Wabunge wa Tanzania fanyanyeni kama alivyofanya mbunge wa Mufindi Kaskazini

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,766
894
Mbunge wa Mufundi Kaskazini, Mahamud Mgimwa? amesema hataweza kuvumilia kuona wagonjwa katika jimbo hilo wakibebwa kwa kutumia machela na kwa hiyo ameamua kutumia Sh. 90 milioni, alizokopeshwa na serikali. ameamua kuzitumia hizo pesa kununulia magari matatu ya kubebea wagonjwa. amesema sina sababu ya kutembelea gari la Sh 90 milioni, wakati wananchi wangu wanatumia baiskeli kusafirisha wagonjwa.
SOURCE: MWANANCHI MEI 23 2010.
Huyu mbunge kwa kweli ni mbunge mwenye kujua majukumu yake, wabunge wengine fanyeni kama alivyofanya mwenzenu
 
Mbunge wa Mufindi Kaskazini, Mahmud Mgimwa, amesema hataweza kuvumilia kuona wagonjwa katika jimbo hilo wakibebwa kwa kutumia machela na kwa hiyo ameamua kutumia Sh90 milioni, alizokopeshwa na serikali, kununulia magari matatu ya kubebea wagonjwa.
Mgimwa alisema sina sababu ya kutembelea gari la Sh90 milioni, wakati wananchi wangu wanatumia baiskeli kusafirishia wagonjwa.
Alisema pamoja na kushughulikia tatizo la magari ya wagonjwa, pia atahakikisha kuwa huduma za afya zikiwemo za upasuaji mdogo katika vituo vya afya vya jimbo hilo zinaboreshwa, ili wananchi wasiangaike kufuta huduma hizo katika hosptali ya wilaya.
SOURCE: MWANANCHI MEI 23, 2011
 
Badala yake wanadai wapewe marupurupu kama ya mbunge ili awakomboe watanzania!
kwenye package hiyo Slaa anapewa na huo mkopo? Wanafiki wakubwa!
 
haahha....yule mbunge ni muongo wa kutupwa na hajafanya lolote lole
 
Na kama mbunge hana hata kibajaj akitumia milioni 90 zote atawafikiaje wananchi wake?
 
Back
Top Bottom