Wabunge wa CHADEMA wanakatisha tamaa

Chadema ni janga la kitaifa, tujihadhari na hawa wanafiki.
 
Chadema ina wabunge 23 tu wakuchaguliwa bado hawakai bungeni sasa siku tukiwapa nchi wakawa na wabunge wengi si ndio atabakia spika peke yake...lakini cha kushangaza kwenye kuchukuwa posho wanakuwepo.
 
Wewe kweli ni GT? Kwani tumewachagua watupe hela ya kula au kutuwakilisha kwa kutimiza majukumu yao mojawapo likiwa kuhudhuria vikao vya bunge bila utoro? Think or sink...

Mkuu umeambiwa walikuwa kwenye vikao vya makati mbalimbali mbona bado unalalamika tu au unajingine..
 
Labda wameenda kunaniliyu.
Yesu alikuja ili tuwe na uzima, kisha tuwe nao tele.
 
Wachangiaji wa namna hii ndo wanawapofusha Wabunge na viongozi wa CDM. Mwenzetu Mohamedi Mtoi anawachukulia CDM kama muhimili (reference pillar) wa mabadiliko na dola tarajiwa inayotegemewa ilete mageuzi ya kimfumo na kimuundo. Hivyo haitegemewi CDM wafanye kama CCM.

Na kwa muktadha huo ndo maana Mohamedi Mtoi anawashangaa na kuwakanya wajirekebishe. Lakini memba ambao wameifanya CDM na viongozi wa CDM kuwa Malaika hawataki daima chama na viongozi wao wakemewe wala kuguswa kwa makosa wanayofanya. Huku ni kupelekea akili na utashi wetu likizo.

Tunaanza kuzidiwa na wanyama wanaopambanua walau kidogo

Mkuu Omutwale nakushukuru kwa kuiona mantiki yangu kwenye hii hoja.

Tatizo kubwa ninalo liona kwa baadhi ya wanachama wenzangu na wapenzi wa chadema ambao tumo kwenye hii mitandao ya kijamii linapo kuja swala la kuijadili chadema wanapeleka akili zao likizo na hata kutoa hoja za kupiga mbizi ili mradi kutetea kila kitu kana kwamba chama chetu ni chama cha malaika! Huwa hawapendi kuuona ukweli kwa gharama yoyote na wanashindwa kutambua kuwa kuto kupenda kuuona ukweli ndio leo kunaigharimu ccm na serikali yake.

Mfano. Ccm hawaku kubali kuwa makada wao wamehusika kuiba pesa za Epa, Richmond na Kagoda haohao hawakubali kuwa Dr Ulimboka hakutekwa na Mkenya, haohao wanazuia mijadala bungeni kwa kusema kuwa ni kuingilia uhuru wa mahakama. Je impact yake huku nje kwenye jamii ikoje?
Hata mbuyu ulianza kama mche wa mchicha. Kulea ujinga hivihivi.
 
Mkuu Omutwale nakushukuru kwa kuiona mantiki yangu kwenye hii hoja.

Tatizo kubwa ninalo liona kwa baadhi ya wanachama wenzangu na wapenzi wa chadema ambao tumo kwenye hii mitandao ya kijamii linapo kuja swala la kuijadili chadema wanapeleka akili zao likizo na hata kutoa hoja za kupiga mbizi ili mradi kutetea kila kitu kana kwamba chama chetu ni chama cha malaika! Huwa hawapendi kuuona ukweli kwa gharama yoyote na wanashindwa kutambua kuwa kuto kupenda kuuona ukweli ndio leo kunaigharimu ccm na serikali yake.

Mfano. Ccm hawaku kubali kuwa makada wao wamehusika kuiba pesa za Epa, Richmond na Kagoda haohao hawakubali kuwa Dr Ulimboka hakutekwa na Mkenya, haohao wanazuia mijadala bungeni kwa kusema kuwa ni kuingilia uhuru wa mahakama. Je impact yake huku nje kwenye jamii ikoje?
Hata mbuyu ulianza kama mche wa mchicha. Kulea ujinga hivihivi.

