Wabunge walipwe mishahara kutokana na elimu zao.

Ta Kamugisha

JF-Expert Member
May 17, 2011
3,536
2,187
Wana jf mnaonaje wabunge wetu nao walipwe kutokana na elimu zao, hapo ndo heshima itarudi, maama hii ya kulipwa mil 10 hata kama ni darasa la 7 ndo kinapelekea hawa wabunge wetu washindwe kuwaheshimu wasomi. naomba kuwasilisha.
 
Una utani na Prof Maji Marefu eeh?
Hivi komba nae ni graduate wa nini?

Te te te! kama darasa la 7 atalipwa mshahara wa muhudumu, yaani kima cha chini. itapendeza sana na watakuwa serious kutetea hoja kwa nguvu zao
 
basi lusinde atapokea 70,000/= ya darasa la saba..ooh almost forgot na lukuvi pia

Dah! kaz kweli kweli, hapo nadhani atawatetea watu wanaopokea kima cha chini, iweje prof maji marefu alipwe vzr kuliko madaktari?
 
Kwani elimu ndiyo nini? Kusoma na kuelimika ni vitu tofauti. Kwanza hakuna shahada ya ubunge kisha hata hao mnaodhani wamesoma mbona wengi wao ni pumba tupu? Mwanawane uongozi ni kipaji pia inategemea sana na busara na uzalendo ulionao hasa katika kazi ya siasa. Haohao wenye madigirii ndio waliouza nchi yetu nma kutufanya tuishi maisha magumu sasa hivi
 
Elimu sio kigezo pekee ya kiwango cha mshahara makazini,,,,,, kuna elimu, ujuzi, maarifa kazini (ubunifu) nk.

katika uchaguzi wa 2010 kama chadema wangechukua nchi kwa sasa tungekuwa na makamu wa Rais darasa la saba labda walizingatia na vigezo vingine
 
We kweli ni rohombaya! ila kiukweli tunaitaji wabunge wasomi, watakao weza kusoma mikataba
 
nambie mwenye elimu ya darasa la 7 na ana ujuzi na maarifa na anapokea mshahara wa kuanzia milioni
 
We kweli ni rohombaya! ila kiukweli tunaitaji wabunge wasomi, watakao weza kusoma mikataba
bado hujanielewa! Mbona hiyo mikataba yote ya kifisadi mbona imesainiwa na haohao wenye madigirii?????? hapa ishu si kuwa na madigirii (kusoma) ishu ni kuwa na uelewa (Kuelimika). kuelimika siyo lazima kwenda darasani ndugu. Tena madarasa yenyewe ya kibongo hapa buree kabisa. Tusiwabague watu kwa kutumia vyeti vyetu katika kazi zi kisiasa.
 
Wana jf mnaonaje wabunge wetu nao walipwe kutokana na elimu zao, hapo ndo heshima itarudi, maama hii ya kulipwa mil 10 hata kama ni darasa la 7 ndo kinapelekea hawa wabunge wetu washindwe kuwaheshimu wasomi. naomba kuwasilisha.

Mishahara ya vyeo vya kisiasa mara nyingi haifuati elimu. Kinachoangaliwa ni cheo cha kisiasa anachokuwa nacho mhusika, mfano Mkuu wa Wilaya, Mbunge n.k. Mkifanya makosa wapiga kura mkamchagua DARASA LA SABA OYEE kuwa Mbunge, moja kjwa moja mmempa mshahara wa mbunge! Hoja ni kwamba bora Elimu ya chini kwa mgombea ubunge ibainishwe na ifuatiliwe! Nayakumbuka ya KIHIYO wa Temeke, kumbe bado kuna "VIHIYO" wengi katika bunge!
 
Kama wanahusika kupitisha mikataba na bajeti ya nchi,elimu ni muhimu sana!
 
na kuchangia kwa mantiki kufute elimu zao??? maana tunawalipa kwa michango yao kwa umma sio elimu yao; labda walipwe kwa kuchangia bungeni na kuwasilisha hoja maoni mbadala.
 
Back
Top Bottom