to rescue the PM

And if the ministers do not want to take actions seriously by themselves and wait for their boss to resign for their malipractices,it will be certainly taken as a total sacrifice of their boss in terms of the hierachy and seniority.

Hatuwezi kuyaacha yote2 pasipo kufanyika ila ni bora zaidi hata yote2 yakafanyika kama si mojawapo.

Watanganyika it's now dawn,hold yr breaths for the battle.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
HOJA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU BUNGENI KWA MUJIBU WA KATIBA IBARA YA 53A NA KANUNI YA BUNGE, KIFUNGU CHA 133 KUWASILISHWA KWA SPIKA KESHO TAREHE 23/04/2012

· Masharti yametimizwa; wabunge 73 wazalendo wamesaini

· Ni mwendelezo wa ‘Operesheni Uwajibikaji'

Mnamo tarehe 19/04/2012 wakati nahitimisha hoja ya Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma nilieleza kusudio langu la kuwaomba waheshimiwa wabunge waniunge mkono katika kutia saini zisizopungua asilimia 20 ya wabunge wote ili kuweza kutimiza matakwa ya Katiba ibara ya 53A kwa ajili ya kuwasilisha Bungeni hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.

Mnamo tarehe 20/04/2012 niliandaa orodha ya waheshimiwa wabunge wote na kuisambaza ndani na nje ya ukumbi wa Bunge ili waheshimiwa wabunge wote waweze kutia saini hizo, na mpaka leo tarehe 22/04/2012 orodha hiyo imetimiza idadi ya wabunge wazalendo wanaopigania uwajibikaji 73 kutoka vyama vyote vyenye uwakilishi Bungeni, isipokuwa chama cha UDP ambacho kina Mbunge 1 na hajatia saini waraka huo mpaka sasa.

Kwa mujibu wa kanuni za Bunge kifungu cha 133 (1) kinasomeka "Mbunge yeyote anaweza kutoa taarifa ya maandishi kwa Spika ya kutaka kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa mujibu wa ibara ya 53A ya Katiba" na kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (3) kinasomeka "hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu haitajadiliwa na Bunge isipokuwa tu kama;

(a) "taarifa ya maandishi iliyowekwa saini na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia 20 ya wabunge wote itatolewa kwa Spika, siku zisizopungua kumi na nne kabla ya siku inayokusudiwa kuwasilishwa Bungeni;"

Hali kadhalika kanuni za Bunge Kifungu cha 133 (4) kinasomeka kuwa "hoja inayotolewa chini ya Kanuni hii na iliyotimiza masharti ya Katiba,itawasilishwa Bungeni mapema iwezekanavyo na itaamuliwa kwa kura za siri".

Hivyo basi baada ya kutimiza matakwa ya kikatiba na kanuni za Bunge kesho tarehe 23/04/2012 tutawasilisha rasmi kwa Spika Taarifa ya Maandishi kwa mujibu wa kanuni 133 (1) na (3) ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa kushindwa kusimamia uwajibikaji wa Serikali Bungeni kwa mujibu wa ibara ya 52 na hivyo kulinda Mawaziri wenye kusababisha matumizi mabaya ya fedha za umma na kulisababishia hasara taifa.

Tunatarajia kwamba siku kumi na nne baada ya kuwasilisha hoja hiyo Bunge litakutana kwa haraka kujadili hoja hiyo ili kuwezesha uwajibikaji na hatua kuchukuliwa za kuhakikisha mapendekezo ya ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na maazimio ya Bunge yanatekelezwa. Hoja hii ni mwendelezo wa 'Operesheni Uwajibikaji' hivyo tunaomba wabunge wazalendo na watanzania wote waiunge mkono ili kuimarisha Uwajibikaji wa Viongozi, kupambana na ubadhirifu na kunusuru uchumi wa nchi na kuchangia katika ustawi wa wananchi.

Kwa niaba ya wabunge wazalendo waliotia saini kuunga mkono taarifa ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ni;
…………………………….
Kabwe Zuber Zitto.
Mbunge Jimbo la Kigoma Kaskazini.
22/04/2012.
 
Lisilowezekana kwa wanadamu kwa mungu linawezekana naamini tusihofu kesho hoja iwasilishwe mama na mahasira yake apasuke situpo
 
Back
Top Bottom