Wabunge wa Chadema waukana udini

armanisankara

JF-Expert Member
Jul 15, 2011
283
49
Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamewataka Watanzania kuondokana na propaganda zinazoenezwa na baadhi ya watu kwamba chama hicho ni cha waumini wa dini fulani na kwamba wanaoeneza uvumi huo wana ajenda yao ya kutaka kukidhoofisha kisiasa.

Wabunge hao wa viti maalum Suzan Lyimo, Grace Kihwelu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Hajjat Shida Salum walitoa kauli hiyo juzi wakati wa futari iliyoandaliwa kufuturisha wananchi wa jJiji la Dar es Salaam katika hafla iliyofanyika makao makuu ya chama hicho Kinondoni.

Kihwelu alisema Chadema ni chama cha watu wote na wala hakina uhusiano na dhehebu la dini fulani na ndiyo maana hata katika safu ya uongozi wa juu chama hicho nafasi zote nyeti zimeshikwa kwa idadi sawa kati ya Waislamu na Wakristo.

Kuhusu sensa, alisema viongozi wa dini waendelee kuwahamasisha waumini wao ili wajitokeze kwa ajili ya kushiriki zoezi hilo kwani ni jambo muhimu litakaloiwezesha nchi kuweka vizuri mipango yake ya maendeleo.

Kwa upande wake Lyimo alisema Chadema siyo chama cha kidini na kwamba wanaoeneza madai hayo wana ajenda yao binafsi hasa kutokana na chama hicho kuendelea kuungwa kwa kasi kubwa na Watanzania wengi.

Alisema ni jambo la ajabu katika karne hii kuna baadhi ya watu wanazungumzia suala la udini ambalo lilikuwa linapigwa vita na muasisi wa Taifa hili, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Akizungumzia suala la sensa, alisema hakuna sababu kwa serikali kuogopa kuweka dodoso za la dini kwa kuwa siyo jambo baya kufahamu idadi ya Waislamu na Wakristo.

Naye Mjumbe Shida Salum ambaye pia ni mama mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, alisema chama hicho kamwe hakitaruhusu suala la udini lijipenyeze kwasababu kilianzishwa kwa malengo ya kuwakomboa Watanzania wa aina zote bila kujali dini au makabila yao.

Hajat Shida aliwataka wananchi waendelee kukiuka mkono chama hicho ambacho kimekuwa pekee chenye mwelekeo wa kuwakombo kuelekea katika harakati za kupata maendeleo.




CHANZO: NIPASHE

 
Udini na ukabila silaha za chama cha mabwe..... kuulaghai umma na kudhoofisha wapinzani wao kisiasa. Wakisema uchafu huu majukwaani watajibiwa ktk kiwango cha kuwafunga mdomo kwa vielelezo visivyo na utata!. Hiyo ni kazi nape, ridhiwan k, na mukama.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom