Wabunge wa TZ wanavyowahujumu Wananchi

Malipesa

JF-Expert Member
Aug 23, 2011
310
32
Wabunge wa bunge la TZ wanawahujumu wananchi kwa kutumia muda vibaya katika vikao vya bunge kwa sababu zifuatazo:-

1. Kutumia muda mwingi kushukuru kuilko kuchangia mada iliyoko mezani kwa wakati huo

2. Kutumia muda mwngi kushutumu vyama vingine na kuwaita wabunge wenzao wanafiki badala ya kujadili mambo ya maana na yenye tija kwa taifa.

3. Baadhi Kujadili mambo kiushabiki, kubeza hoja zinazotolewa na wabunge wenzao

Sasa wabunge wa namna hii wanawahujumu wananchi kwa kuacha kutumia muda mwingi kujadili mambo ya maana na yenye manufaa kwa wananchi badala yake wanajadili mtu, ama chama na kutoa shukrani tu tena ukizingatia muda wanaopewa ni mchache.

Kwa hiyo inatakiwa ifike mahali wabunge wote wajue kwamba:-

1. Wamechaguliwa na wananchi na kwa hiyo

2. Wako bungeni kwa ajili ya wananchi

3. Wanatakiwa wafanye yale tu yenye maslahi kwa wananchi na sio kwa ajili mtu mmoja ama chama kimoja.

4. Ubunge wao ni wa msimu, wasije wakajisahau wakafikiri wao ndio wao milele.

Hayo ni mawazo binafsi tu.

Karibuni kwa mawazo mengine na michango zaidi.

Thanks.
 
Ni bahati mbaya kwa watanzania kuendelea kuwaamini wabunge wa ccmchoo na kuwapa kura kwa wingi
na hao wingi wao umewapelekea kujisahau na kudhani kuwa wametumwa kukiwakilisha chama badala ya kuwawakilisha wananchi
na wabunge wa ccmchoo wajifunze na wajue kuwa wananchi wa leo sio wale wa miaka ya 1960
na pia wajue ile nec sio ya kudumu kwa hiyo uongozi wa nec kila ukija utakuja kitofauti walitambue hilo
kwa kifupi wasome alama za nyakati.miaka 4 sio mingi nawatabiria anguko la ajabu.huu sio ufalme ni uongozi ndio tunaoutaka.
na wasijisahau kuwa hii nchi ni ya watanzania na sio ya ccmchoo.powa kazi kwao.miaka mine!!!!?
 
Back
Top Bottom