Wabunge wakerwa na wasanii wa kiume kuvaa kike

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,871
Wabunge wameonyesha kuchukizwa kwao na wasanii wa kiume kuvaa kike kwa kupaka wanja, lipsticks na kuvaa nguo za kike wanapoigiza.

Waziri ameomba wakanywe kwakuwa wanadhalilisha wanawake. Kasema wasitengeneze hela kwa kudhalilisha wanawake.

Waziri kataka mamlaka husika kulifuatilia hili na kutafuta njia ya kutatua.
 
Huyo Waziri ni mnafiki.

Wasanii wenyewe wanaopaka Lipshine na kuvaa hereni na majeans ya kike na wengine kuigiza kama wanawake ni walewale ambao mwaka jana walikuwa na CCM bega kwa bega kuhakikisha Ushindi wa TSUNAMI unapatikana. Kwanini hawakuelezana huko huko?
 
Hoja hii nadhani haitawagusa Ze komedi kwani ni kundi linaloisaidia CCM katika kampeni
 
Serikali imesema itaongea na basata ili kuhakikisha vikundi ambavyo vinawashilikisha wanaume kuact kama wanawake vitafute wasichana wa kuact sehemu husika.

Inasema hii hali inadhalilisha wanawake na hii inapelekea kushamili kwa haya mambo ya ushoga kushamili. Selikali hainasheria kuhusu uvaaji wa mtanzania bali mila zetu ndo zinatuongoza.

MY TAKE;
hapa mimi naona wananza kuwasakama wasanii wa komedi wa Tanzania wakima mtanga na masanja.mia
 
WASANII WANAOWADHALILISHA WANAWAKE NDIO HAO WALIOKUWA IGUNGA KUISADIDIA CCM ISHINDE LEO WANAWAPONDA MBONA HAWAKUWAONA WAKATI WA KAMPENI NA KUWATEMA?

KWELI CCM NI GAMBA LA MAGAMBA YAANI LEO BLUU KESHO NYEUSI HAYA JOTI NA WENZAKO HAMIENI CUF SASA MAANA CUF NA CCM NI MTU NA NYUMBA NDOGO

Kazi kwenu
 
Hawa wa Heshimiwa Wabunge wasiigombee hii hoja na kuifanya suala la kujadiliwa sanaa!!! Wasanii wa kike wana-act kama wanaumme hakuna malalamiko........

Wabunge wajue kuna na rehersal ya U-CAMERON...Bila kufanya zoezi la kuigiza jinsia isiyo yako ni ngumu maagizo ya UK kutekelezeka:)
 
wanaota ndoto za mchana hawa hiyo ni sanaa lazima ifanye reflection ya mambo ya jamii .hii ni njia ya kuuwa sanaa wanaacha watu wanaofanya sanaa uchi wanapambana na watu smart huyu waziri hazimtoshi
 
Sasa naona wanataka kuingilia maslahi ya CCM hawajui kuwa CCM ndiyo inayofadhili kina Joti na wenzake wajichubue ili iendelee kutawala nchi?
 
wamekosa cha kufikiria. hili limeshaitwa kuwa ni usanii na mtu yeyote anaweza kuigiza chochote wakati wowote!
Kwa nini wasishughulikie maslahi yao kwanza na wezi wa kazi zao!?
 
Mbona hawasemi tunapoelekezwa na WASHIKA KIBABA tukubali ushoga??? Au huo kwao ni poa issue wasiyotaka ni wasanii kuuigiza jinsia ingine??? Ipi bora kuigiza tuu au kubeba msalaba wa MAJUKUMU YA KIMWILI ya jinsia hiyo???
 
yule muimba hip hop wa mbeya vip? huwa hatumii mkorogo?
Unasemea huyu! Kuna dalili ya mkorogo hapo? EPEAN Wenu ndio anapaka mkorogo.

sugu-1.jpg
 
Binafsi nakerwa sna na kundi la kina Joti na hii inaonyesha jinsi wale vijana wanavyotegemea jeuri ya Magamba, matokeo yake hao kina Bambo nao ndiyo usiseme ni dallili za Cameroun kwenda mbele.Tusije shangaa wasanii hao hao muda si mrefu watataka haki zao za ki-cameroun zitambuliwa.

PIGA MARUFUKU WASANII UCHWARA WALE WANAHARIBU HALI YA HEWA YA NCHI
 
Na hayo ndio maigizo, ukichukua muhusika akauvaa uhusika mwenyewe si maigizo tena bali itakuwa ukweli katika sanaa ya maigizo msanii auvae uhusika ili aonekane kama muhusika wakati si muhusika, hawa wana sanaa wakiume wao wanaigiza nadhani wapo sahihi kwa maana nzima ya sanaa ya maigizo.

Namemkumbuka Mudhihir wa Mudhihir nadhani angewafafanulia hilo jambo. Shibuda yeye amejawa na misemo hana lahaja
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom