Wabunge wa kuteuliwa: Msimamo wa CHADEMA ni upi?

BondJamesBond

Member
Jul 6, 2011
85
60
CCM walikuja na hii scam ya wabunge wa kuteuliwa kwa sababu ya jinsia na sio merit kama yule mama anaiyeitukana JF kila kukicha, Mchungaji Rwakatare ambaye naona anakula sana pesa za walipa kodi japo hawakumchagua awawakilishe.

Je CHADEMA wanamsimamo gani juu ya hii scam ya CCM? Je wakichukua nchi wataiondoa au itabaki? na sababu zao ni zipi?
 
Hii nadhani iko kikatiba (Naweza kurekebishwa) kwa hiyo Chadema kwa sasa hawana la kufanya, lakini kwenye katiba mpya, upuuzi kama huu ndio unatakiwa kuondolewa.
 
Hii nadhani iko kikatiba (Naweza kurekebishwa) kwa hiyo Chadema kwa sasa hawana la kufanya, lakini kwenye katiba mpya, upuuzi kama huu ndio unatakiwa kuondolewa.

wanaweza kupeleka mswada bungeni wa kubadilisha kipengele hicho cha katiba. Ila ni mpaka mtakapowapa dhamana.
 
Basically hao wamekuja kwa shinikizo la nchi za magharibi ili kuleta uwiano wa jinsia ila tatizolao hawajitambui
 
Basically hao wamekuja kwa shinikizo la nchi za magharibi ili kuleta uwiano wa jinsia ila tatizolao hawajitambui

Kama ni kweli! mbona wao nchi za Magharibu hawana Wabunge wa kuteuliwa?!.
 
Si wabunge tu peke yao hata wakuu wa Wilaya hawana kazi na wanakula tu pesa za walipa kodi bure,hili nalo litaondoka chini ya CDM.
 
CCM walikuja na hii scam ya wabunge wa kuteuliwa kwa sababu ya jinsia na sio merit kama yule mama anaiyeitukana JF kila kukicha, Mchungaji Rwakatare ambaye naona anakula sana pesa za walipa kodi japo hawakumchagua awawakilishe.

Je CHADEMA wanamsimamo gani juu ya hii scam ya CCM? Je wakichukua nchi wataiondoa au itabaki? na sababu zao ni zipi?
Teh teh teh, Hivi unategemea wabunge kama akina Lucy Owenya, Grace Kiwellu, Chiku Abwao, dada yake na Lissu waingieje mjengoni kama siyo kupitia viti maalum tena baada ya kukutwa na Maswahibu makubwa toka kwa mkubwa wa Chama? funika kombe mwana haramu apite.
 
Kama ni kweli! mbona wao nchi za Magharibu hawana Wabunge wa kuteuliwa?!.
Kwani mkuu, ulishaona vyama vya upinzani vya nchi za magharibi vinafungua matawi huku kwetu? angalia tunavyong'ang'ana kuhutubia kule kwao na sijui ni ili iweje. Wao ni wa kwanza kusema haki sawa kwa jinsia zote.
 
Kama michango yao bungeni inaonekana na inatija sio mbaya wakiwepo, tatizo wengine hawazitendei haki nafasi hizo.kama mchungaji Lwakatare (licha ya TZ kupata misukosuko mingi ya kisiasa/uchumi/kijamii) yeye hakuna chochote alichokifanya bungeni licha ya watu kuufahamu uwezo wake mkubwa wa kuongea majukwaani.Ninamashaka sana na hiyo PhD yake.
 
Back
Top Bottom