Wabunge wajadili UDA kwa dharura

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,109
Mnyika%20J(3).jpg

John Mnyika

Kamati ya Wabunge wa Dar es Salaam jana ilikutana kwa dharura baada ya kupokea taarifa na nyaraka mpya za tuhuma za ufisadi, ukiukwaji wa sheria, kanuni na maslahi ya wananchi unaodaiwa kuendelea katika Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA).

Ukiukwaji huo wa sheria, kanuni na maslahi ya wananchi, unadaiwa kufanyika kinyume cha maagizo ya mamlaka zinazohusika, likiwamo Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Katibu wa Wabunge hao, John Mnyika, alisema nyaraka ambazo kamati yake imezipokea ni pamoja na barua ya UDA ya Januari 26, mwaka huu.

Barua hiyo yenye kumbukumbu namba CBA/Reg/01/UDA, inataka dola za Marekani 133,125 zitolewe kutoka kwenye akaunti ya UDA, ambayo ilishaagizwa awali fedha zisitoke kinyemela. Nyaraka nyingine ni Muhtasari wa kikao kinachodaiwa kuwa cha wanahisa wa UDA cha Februari 13, mwaka huu.

Mnyika ambaye ni Mbunge wa Ubungo alidai kuwa ikao hicho kilifanywa na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi, akiwa ni mwenyekiti pamoja na Robert Kisena aliyetambulishwa kwenye muhtasari huo kama Mwenyekiti Mtendaji wa UDA na Katibu wa Bodi ya Shirika hilo.

Alidai kikao hicho pamoja na mambo mengine, kilifanya maamuzi haramu ya kubadili waweka saini katika akaunti ya UDA iliyozuiwa kwa lengo la kuwezesha fedha kutolewa kinyemela na Simon Group.

CHANZO: NIPASHE
 
Mnyika J(3).jpg

Mtemvu,Mnyika, Zungu,Iddi Azzan,Dr Faustin, Mdee,Mwaiposa kasoro Mahanga.
Tumechoka na vikao vyenu. Kama mna ukweli SI MUMSIMAMISHE Masaburi ?
Tata 30 teyari, menejimenti ya Simon Group Nyinyi kazi yenu Vikao tu,,,
Au mnataka mkatiwe (RUSHWA) ndio mnyamaze ?
Corcodio
 
Back
Top Bottom