Wabunge wakerwa na wasanii wa kiume kuvaa kike

Wabunge wameonyesha kuchukizwa kwao na wasanii wa kiume kuvaa kike kwa kupaka wanja, lipsticks na kuvaa nguo za kike wanapoigiza.

Waziri ameomba wakanywe kwakuwa wanadhalilisha wanawake. Kasema wasitengeneze hela kwa kudhalilisha wanawake.

Waziri kataka mamlaka husika kulifuatilia hili na kutafuta njia ya kutatua.

Wabunge hao wasibwatuke kabla ya kuhojiana na wakufunzi wa Sanaa mbalimbali. Hiyo kwenye sanaa inakubalika na ndo maana hata enzi zile kabla wanawake hawajawa na mwamko wa kuimba muziki; wanaume walikuwa wakiigizia sauti ya kike ili ujumbe uwafikie walengwa. Sanaa ni uwanja mpana waelewe hilo!
 
yule muimba hip hop wa mbeya vip? huwa hatumii mkorogo?
Sijui kama anatumia, mbona sura yake ngumu kama ya mwanamume yeyote shupavu? ila nadhani huu ni mwanzo mzuri tukimaliza wana-Music twende na Bungeni kuna uvumi kwamba kuna baadhi ya wabunge wakike wana vaa vikuku bungeni kiasi kwamba inakuwa vigumu sana kuwaonya watoto wa form two wasivae vikuku kwani wanadai vikuku ni kitu cha heshma hata bungeni huvaliwa, mimi sina uhakika kama kuna mbunge anaweza kuvaa kikuku Bungeni huu utakuwa ni uzushi.
 
Wabunge wameonyesha kuchukizwa kwao na wasanii wa kiume kuvaa kike kwa kupaka wanja, lipsticks na kuvaa nguo za kike wanapoigiza.

Waziri ameomba wakanywe kwakuwa wanadhalilisha wanawake. Kasema wasitengeneze hela kwa kudhalilisha wanawake.

Waziri kataka mamlaka husika kulifuatilia hili na kutafuta njia ya kutatua.
Yaa hii kali, katika kipindi hiki ambapo maisha magumu yanawazonga Watanzania na shiringi kupoteza thamani yake, kiongozi anaamua kujikita zaidi na kufuatilia mavazi ya wanamziki.
 
Elimu ndogo ya mbunge kwenye sanaa ukitaka kufikisha ujumbe fulani kwa jamii ni lazima uhuvae uhusika halisi ,unaigiza nafasi ya mke alafu una madevu wapi na wapi?
 
Yaa hii kali, katika kipindi hiki ambapo maisha magumu yanawazonga Watanzania na shiringi kupoteza thamani yake, kiongozi anaamua kujikita zaidi na kufuatilia mavazi ya wanamziki.

Yaani hapo mi ndio nachoka kabisa, ndio walichofuata huko mjengoni hicho, kuna issues nyeti sasa hivi za kutatua wao wameona mavazi ya kuigizia jamani, tuwaiteje hawa?
 
Ccm na Cuf ni ndoa ya jinsia moja.
WASANII WANAOWADHALILISHA WANAWAKE NDIO HAO WALIOKUWA IGUNGA KUISADIDIA CCM ISHINDE LEO WANAWAPONDA MBONA HAWAKUWAONA WAKATI WA KAMPENI NA KUWATEMA??KWELI CCM NI GAMBA LA MAGAMBA YAANI LEO BLUU KESHO NYEUSI HAYA JOTI NA WENZAKO HAMIENI CUF SASA MAANA CUF NA CCM NI MTU NA NYUMBA NDOGO

kazi kwenu
 
Unasemea huyu! Kuna dalili ya mkorogo hapo? EPEAN Wenu ndio anapaka mkorogo.

sugu-1.jpg

Aaaaah!!!SUGUUUUUU
 
Wabunge wameonyesha kuchukizwa kwao na wasanii wa kiume kuvaa kike kwa kupaka wanja, lipsticks na kuvaa nguo za kike wanapoigiza.

Waziri ameomba wakanywe kwakuwa wanadhalilisha wanawake. Kasema wasitengeneze hela kwa kudhalilisha wanawake.

Waziri kataka mamlaka husika kulifuatilia hili na kutafuta njia ya kutatua.
Waache ujinga,kuigiza ni kipaji!

Kwani hawajui kuna watu (wanaume) wanaweza kuigiza kama wananwake kuliko hata wanawake wenyewe?

Muigizaji wa kweli huweza kuigiza nafasi yoyote ile bila shida.

Wameona big momma's house jinsi Martin Lawrence alivyoweza kuigiza?

Kwani ina maana Martin ana tabia za kike?

Kama hawajui mana ya sanaa ya ugizaji wakae kando!

Unless mnasema kuwa hizo ndo tabia zao yaaani kuvaa na kujipodoa kama mademu,ila kama it was a role in a movie,sioni shida!