Ukisoma mada ya hiki kipande https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...uwa-dawa-za-ccm-ndizo-sumu-zinazoiua-ccm.html, utagundua uliyoyaona leo yana uzito na madhara gani huko mbele ya safari. English Learner kayachambua walau kwa ufupi lakini kwa maono
.....Ni rahisi kwa CCM kurudi ndani ya muda mfupi namna hii kwa sababu, pamoja na maandalizi yanayoendelea kwenye vyama vya upinzani kushika dola, bado ni yatima wa mipango na rasilimali watu makini wa kutekeleza na kukidhi matumaini ya Wananchi ndani ya kipindi kifupi cha miaka mitano (5). Vyama vya Upinzani vimefanya na vinaendelea kufanya makosa makubwa sana kwa kuacha wananchi kuweka matumaini makubwa kupitiliza juu ya nini watakifanya wakiingia madarakani. Wamewaaminisha wanancnhi kwamba kile walichoshindwa CCM kwa miaka 54 (hapo 2015) wao watakifanikisha ndani ya miaka mitano! Kwa kosa hili, wategemee kuchukiwa haraka sana na kupingwa na wananchi hao hao watakaokuwa wamewapa ushindi. Ebu nisitoke ndani ya mada maana hii tayari ni mada nyingine kabisa. Nakutakia tafakuri njema.
 
Kuweni makini wakuu! Utoro na kutokuwa makini ndio umechangia kupitisha sheria ya mifuko ya pensheni ambayo leo ndio bunge limegundua kuwa walichemka baada ya kelele za wananchi makini.

Jiulize, wabunge wa chadema ambao ni mahiri kwa kuibua hoja nzito na kusimamia maslahi ya wanyonge walikuwa wapi? Au ndio utetezi wenye makengeza kuwa walikuwa nje wanatafiti na kazi yao ni kuisimamia serikali?

Sheria ya mifuko ya pensheni ya mashirika ya umma inamgusa kila mlalahoi aliye ajiriwa kwa hiyo wabunge kutokuwemo ndani ya bunge na kuwa makini na mijadala athari yake ni kama hii ya kurudisha upya mjadala nakupoteza muda ambao ungetumika kujadili mambo mengine ya msingi yanayo tukabili.

Hiyo sheria alipitisha Mh. Jenista Mhagama; yeye ni mwenyekiti wa kamati na siku ya majadiliane akawe ndio mwenyekiti wa bunge na jioni yake akawa mchangiaji kwa ajili ya kuitetea zaidi
 
Hata sijui una tamaa ya nini inayokatwa na na wabunge wa chadema

Nina TAMAA ya kuona wana onyesha utofauti na wabunge wa ccm hasa ukichukulia ndio kwanza wameaminiwa kwa mara ya kwanza kuwa chama kikuu cha upinzani na wao ndio wamebeba matumaini makubwa ya mabadiliko na ndio serikali inayo subiri hivyo hatuwezi kuwa serikali mbadala yenye kufuata tabia zilezile za serikali zee. Period.
 
Hapo nina mashaka sana. Hivi serikali ya CCM ingewaachia tu jamaa wa Chadema wachukue rushwa huku inajua ??? Labda sio serikali hii tunayoifahamu sisi.
Serikali hii, jambo dogo sana likifanywa na Chadema litakuzwa saaana. Mpaka hoja za msingi zinapingwa kwa sababu tu zimetolewa na Chadema.
Hapo umechemka. Au labda huyo uliyemnukuu naye kachemka. Rushwa ni kosa kubwa sana, lisingeweza kuachiwa hivi hivi.

Hilo la kuchukua rushwa sijasema mimi. Ni live experience ya mgombea wa ubunge wa Afrika Mashariki William Malecela a.k.a Le Mutuz ambaye wabunge wa CHADEMA walimuomba rushwa ili wampigie kura, akawapa lakini hawakumpigia so akaja kuwasemea hapa JF. Kwa kiswahili cha kisasa tunaweza kusema kuwa "walimpiga"!. Hakuna mbunge wa CHADEMA aliyekanusha hilo, so inaendelea kuwa valid information unless otherwise. Serikal haihusiki na rushwa kama hiyo iwapo haijaripotiwa TAKUKURU.
 
Chadema ni janga la kitaifa, tujihadhari na hawa wanafiki.



Habari za jioni ndugu mzee!!
Nitajie janga la kiwilaya!
Nitajie janga la familia yako!
Nitajie janga lako binafsi!
Tazama jinsi unavyoyakodolea maswali yangu ewe ndugu Mzee.
Halafu nani alileta hili janga?na liliwasili lini,likitokea wapi?
Na watawala wamefanya nini kutuepusha nalo.
Tazama unavyokuna kichwa kwa kukosa majibu!
Habari za jioni Ndugu Great Thinker Mzee!


 
Hakuna mtu aliyezaliwa kuishi maisha ya mwingine. Fight for your daily bread na usitegemee lolote toka kwa mwana siasa...kila mtu yuko kwa maslahi yake pale. Huyo JOHN Mnyika kila siku ni miongozo na taarifa lakini ubungo yote haina maji.

Kwani mnyika ni meneja wa dawasa?
 
Back
Top Bottom