Wabunge wa Cdm wakatwa mapanga,waokolewa na polisi!

Ralphryder

JF-Expert Member
Nov 16, 2011
4,933
1,294
Jana usiku wamekutwa kata ya kirumba ibanda wakituhumiwa kugawa mlungula na kupigiwa kelele za wezi na watu. Ni Kiwia na Machemuli,hali zao mbaya kwa majeraha ya mapanga. Source wapo rdo.
 
Ahsante Angel nilikuwa nimeshaamini duh leo inabd niwe mwangalifu nisekamatwa tena masikio,
 
Ahsante Angel nilikuwa nimeshaamini duh leo inabd niwe mwangalifu nisekamatwa tena masikio,

Sidhani kama redio ya watumishi wa Mungu ina siku ya wajinga. Si uulize kwa walio karibu nao? Sio kuamini siku ya wajinga basi hakuna matukio ya kweli!
 
Nimekupa source,shauri yako usipoamini.

wangekua wa ccm kama wale waliokamatwa jana kule mbeya ambao ni mh anna kilango na mafisadi wenzake mpaka polisi ikabidi iwalinde kwa mabomu ya machozi ningeamn,but kwa CDM hawana tabia hiyo
 
Mlungura!? Tabia hii CDM wameanza lini?

ushahidi wa Mlungula hauko wazi ila wananchi walipoona magari ya wah. Yakiranda nyumba hadi nyumba usiku,wakaamua kuchukua sheria mkononi na kuwapigia mwano wa kelele za wezi na kuharibu magari yao vibaya na kuwajeruhi kwa silaha za jadi hadi polisi walipofika na kupiga risasi hewani na kuwaokoa.
 
ushahidi wa mlungula hauko wazi ila wananchi walipoona magari ya wah. Yakiranda nyumba hadi nyumba usiku,wakaamua kuchukua sheria mkononi na kuwapigia mwano wa kelele za wezi na kuharibu magari yao vibaya na kuwajeruhi kwa silaha za jadi hadi polisi walipofika na kupiga risasi hewani na kuwaokoa.

ukiona ivyo jua ccm mambo yamewaelemea, duh roho zinawauma ccm kwani hawakuzoea stiff competition kama enzi izo za ccm nambari one.. Te te te sku izi raha pia utamu, ccm maji ya shingo, ushindi kwao ni kwa mbinde na kuiba
 
SIO UONGO SOMENI HAPA


Tupo Hospitali ya Bugando hapa. Ndg. Kiwia, mb anatoa maelezo kwa maafisa wa polisi.

Kuna mmoja wa majeruhi ambaye yupo hapa mwanzoni alisema yeye ni mtu wetu na ameumizwa pia. Imegundulika ni mtu wa UVCCM, Ahmed Mkilindi ambaye ndiye alikuwa anaongoza kikosi kilichowavamia kina Kiwia. Amepata jeraha mkononi (friendly fire?). Mwenyekiti wa CCM mkoa yupo hapa kaja kumwona. Nimewaambia Polisi mtu huyu asitolewe hospitali kinyemela bali atoe maelezo polisi kwanza. Huyu ni mtuhumiwa wa kwanza kabisa.

Hali ya ndg. Kiwia sio nzuri sana. Anatakiwa kufanyiwa ct scan kuona athari aliyopata (maana kapigwa na shoka na mapanga kichwani). Bahati mbaya hapa Bugando kifaa hicho hakifanyi kazi.

Nimezungumza na Katibu wa Bunge na ndani ya muda mfupi ndg. Kiwia atasafirishwa kupelekwa Muhimbili kwa uangalizi zaidi.
Ndg. Machemuli anaendelea vizuri alitoka hospitali jana (alipata huduma ya Kwanza Sekou Toure).

Siasa za Tanzania zinazidi kujidhihirisha kuwa hazina tofauti na nchi nyingine za Kiafrika. Chama cha siasa kuwa na makundi ya wahuni na kupiga watu ni hatari na chama hicho kinakosa 'moral' authority ya kutawala.

Tusubiri uchunguzi zaidi wa Polisi. I am so depressed
 
HIYO HAPO JUU NI KALULI Y ZITTO HIZI HAPA ZINGINE



Zitto Zuberi Kabwe ‏ @zittokabwe
Mbunge wa Ilemela ndg. Kiwia amepigwa mapanga usiku wa kuamkia jana na kundi la watu wanaodhaniwa ni wa #CCM. Amelazwa Bugando @JamiiForums

Zitto Zuberi Kabwe ‏ @zittokabwe
This isnt April fool. Ndg. Kiwia kapigwa mapanga, amelazwa. Ndg. Machemuli wa Ukerewe naye kapigwa. Inasikitisha sana nchi yetu inafika hapa

Zitto Zuberi Kabwe ‏ @zittokabwe
@nanyaro_ guys i dont entertain this fool thing. Tupo hospitali ndg. Kiwia amejeruhiwa kwa mapanga
 
Back
Top Bottom