Wabunge wa ccm wataka madiwani wakopeshwe magari

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,385
Wabunge wataka madiwani wakopeshwe magari Send to a friend Saturday, 16 April 2011 08:31 0diggsdigg

Boniface Meena
WABUNGE wa CCM, wameishauri serikali ifanye jitihada za kupeleka fedha za mikopo kwenye halmashauri, ili kuwawezesha madiwani, kupata mikopo ya kununulia vyombo vya usafiri na hatmaye, kuwafikia wananchi kwa urahisi.

Baadhi ya wabunge hao pia wamelaumu upotoshaji uliofanywa na wabunge wenzao, kuhusu mikopo ya magari iliyotolewa na serikali kwa wabunge wote nchini.

Akichangia Azimio la Bunge la kutenganisha mfuko wa mikopo kwa wabunge na ule wa watumishi wa serikali, Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango, alisema ni muhimu serikali ikashusha mikopo katika serikali za mitaa, ili kuwawezesha madiwani, kukopa na kununua vyombo vya usafiri, vitakavyowawezesha kuwafikia wananchi wa maeneo yao na kujua kero zinazowakabili.

"Serikali ione umuhimu wa kuharakisha mikopo kwenye serikali za mitaa,ili madiwani waweze kukopa na kununua vyombo vya usafiri ili waweze kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi kuliko ilivyo sasa,"alisema Kilango.

Kilango pia alitoa malalamiko yake kuhusu baadhi ya wabunge kupotosha mkopo wa Sh90 milioni, uliotolewa na serikali kwa wabunge wote kwa ajili ya kununulia magari."Zile milioni 90 zilikuwa ni mkopo kwa wabunge wote na si kwamba tumepewa na serikali. Tunakatwa kwenye mshahara ya kila mwezi, wananchi watuelewe,"alisema Kilango.

Mbunge wa Nzega, Dk Khamis Kigwangala, alisema ni muhimu madiwani nao wakapatiwa mikopo ya vyombo vya usafiri ili waweze kuwatumikia wananchi kwa uharaka zaidi.

"Madiwani nao wapewe mikopo ili waweze kuwafikia wananchi kwa haraka na kutatua matatizo yao,"alisema Dk Kigwangala.Pia alionyesha kukerwa na upotoshaji wa baadhi wabunge kuhusu mikopo iliyotolewa na serikali.Alisema wenzao walitoa kauli ambazo hazifai na zinaoashiria kama nao hawakuchukua mikopo hiyo.

"Upotoshaji wa mikopo ya vyombo vya usafiri baada ya kupewa mikopo, wenzetu walitoa kauli ambazo hazifai. Hakuna kitu cha ajabu mbunge kupewa mkopo wakati anakatwa kwenye mshahara wake,"alisema Dk Kigwangala.

Mbunge wa Ukonga, Eugen Mwaiposa, naye aliiomba serikali itoe mikopo kwa madiwani na iende mbali zaidi hadi kwa wenyeviti wa serikali za mitaa kwa kuwa wao ndiyo wako karibu zaidi na wananchi
Wabunge wataka madiwani wakopeshwe magari
 
Tusiogope kukopa, nisingeunga mkono kama ingekuwa kupewa bure huo utakuwa mkopo si watarudisha! Watz tusiwe wepesi wa kupinga kila wazo
 
Hii ni balaaa,

wanasiasa ndo wanaonekana wanafaa kurahisishiwa maisha kwa kupewa usafiri n.k lkn tunasahau kwamba kuna watumishi wa serikali wanaofanya kazi muhimu za kijamii na bado wana chapa lapa(wanatembea kwa mguu kutekeleza majukumu yao kikazi).

Sasa jicho kama limewamulika madiwani ambao kipindi chao cha kuwa madarakani ni miaka mitano ni bora pia liangazie hata kwa watumishi wa serikali ambao kazi zao ni endelevu kama vile
1 Walimu
2 Madaktari
3 Maafisa wa serikali wanaoshughulika na ukaguzi maeneo mbalimbali ya kazi
4 Maafisa kilimo
Na wengineo kwenye vitengo muhimu ambao hawana nyenzo za kuwasaidia kufanya kazi kwa ufanisi.
 
Hii ni balaaa,

wanasiasa ndo wanaonekana wanafaa kurahisishiwa maisha kwa kupewa usafiri n.k lkn tunasahau kwamba kuna watumishi wa serikali wanaofanya kazi muhimu za kijamii na bado wana chapa lapa(wanatembea kwa mguu kutekeleza majukumu yao kikazi).

Sasa jicho kama limewamulika madiwani ambao kipindi chao cha kuwa madarakani ni miaka mitano ni bora pia liangazie hata kwa watumishi wa serikali ambao kazi zao ni endelevu kama vile
1 Walimu
2 Madaktari
3 Maafisa wa serikali wanaoshughulika na ukaguzi maeneo mbalimbali ya kazi
4 Maafisa kilimo
Na wengineo kwenye vitengo muhimu ambao hawana nyenzo za kuwasaidia kufanya kazi kwa ufanisi.

hawa wabunge wengine sijui hata wamefikaje bungeni, tutegemee mengi zaidi
 
Back
Top Bottom