Wabunge waionya serikali

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
Nakubaliana na Kitime kwamba mpaka hapo wahusika wa ufisadi uliofanywa BoT, Richmond, Kiwira Coal Mining, ununuzi wa rada, ndege ya rais, magari na helicopters za jeshi na mikataba ya madini watakapochukuliwa hatua za kisheria, basi hakuna sababu yoyote ya kuuweka mjadala wa ufisadi kapuni.

Wabunge waionya serikali

na Salehe Mohamed
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

SERIKALI imeonywa kutowachagua wenyeviti na wakurugenzi wa bodi za mashirika ya umma kwa misingi ya uswahiba, kulipa fadhila, dini na kabila, bali ifanye hivyo kulingana na uwezo wa wahusika hao.

Onyo hilo lilitolewa jana Dar es Salaam na baadhi ya wabunge, watendaji na wenyeviti wa bodi za mashirika ya umma walipokuwa kwenye kikao cha wabunge wa kamati ya hesabu za mashirika ya umma, wenyeviti na watendaji wakuu wa mashirika ya umma.

Peter Serukamba, Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), alisema umefika wakati kwa Serikali kuangalia watu wa kuwapa nafasi ya kuendesha mashirika ya umma na kuachana tabia ya kutoa madaraka kwa watu wasiostahili.

Alisema watu wasiostahili wanapopewa madaraka huwa chanzo cha shirika au taasisi za serikali kutofanya vizuri, hali inayosababisha taifa kupata hasara kubwa pamoja na kupoteza ajira kwa baadhi ya watumishi.

“Tabia ya kufanya kazi kwa mazoea na kuwapa watu madaraka kwa kuangalia uswahiba haifai, kwani tusipoitokomeza, mashirika na taasisi zetu zitaendelea kuwa hoi kiuchumi,” alisema Serukamba.

Elisa Mollel, Mbunge wa (CCM) Arumeru Magharibi, alisema ufanisi katika mashirika hayo unategemea zaidi kuchagua kiongozi mwenye taaluma katika sekta husika pamoja na uzoefu alionao kwenye uongozi.

Awali akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, alisema ni vema watendaji wa mashirika na taasisi za serikali wakawa makini katika utiaji saini mikataba ili kuepuka mambo ya ufisadi ambayo yameligharimu taifa fedha nyingi.

Alisema kila kukicha taarifa za ufisadi ndizo zinazopewa nafasi katika vyombo vya habari na watendaji wamekuwa wakitumia muda mwingi kushughulika na mambo hayo, jambo linalofanya muda wa kushughulikia maendeleo kuwa mdogo.

“Muda mwingi tunautumia katika kupiga kelele kuhusu ufisadi, sasa ni wakati kwa wenzetu kufanya kazi kwa umakini ili tuweze kwenda mbele na kutimiza malengo yetu,” alisema Zitto.

Kauli hiyo ya Zitto ilipingwa na aliyekuwa Mbunge wa Makete, Hans Kitime, ambaye alitaka suala la ufisadi liendelee kuzungumzwa hapa nchi na kuionya serikali kuhusu kuchukua muda wa kuyashughulia matatizo ya ufisadi na watu wanayoyasababisha.

Alisema mambo ya EPA, Richmond, Buzwagi, Meremeta na mengineyo, hayawezi kuachwa kuzungumzwa wakati taifa linapata hasara kubwa na wananchi wanaishi maisha ya tabu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom