Wabunge wageuzia kibao Takukuru

KIGENE

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,552
813
amka2.gif
WABUNGE wameigeuzia kibao Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwa ndiyo inaongoza kwa vitendo vya rushwa.
Wakizungumza kwa jazba jana jijini Dar es Salaam katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa, ikiwa ni harakati ya mapambano ya rushwa, wabunge hao waliwashutumu vikali watendaji wa TAKUKURU na kuwatupia lawama kuwa ni vinara wa rushwa.
Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Assumpter Nshiyu Mshama, alisema kuwa TAKUKURU ndio wala rushwa wakubwa, huku akiwataka wabunge kuamua rushwa iishe kwani inawezekana.
Naye Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msingwa, alisema kuwa rushwa iko kila mahali, lakini kikubwa TAKUKURU watakasike, kwani wao ndio wanaoongoza kwa kukumbatia rushwa.
“TAKUKURU wao ndio vinara wa rushwa. Kwa mfano katika uchaguzi uliopita wakati wa kampeni ukiwapigia simu kuna rushwa sehemu fulani wao ndio wanakuwa wa kwanza kuwapigia watoa rushwa wakimbie eneo husika, baadaye wanajifanya kwenda na kukwambia hakuna wala rushwa, wajitakase wao kwanza,” alisema Msigwa.
Hata hivyo Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy, alizitupia lawama nchi za Magharibi kwa kukumbatia wala rushwa, hasa wanaoficha fedha benki za nje.
“Mataifa yaliyoendelea ndio waficha rushwa, ni wabaya sana, watu wanaweka fedha katika mabenki ya Ulaya nao wana wakumbatia, kesi za TAKUKURU hakuna hata moja serikali imeshinda, ifike wakati mwenye mali kuliko uwezo wake akamatwe,” alisema Keissy.
Pia Keissy alisema kuwa TAKUKURU wanatakiwa watende haki katika suala zima la rushwa, ikiwemo kuacha kuwakumbatia na kuwasafisha wala rushwa.
Katika hatua nyingine, wabunge hao waliijia juu TAKUKURU kwa kutoa chapisho linalomuonesha Mbunge wa Bahi, Omari Badwel, ambaye anatuhumiwa kwa rushwa wakidai kuwa ni kuingilia Mahakama.
Akijibu shutuma hizo, Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Mashitaka TAKUKURU, Donasian Kessy, alisema watalifanyia kazi suala hilo, ikiwamo kuwataka wabunge wasiiogope TAKUKURU pindi wanapokuwa na ushahidi.
Kessy pia alisema kuwa tayari TAKUKURU wameshawakabidhi Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba mapendekezo mapya ya sheria kuhusiana na rushwa.
Akizungumzia utoaji wa picha ya Badwel, Kessy alisema kuwa picha hiyo haijengi mazingira ya kuingilia uhuru wa Mahakama na utendaji kazi wake, bali ni moja ya matukio yaliyotokea katika kipindi cha mwezi Aprili, mwaka huu, hivyo ni kawaida kwa TAKUKURU kuchapisha matukio hayo.
Source : Tanzania Daima

Commonsense is not a gift it is a punishment because you have to deal with anyone who doesn't have it.


 
Angalia nchi isiyokuwa na wenyewe hata wabunge hawajui wajibu wao. Walikuwa wapi kusema yote hayo hadi umoja wa mataifa uandae semina ndiyom waaze kusema. Kwangu mimi hii ni mbinu mpya ya wabunge baada ya kuumbuliwa kwa kiwango kikubwa wajihusisha na rushwa na maelezo yao hayo ni sawa na kusema "ndiyo sisi wabunge tunakula rushwa lakini mbona na nyie TAKUKURU MNAKULA" kwa hiyo hakuna haja ya kuumbua tuwaache wajinga (wananchi) ili sisi wabunge na Takukuru tufaidi.

Mbunge ni mtu mkubwa na ana mamlaka makubwa tu, ni aibu kuja kulalamika kwenye semina kisa wameumbuliwa kula rushwa. Wafanye kazi waliyotumwa na wananchi.
 
Hii nchi haina usawa hata kidogo. Unapofikiria kuondoa rushwa unatakiwa kufikiria kwanza kujenga mazingira ya kuondoa hiyo rushwa kwa wala rushwa. Jaman hebu tujaribu kuchangiana mawazo kidogo juu ya mifumo ya Tanzania. Inapotokea serikali moja kuajili watu wenye elimu sawa katika taasisi mbili tofauti na kuwalipa mishahara tofauti kwa kiwango kikubwa hatuoni kama serikali inaweka mazingira ya rushwa? ADA holder akiajiliwa Tanesco na mwingine akaajiliwa Tamisemi yaani LGA mishahara ni tofauti kwa kiwango kikubwa, vivyo hivyo kwa TRA na taasisi nyingine. Ss nikirudi kwenye mazingira ya kuandaa rushwa ni kwamba always mtu hujilinganisha na mtu aliye juu yako na hapo ndipo tunapoingiliwa na tamaa. Serikali ingekuwa na usawa juu ya mishahara kwa maana kwamba watu wenye elimu sawa kwa taasisi zote waanze na mishahara sawa kwa course sawa, watofautiane kwa uzoefu tu na iswe kwa kiwango kikubwa. Naomba kwa wale wafanyakazi wajaribu kufuatilia utofauti wa mishahara kwa wafanyakazi wa taasisi za serikali.
 
Kule kwetu mtu akiumwa na nyoka hupewa dawa ya mzizi. Sasa ikiwa mzizi ndio umnauma watu, wapewe dawa gani? Huwezi kuutenga mfumo wetu wa utawala na rushwa! Sitegemei kuwa pawe na TAKUKURU safi ndani ya mfumo huu unaozalisha rushwa. Ni pale mfumo mzima utakapong'olewa tu ndipo......!!!
 
Inapokuja swala la rushwa hii nchi kuna sarakasi bado kila mtu anazicheza.
Haya mengine yako wazi sana ila inashangaza eti kwa sasa bado yanaonekana kama mageni!
Enewei, hili nalo litapita.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hayati baba wa taifa aliwahi kusema, Serikali iliyoingia madarakani kwa njia ya rushwa haiwezi kuwakemea wala kuwashita wala rushwa, so kwa hali hyo Rushwa haiwez komeshwa chin ya "SIRIKALI'' hii ya CHUKUA CHAKO MAPEMA.
 
Tukibadili mfumo mzima wa uongozi Rushwa itaondoka. Tofauti na hilo hakuna no thank u
 
Hiyo TAKUKURU ni idara ya CCM hivyo haina jipya na ningekuwa na uwezo ningezuia kodi yangu ninayolipa serikalini kutumika kuwalipa hao jamaa mishahara yao maana hakuna kazi wanayoifanya kuhalalisha ujira huo.CCM wamehongana nchi nzima wakati wa chaguzi zao ndani ya chama lakini TAKUKURU hawakumkamata hata mtu mmoja, shame on them!
 
Back
Top Bottom