Hawana kazi wabunge.Watanzania mtakoma kuchaguwa maboga!
 
Wabunge wameonyesha kuchukizwa kwao na wasanii wa kiume kuvaa kike kwa kupaka wanja, lipsticks na kuvaa nguo za kike wanapoigiza.

Waziri ameomba wakanywe kwakuwa wanadhalilisha wanawake. Kasema wasitengeneze hela kwa kudhalilisha wanawake.

Waziri kataka mamlaka husika kulifuatilia hili na kutafuta njia ya kutatua.

SIKUTARAJIA MH WAZIRI TENA MWENYE ELIMU NA SURA NZURI KUONGEA MAMBO YA OVYO KAMA HAYO. WMAUME WANAIGIZA NGUO ZA KUBANA UNASHANGAA BADALA YAKUSHANGAA WANAWAKE WAKITEMBEA MAZIWA NJE KWANI TWAYATAKA? MAMA YANGU ANA MAZIWA NA HULIFICHA JAPO NILINYONYA, NINI HAJA YA MAZIWA YA WANAWAKE AMA WASICHANA WA TZ? NGUO ZIMEBANA NA KTK HILI WAZIRI HUKEMEI WASICHANA WAKIVAA HIVYO, UNAKERWA NA WANAUME? nANI HANA MAPAJA? NANI KASEMA LAZIMA TUTEMBEE BARABARANI TUKILINGANISHA MAPAJA YA WANAWAKE? KAMA ISSUE NI MAPAJA HATA NG'OMBE ANAYO.

TUMIA ELIMU YAKO NA UZURI WAKO MH WAZIRI KUKEMEA WANAWAKE NA WASICHANA WANODHANI MAPAJA AU MAZIWA YAO NA AMBAYO WAKATI MWINGINE MTU HAKUMBUKI KAMA ALIUGUA UPELE KABLA NA MAKOVU HAYAJAWI FUTIKA
 
Waende sambamba na kuwabana wanawake wanaovaa nguo za kiume,tena ndo weng zaid..wanawadhalilisha wanaume!!kwel wazir kachoka
 
Mh, jamani! hivi maana ya UIGIZAJI NI NINI? Kwa mtazamo maana yake ni kutoka kwenye hali yako halizi na kuvaa uhalisi wa mtu mwingine na lengo linaweza kua kuelimisha, kuburudisha au kukosoa. Kweli sasa hao wabunge wamekosa vya kujadili. Sioni tatazo la wasanii waigizaji wa kiume kuvaa nguo za kike na wale wa kike kuvaa za kiume.
 
Wabunge wameonyesha kuchukizwa kwao na wasanii wa kiume kuvaa kike kwa kupaka wanja, lipsticks na kuvaa nguo za kike wanapoigiza.

Waziri ameomba wakanywe kwakuwa wanadhalilisha wanawake. Kasema wasitengeneze hela kwa kudhalilisha wanawake.

Waziri kataka mamlaka husika kulifuatilia hili na kutafuta njia ya kutatua.

Hivi hawa wabunge wanaelewa maana ya sanaa na usanii?! Sidhani, kama wangekua wanaelewa wasingesema kuna udhalilishaji!!
 
Hivi hawa wabunge wanaelewa maana ya sanaa na usanii?! Sidhani, kama wangekua wanaelewa wasingesema kuna udhalilishaji!!
Nawashangaa kweli,na ukiigiza kama jambazi kwenye movie utakamatwa kama ni that serious?Uelewa wa wengi wa viongozi wetu ni wa mashaka sana.

Kam hawaelewi issue ndogo kama hii, issues za kitaifa watazielewa kweli hawa?
 
Zege limeisha, na sasa karai linaonekana ni uchafu. Poleni Ze Original Comedy!
 
Hao Ze Komedi lazima wana element za ushoga siyo bure, waendelee tu Cameruni anaweza kuwapa ufadhili.
 
Wabunge wameonyesha kuchukizwa kwao na wasanii wa kiume kuvaa kike kwa kupaka wanja, lipsticks na kuvaa nguo za kike wanapoigiza.

Waziri ameomba wakanywe kwakuwa wanadhalilisha wanawake. Kasema wasitengeneze hela kwa kudhalilisha wanawake.

Waziri kataka mamlaka husika kulifuatilia hili na kutafuta njia ya kutatua.

Nadhani yako mambo mengi ya kushughulikia ambayo ni muhim; itakuwaje pale ambapo msanii atataka kuigiza kama mgonjwa hivyo aende Muhimbili kupata mgonjwa halisi? au kuigiza kama kichaa atafutwe mtaani kicha halisi? mambo mengine madogo sana hayana mshiko.
 
Kazi ya sanaa haitakiwi kuwekewa vikwazo, wabunge watuache tuichambue na kuifurahia au kuichukia sanaa bila kuingiliwa na wabunge wapuuzi. Sanaa inaitwa sanaa kwa sababu ni sanaa(kubuni).Mbunge mkware afie mbali.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom