Wabunge wa CHADEMA isipokuwa Zitto wanalamba Posho za Vikao Bungeni

MAFILILI

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
2,377
1,194
Zito leo kaweka mambo hadharani kuwa ni yeye pekee ndani ya CDM hajachukua posho za vikao tangu Julai 2011 akiwa bungeni. Mbowe na wengineo toka CDM wameshindwa kutekeleza kivitendo hoja ya kupinga posho. Hongera Shibuda kwa kuwa muwazi
 
katika kipindi cha leo jumapili cha Hamza KasongoChannel 10 .waziri kivuli wa fedha Zito Kabwe amezidi kusisitiza katika bajeti ya mwaka wa fedha 2012/2013 msimamo wake uko palepale huku akiomba wabunge wamuunge mkono kwani mpaka sasa yeye na january pekee ndio ambao hawachukui posho
 
Zito leo kaweka mambo hadharani kuwa ni yeye pekee ndani ya CDM hajachukua posho za vikao akiwa bungeni. Mbowe na wengineo toka CDM wameshindwa kutekeleza kivitendo hoja ya kupinga posho.
Posho kuiacha yataka imani hawa jamaa hawatendi wanachokihubiri majukwaani na tunafahamu kuwa nao Chadema wanauhadaa tu umma wa Watanzania!
 
Huyu anachukua posho kwa shemeji yake mzungu wa barrick
 
Ni unafiki wa aliyekuwa waziri wa fedha kukataa ku design form ambazo wabunge wasiotaka posho badala yake kutumia kisingizio eti posho zinakwenda moja kwa moja kwenye akaunti!!!!!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Posho kuiacha yataka imani hawa jamaa hawatendi wanachokihubiri majukwaani na tunafahamu kuwa nao Chadema wanauhadaa tu umma wa Watanzania!

Nadhani ni wakati sasa wanasiasa watwambie ukweli watapunguzaje matumizi makubwa na ya anasa kama ununuzi wa v8 maposho makubwa yasiyolingana na hata kima cha chini cha mshahara, mpango ambao tunahitaji kuona ndani ya vyama vyetu na hata ktk misimamo yao.
 
Zito leo kaweka mambo hadharani kuwa ni yeye pekee ndani ya CDM hajachukua posho za vikao tangu Julai 2011 akiwa bungeni. Mbowe na wengineo toka CDM wameshindwa kutekeleza kivitendo hoja ya kupinga posho. Hongera Shibuda kwa kuwa muwazi

Zitto hawezi sema hayo hata kidogo. Kwanza posho inalipwa kwenye akaunti ya mbunge na hapo haulizwi mtu. Wanaangalia attendancy yako then unadakishwa na asikudanganye mtu na ZK UNAMSINGIZIA. Umenoa na mbinu zenu za kuvuruga uongozi wetu wa cdm.
 
We ulikuwa unamsikiliza peke yako? kaya semea wapi hayo? au unalako jambo Mafilili. Ni kawaida ukiwa gamba lazima uwe mwongo
 
binadamu kaumbwa na tamaa ila tamaa ikizidi ni uchafu..
na kama binadaamu unahusudu uchafu,basi we ni wa kuokopwa..
wapokea posho wote ni wachafu.(tamaa mbaya).
na watoa posho wote ni zaidi ya uchafu,wananuka(uroho wa madaraka)..
hebu hii siri-kali ya ccm iwaonee huruma walala hoi wa tz..
rais JK,hata aibu!!!! posho ndo nini?..
bigup zitto.utakumbukwa daima..
 
Pamoja na hayo yote, posho iko kwa misingi ya sheria ya nchi na zito wenu anajua. Kama ni kuitoa pia itatolewa kwa misingi hiyo hiyo. Zitto bado hajamaliza kile kihela cha hongo ya Barrick kwenye tume ya kuchunguza mikataba ya madini. Huyu marope nae yuko na change za shemeji zake na kale ka usd 5mil ka wakati uuleee kanawasumbua. Cha mwisho ni tatizo lao kubwa hawa madogo wote. Wanatafuta popularity kwa kugandamiza wenzao bila sababu. Na hata hivyo wasijidanganye. Watanzania wako macho na kila siku nasema. Zitto hawezi na hatokuwa Rais wa nchi hii na hata huyo rafiki yake alomnyima sahihi ya 70.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Neno posho katika context ya wabunge ni pana sana. Wanachopinga CHADEMA ni 'seating allowance' na sio hela za kijikimu kama malazi ya mafuta. Hela za kijikimu zinaingia moja kwa moja kwenye account ya mbunge, sasa sijui kama Zitto na Janaury wanazitoa na kurudisha kwa Spika au vipi.

Kumbuka mbunge anaweza kufanya vikao hata vitatu kwa siku na kila anapohudhuria kikao anatakiwa ku-sign kwa seating allowance. Hiki ndicho wanachopinga CHADEMA na ndio maana walisema kama ndivyo basi waalimu nao wapewe standing allowance.
 
We ulikuwa unamsikiliza peke yako? kaya semea wapi hayo? au unalako jambo Mafilili. Ni kawaida ukiwa gamba lazima uwe mwongo

HAUTAKI KUAMINI? KATAMKA KUPITIA HAMZA KASONGO HOUR-CHANNEL TEN. Leo wabunge wako wameumbuka
 
Nadhani CDM katika kikao hiki watafanya maamuzi magumu na kukataa posho za vikao. Wapige tu moyo konde wamuunge mkono zitto. Kama wanaona Zitto atapata umaarufu kwa hilo basi wakae wampe Mwenyekiti nguvu ya kulitamka ama wampe chief whip wao aliseme.
 
Back
Top Bottom