Wabunge wa TZ kwenye Bunge la EAC watetea kwa nguvu zote Kenya kujenga Uwanja wa Ndege Taveta

Kwani wabunge wa Tz wana haki ya kuingilia mipango ya Kenya? Iwapo tutanufaika pamoja nao hao wakenya watakapokuja watalii kwao. Tukumbuke kuwa tuna vivutio vingi zaidi upande wa kwetu kuliko huko Kenya.

Hata mlima Kilimanjaro uko kwetu ila isishangae kusikia kuwa unawafaidisha sana wao (Uwanja wa ndege wanakoshukia na kuondokea, hoteli wanakolala, "tour operators wanaowatumia n.k.)
 
Mnalia nini na hao vilaza ndio waliochaguliwa na wabunge wa magamba? Did you expect anything substantive from people like Kimbisa and Shy Rose Bhanji?

Acha tu, yaani mimi nimewasikiliza vilaza wale.. yaani kabisa wao wamekaa kutetea oooh katiba ya Kenya, nilidhani wao wangetoa mapendekezo ya namna gani sisi pia tufanye kuweza kuboresha biashara ya utalii ili kukamata soko la utalii kwa EA. Wanaonekana kama walipewa safari ya Kenya wamevimbiwa sasa ni kusifia tu... hata ukiwaangalia inaonekana walikuwa na njaa sasa wameona mwezi ni kusifia Kenya tu... s*****i type!!
 
Watanzania tuna matatizo makubwa kuliko tunavyofikiri.Kama wawakilishi wetu katika bunge la EAC wana ubongo mdogo kiasi hicho basi tunalo tatizo kubwa kupita kiasi nadhani tulichagua kwa kigezo cha lugha pekee badala ya kuangalia mambo mengine mengi.
 
Hivi kwanini tunawaogopa sana wakenya jamani?

Maana kila mtu humu anakomenti akimaanisha KIA ndio kwisha habari yake, kwanini? Kwasababu wao wakenya sisi watanzania!!!! Upuuzi

Wakati mwingine tunapenda mno kulalama bila sababu za msingi, hii ni dunia ya ushindani ukilaza damu wenzio wanachangamkia
 
Hivi tuna haki gani ya kuingilia mipago ya Serikali ya Kenya? wao wanapanga mambo na wanatekeleza - hawana muda wa kupoteza kwenye misamiati ya kiswahili kama sisi, uwezi kusikia Waziri wa Kenya akileta mambo ya longolongo kwenye Bunge lao i.e kusema: mara tuko kwenye mchakato mara mipango yakinifu mara mshauri mkazi sijuhi nini! come next year wanarudia ngojera hizo hizo; ukifikilia tunavyo fanya kazi kwenye Taifa letu mtu unaweza kupata wenda wazimu.

Juzi Juzi hapa niliona mbunge wa upinzani akija juu kwa kupinga kauli aliyo toa Bungeni Waziri, mbunge huyo alisema Waziri anayo sema mwaka huu hayana tofauti na aliyosema mwaka jana na ahadi zake ambazo azitekelezeki ziko palepale, sasa mwaka huu atafanya mihujiza gani? Wakabishana kidogo, ndipo mbunge akamwambia Waziri alete hansard za mwaka uliopita walinganishe na kauli ya Waziri ya sasa hivi tuone kama kuna tofauti yoyote! Nilimuona Waziri anakaa kimya.

Sasa tukirudi kwenya mada, hivi hicho kiwanja cha Kilimanjaro kilijengwa lini? Zaidi ya maika arobaini na ushee, je tunaweza watanzania kusema kiwanja hicho kimewahi kunufahisha taifa letu kweli - licha ya kujengwa kwenye mbuga za wanyama, tatizo letu hatujuhi kufanya bihashara hatuna habari kwamba kujitangaza ni muhimu sana, tunabakia kuwalahumu Wakenya wakati sisi ndio wenye matatizo, kila kitu tunafanya kimazoea tu mradi unapata mshahara kila mwezi kutoka serikalini watu wanajisahau waona wafanye kazi wasifanye mshahara huko pale pale - Wakenya hawako hivyo, kwao kazi ni kila kitu(uhai).

Wakenya walichofanya bila shaka katika utafiti wao waliona kumbe kiwanja cha Kilimanjaro hakitumiki kikamirifu, sasa kutokana na business acumen walio nayo wakaona wakijenga kiwanja cha kimataifa karibu na Kilimanjaro watanufahisha Taifa lao, kumbe wafanye nini kama sisi hatujuhi kuchangamkia fulsa. Huwa nawasena sana Wakenya lakini katika hili tujilahumu sisi sio WAO.
 
