Wabunge wa mkoa wa DSM kumbana mkurungenzi mkuu wa NHC (Nehemia Msechu)

Leo wabunge wa mkoa wa DSM pamoja na mkurugenze mkuu wa NHC watafanya mkutano na wakazi wa Ubungo NHC. Wabunge hoa watataka kujua ujenzi unao endelea hapa ubungo kama umefata taratibu zote za ujenzi maana sasahivi ukipita katikati ya haya magorofa ni hatari tupu, vile vile wabunge watataka kufahamu kuusu uzwaji wa magorofa ya zamani maana mswada ulisha pitishwa bungeni tangu mwaka 2005 kama wakazi wa ubungo wauziwe izo nyumba. Wakazi wa ubungo NHC wamejikusanya kwa wingi wakiwasubiri wiongozi hao wafike ili kikao kianze. Kama Mchechu hakishindwa kujieleza vizuri, wabunge hao wamepanga kukwamisha majeti nzima ya wizara ya mama Tibaijuka!

dogo jaribu ku-edit kidogo
 
yule kama una ongelea magorofa ya ubungo karibu na Ubungo plaza "shekilango/moro road" mbona yaliushauzwa kwa wapangaji?
 
yule kama una ongelea magorofa ya ubungo karibu na Ubungo plaza "shekilango/moro road" mbona yaliushauzwa kwa wapangaji?

bdo: ndio ayo ninayo ongelea, yalio uzwa ni aya yanayo jengwa, yazamani bado hayajauzwa
 
DG kwa upande mmoja anastahili pongezi. Ningependa kumpa ushauri wa wa jinsi ya kuweza kuendeleza NHC.

  • Angeacha kuvunja nyumba za zamani na kujenga mpya zenye ghorofa nyingi. Tanzania haina shida ya ardhi. NHC ikishirikiana na wizara mama, wangeanzisha miji mipya , iliyokuwa imepimwa vizuri kwenye maeneo kama Buyuni, Kigamboni, Boko. Majengo haya mapya yasizide ghorofa tano. Wajenge pia (kwenye haya maeneo mapya) facilities kama shule, hospital. Kujenga 14 floors building ina cost 30 billion tshs. Ukipeleka hizi kwenye maeneo mapya , alot will be done.
  • Angefanya stock of what he has (land and majengo)
  • Kama kubomoa na kujenga , afanye hivyo kwa uangalifu sana. Asiwafuate wahindi. Wale waliwahi. Kwa sasa hata wale waliyinunua nyumba , hawajapata tenants. Vilevile infrastructure haipo. DG pita mtaa wa MIndu usiku (saa mbili) kuangalia situation ikoje. Ziko nyumba nyingi katika stages mbalimbali za ujenzi. Can you compete?
  • kama utabomoa , jenga nyumba zenye floor chache (max 5). Nina uhakika kuwa utapata soko kwa haraka zaidi

Lakini utakubaliana na mimi kwamba the future is brighter kwa sisi ambao tunaishi nyumba za kupanga na kulipa kodi ya mwaka mzima!

Hilo la miji mipya naku support kwa 100% na isiishie kujenga majengo ya kuishi tu bali hata maofisi ili hawa watu wasilete msongamano city centre.
 
eti wabunge kumbana DG...wanapoteza tu mda wao...the boy is clever and he knows what he's doing. in the next ten years National Housing watakua wana nyumba nzuri na za kisasa compared to miaka ya nyuma. Yule DG kabla ya mchechu alikua ovyo, alikua anasoma magazeti tu ofsini kwake...
 
Bila kupinga kuwa DG amefanya kazi nzuri kuiinua NHC hongera kwake ila ninacho jiuliza nia Watanzania wangapi wanaweza kumudu gharama za kununua achilia mbali kupangisha hzo apartments zinazooteshwa kila uchwao?Mm ningetoa ushauri wangu kuna technologia ya low cost houses ni rahisi na hata mwananchi wa kawaida anaweza kumudu gharama zake akiwezeshwa ili kuboresha makazi,nyumba inajengwa kwa interlocking bricks na kiasi kdgo sana cha cement kinatumika na machine inapatikana kwa gharama za chini kabsa kwa wanaoweza kwenda mnaweza kwenda mwenge round about mkono wa kushoto kujionea hiyo technologia na nyumba za bei ya chini kabsa.
 
bdo: ndio ayo ninayo ongelea, yalio uzwa ni aya yanayo jengwa, yazamani bado hayajauzwa
please nenda blck F, B, A magorofa ya zamani, vyumba kibao vishauzwa na unakuta wenyewe wameisha weka hata mageti, katikati ya corridor
 
Kwa taarifa tu Mama Porojo, Ujenzi pale NHC Ubungo (Shekilango) ulianza miezi miwili au 3 iliyopita na bado haujafika mbali sana. Nafikiri mtoa mada anaposema wakazi wa ubungo anamaanisha wapangaji wa ubungo nhc.

Kwa upande wangu mimi nina imani kubwa na uwezo wa Nehemia Mchechu lakini kwa hili alilolifanya pale shekilango naanza kumtazama kwa jicho la ziada. Haiingii akilini ule ujenzi unafanyika katika mazingira yale, sidhani pia kama mkandarasi aliyepewa kazi ni competent hasa.