Bukyanagandi nakubaliana na maoni yako,mimi huwa najiuliza ni kwanini Landing charges na bei ya mafuta pale KIA ni kubwa kulinganisha na Viwanja vya ndege jirani kama Kenyatta,Mombasa na JK Nyerere? Kila mwaka tunaambiwa kwamba gharama za kutua na mafuta ni kikwazo kwa ndege kubwa za kibiashara kutua KIA,lakini serikali haichukua maamuzi yeyote. Imefika sasa wakulima wa maua na mboga toka mikoa ya Kaskazini wanasafirisha mazao yao kupitia Kiwanja cha Kenyetta kwasababu ya gharama kubwa kupitisha KIA zinazotozwa na KLM. Hata nauli ya abiria wa KIA toka/kwenda Ulaya ni kubwa sana kwa zaidi ya dola 600 kulinganisha na anayetumia Uwanja wa Kenyatta! Wachumi wetu wanafanya nini?
 
Wajenge tu Tanzania hakuna kitu,wananchi wake walishakata tamaa siku nyingi
 
kimbisa namfahamu nimefanya naye kazi redcross leo sitaki kuzungumzia juu ya madudu yake anayofanya huko pamoja na wizi wake ila nazungumzia aina ya wabunge tuliopeleka afrika mashariki wengi tuliona uchaguzi ulivyotawaliwa na rushwa na pia watu wenye uwezo wakiachwa na kuchukuliwa hao ambao naweza kuwaita ni mzigo kwa taifa letu.Wamezungumzia juu ya kenya kujenga uwanja wa ndege mpakani mwa tanzania wakiuhalalisha kuwa ulikuwa kwenye mipango ya kenya hapo wamejionyesha udhaifu wao kwani wenzao walijenga hoja lakini wao kwa umbumbu wameshindwa kujenga hoja na kukubaliana na mpango huo wakati wanajua kabisa kujengwa kwa uwanja huo ndio kifo cha kia kama kenya wangekuwa wanajali maslahi ya jumhiya ya afrika mashariki wangezungumzia kuboresha uwanja wa kia badala ya wao kujenga mwingine mpakani mwa tanzania mbona sisi tunapotaka kujenga barabara serengeti wamekuwa wanapiga kelele wakati swala hilo lipo nani ya mipango yetu ya maendeleo .kwa stahili waliyoanza nayo tutashuhudia madudu mengi tu.
 
Wabunge wa Tanzania kwenye Jumuia ya Africa Mashariki wametetea kwa nguvu zote kenya Kujenga Uwanja wa Kimataifa wa Ndege jirani na Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro, wanadai hauna shida kabisa na ni mipango ya Serikali ya Kenya,

Source CHANNEL 5(EATV)
halafu mtasema kuna ushirikiano.. halafu tatizo la hawa wabunge hawajui Economics hawaelewi Uwanja wa ndege una manufaa gani kwa nchi kiuchumi hivyo kwao ni sawa tu ili mradi twende..
 
How effective are our EALA members from Tanzania in terms of influencing the debates and responding to issues raised during the meetings, please watch:

1ST MEETING- 4TH SESSION -SEPT 2010-EALA debates on Yellow Travel Fever requirements for East Africans travelling to Tanzania through Kilimanjaro Int'l Airport.


Source: jumuiya1 of youtube

Wadau,
Nimefanya usaili ktk youtube na kushindwa kuona clip yoyote toka Tanzania juu ya Bunge la Mashariki lakini wenzetu Kenya na Uganda ndiyo wana-clip za video kibao kutetea masuala mbalimbali. Rai yangu wabunge toka Tanzania ktk Bunge la Afrika Mashariki 'wajiuze' zaidi ili Wa-Tanzania tujue wanachofanya ktk vikao vya Bunge la Afrika Mashariki.


Dr. Kitila Mkumbo akizungumzia upungufu wa uchaguzi wa EALA

Mwisho tumsikilize Dr. Kitila Mkumbo wa UDSM akichambua kitu hiki 'Bunge la Afrika ' kwa mtazamo wa kutetea maslahi ya Tanzania ambacho hivi sasa hakipo kwa wabunge wa Afrika Mashariki toka Tanzania


source: mwanakijiji wa youtube
 
Last edited by a moderator:
Hili liinchi limeoza. Kenyans wanakataa na kulalamika wanapoingiza magari yao Tanzania wasilipe wakati kwenye barabara zao wanalipia. Dhaifu maliza muda wako mapema.
 
Kama ni kweli basi kunaweza kusababisha KIA ifungwe kwa kukosa wateja.
 
Back
Top Bottom