Baada ya kusikia matangazo ya uuzaji wa nyumba mpya nami nilienda kutazama eneo ambapo maghorofa mapya yatajengwa ili nami ninunue lakini baada ya kupaona kwakweli nilighairi kuchukua form. Yaani ghorofa linajengwa katikati ya maghorofa mawili, kwenye eneo lililokuwa wazi la takribani mita 25 au 30 tu, kwa vyovyote kutakuwa na tatizo la kukosa hewa/upepo na maghorofa yatabanana.

Kadhalika eneo hilo ndilo lililokuwa likitumika kama parking, sasa nikinunua nyumba nitapata tabu pia kumtafutia parking mpangaji wangu! Tembelea mitaa ile nyakati za usiku ujionee vurumai la parking.

Pia ujenzi ulianza kabla nhc hawajapata kibali cha kubadilisha matumizi ya ardhi na building permit, hivyo ujenzi ulianza kabla hawajaweka bango la kuonyesha project. Kwa kifupi kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria za nchi, taratibu na kanuni mbalimbali za ujenzi na makazi bora.

Bado naendelea kufuatilia kulikoni Nehemia Mchechu afikie kufanya mambo ya kihuni yasiyoendana na akili na integrity yake kama ninavyomfahamu!!
 
eti wabunge kumbana DG...wanapoteza tu mda wao...the boy is clever and he knows what he's doing. in the next ten years National Housing watakua wana nyumba nzuri na za kisasa compared to miaka ya nyuma. Yule DG kabla ya mchechu alikua ovyo, alikua anasoma magazeti tu ofsini kwake...

- AHSANTE SANA, kumbe tupo wengi tunaothamini kazi yake!

William.
 
Tatizo lako Wiliam Malecela unasifia tu hata bila kufuata logic ya hoja hata kama kuna total blundering.Kama kazi yako ya utarishi nje imechoka na kuamua kurudi kwa kisingisio cha kugombea ubunge wa EAC kwa ajili ya kuzuga tu tafadhali usiharibu maana na credit nzima ya jf.Endelea na kazi yako hiyo wajanja tunajua kazi yako ni nini.

- Huku bongo zinaitwa swagaz, ungefanya utafiti usingesema haya, pole sana!

William.
 
Tungepaa kuelekea chiloonwa, baba yako alishindiwa nini, una maana mdingi kichwa cha panzi sio!
hamuwezi kuifanyia lolote la maana tz.
sikutarajia ungefichua jinsi akili yako alivyo athiriwa na kuyumba kwa meli. kkhhhaaaa. . . . . . . . . . likupate hukohuko uliko . . . .phooooo!

- Siwezi kumjadili baba yako maana nitakuwa ninajivua nguo kama wewe, wenye akili watashindwa kutofautisha nani ni nani, hapa ndipo uwezo wako wa kufikiri unapoanzia na kuishia!

- Mmezoea kurusha matusi tu mkirushiwa kule Arumeru vilio, kwa huyo wa NHC hakuna longo longo ni Super kazi tu, baack off!

William.
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya mwili wako na uwezo wako wa kufikiri......

- At least ina maana moja tu kwamba Somo limeeleweka, saafi sana that is all I could kutoka kwa Great Thinker kama wewe, mengine ni swagaz yaani kelele za mlango!

William.
 
Mkuu Nasema mimi niliishi maeneo hayo miaka ya nyuma kidogo. Niliposikia kwamba kuna maghorofa yanajengwa pale nikajiuliza wanajenga eneo gani kwa sababu naijua geographia ya pale. Nikaambiwa wanajenga kati ya ghorofa mbili. Nikashangaa. Hakika pale hakuna nafasi.

Pale Ubungo kulikuwa na vijumba vidogo vya NHC vingi tu na vina viwanja vizuri tu lakini maamuzi yakapitishwa ati kuwauzia waliokuwa wapangaji mle. kinachofanyika sasa ni uchafuzi tu wa mazingira huko nyuma ya Ubungo Plaza. Kabla havijauzwa kulikuwa na mitaa safi mabomba ya kupitish maji machafu lakini leo hakuna mitaa ni vichochoro tu! Hali mbaya kweli huko. Mchechu afikirie kuvifidia hivi vijumba ili wapate sehemu ya kujenga nyimba nyingi kwa ajili ya makazi. Pia itaokoa uharibifu wa mazingira eneo hilo.

Mimi namkunali Mchechu ameleta chachu NHC lakini kuna mambo mengine hayaendi vyema. Sijui soko la hizo nyumba zinazojengwa ni lipi. Yaani ametarget watu gani? Nyumba z Ilala Mchikichini ni Tshs. 168 mil. VAT exckusive na inatakiwa ulipe 10% upfront. Mtanzania gani wa kawaida atainunua hiyo nyumba?
 
Last edited by a moderator:
Wabunge Nawashauri Muandamane Miji Yetu Iwe Planned!! na fungu litengwe kwa ajili ya planners na surveyors Kwenda site Kuweka demarcations (Mipaka) Kwa ajili ya public land kama barabara na Shughuli za Kijamii!! Ibaneni Wizara itekeleze Hili!! Ni Muhimu sana kwa Vizazi Vijavyo na sasa!! Lah Hivyo hawa wanetu watajatucheka na kuonekana Hatuna uwezo Kiakili!! Suala la Hizo Nyumba ni expensive Project!! Very few are Interested!! don't Bother on That!!
 
Nakubaliana na maoni yako Kimbunga. Napata tabu kuamini kama ni makosa tu ya kiufundi au kimkakati yaliyopelekea haya. Huenda kuna siasa na michezo michafu ndani yake. Maswali zaidi yanaibuka pasipo majibu. Ukweli utafahamika soon.
 
Back
Top Bottom