Wabunge wa CCM wana mkutano Kasulu mjini

kajunju

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
999
315
Wabunge wa ccm wana mkutano wa hadhara.wabunge walioteuliwa na rais ndiyo wamekuja kuelezea mchakato wa katiba mpya.nitawajuza kadiri ninavyoweza.kwa mbali namuona mkuu wilaya dan makanga yupo na josephna ngenzabuke
 
Mbunge wa ccm viti maalum mkoa wa tabora.ameongea anavyoweza ila jazba imetawala kwa mama huyu
 
Wameulizwa kama wamekuja kichama au kiserikali. Wanaulizwa mbona hawakuusisha wananchi kabla ya mswada haujaenda bungen na kupitishwa? Mkutano unaanza kuvurugika kwa zomeazomea
 
Makanga ameingilia kati zomeazomea. Anaeleza miaka 50 ya uhuru na si katiba mpya
 
Kajunju nakuomba usiondoke hapo wasikilize kwa makini wananchi wanapouliza maswali na kila yanapojibiwa na wabunge wa Magamba,jitahidi kila yanapoulizwa maswali yenye kuvuta hisia za watu uthabarishe,maana kama swali la kwa nini hawakuuleta mswaada ujadiliwe na wananchi kwanza kabla ya kupelekwa bungeni ni swali la msingi,leo wanajifanya kupiata huko waulizeni hata katiba ya zamani kwanini walikuwa hawaitembezi.
Mkuu endelea kutuhabarisha
 
Mh josephine na huyu mama mwingine wameshndwa.makanga anajibu maswali. Anaeleza anani eti tusiwe kama burund.
 
Mkutano umekwisha. Aibu imewakuta hawa akina mama.piki pik kila mtu kapewa lita 5 ndo wanawaondoa hapa
 
mkutano ulikuwa na mvutano.walisema wameweka maslahi ya watanzania kwanza na si vyama. wananchi wakawaeleza washushe bendera ya ccm kama wako kiserikali zaidi.wameulizwa je wabunge wengine kama machali na zaituni mbona hawajausishwa kwenye mkutano huu.wHuyu mbunge wa tabora viti maalumu hamna kitu.:lol:
 
Cha ajabu ni kipi wabunge hao kuwa na mkutano?

Hakuna cha ajabu wao kuhutubia ila wamefungua macho ya wengi. Kwanza waliingia kwa msafara wenye pikipiki wenye bendera za ccm akiwemo Dani Makanga kaimu DC. Mkutano ukaanza DC akaanza kuongea bila kufanya utambulisho wa wageni Rasmussen bali aliwatambulisha makatibu wa ccm wilaya na mkoa, Josephine ngenzabuke mb Viti maalum akaanza kuongea pumba huku akiwashukuru wananchi kwa kumchagua awe mbunge(viti maalum hawachaguliwi) wananchi wakamzomea akashuka kisha mb viti maalum tabora akapandana kuongea kuhamasisha uchangiaji wa katiba. Mwisho makanga akafanya majumuisho akaanza kusoma sheria ya rasimu ya katiba na adhabu za kujadili katiba. Akawaambia wananchi wajadili hiyo sheria. Mwananchi mmoja aliuliza kwa nini muswada wa sheria yenye vitisho hivyo haukuletwa kwa wananchi kabla haijasainiwa na kwa nn ina vitisho kwa wananchi pia kama mkutano huo ulikuwa wa kuhamasisha katiba kwa nini DC alianza kutambulisha makatibu wa ccm kigoma na yule wa kasulu bila ya kutambulisha viongozi wa vyama vingine. Aluminum kibabe na majibu alitoyatoa kwanza walimzuia muuliza swali asiendelee kuuliza kwani atamaliza muda wa kuuliza maswali mengine. Huyu mkuu wa wilaya hana tofauti na hao wabunge wa viti maalum kwani wote ni wa kuwekwa ili wafurahishe wakubwa Baba riz. Wanafuata upepo tu hawana lolote kichwani. Natamani viti maalum vifutwe na DC wote watimuliwe kwani hawana kazi madc kazi yao kuijenga ccm kwa hela zetu
 
Cha ajabu ni kipi wabunge hao kuwa na mkutano?

Ajabu haikuwa mkutano bali maudhui ya mkutano wenyewe.walieleza kuwa na nia moja kwenye hoja ya katiba mpya. Mwanzon walikuwa wapi?kama wanashrikiana mbona wabunge wa nccr wenye majimbo hatukuwaona? Kwanin mswada ulipitishwa kwanza then ndio wanakuja kuturaghai? Mama tau nawe bado unadanganywa?mwishon hoja ya katiba waliiacha makanga akaanza kuubil miaka 50 ya uhuru,eti basi apa 2 mwnza walitumia siku 3 leo ni siku 1. Je mswada una miaka 50 ya uhuru?
 
Hakuna cha ajabu wao kuhutubia ila wamefungua macho ya wengi. Kwanza waliingia kwa msafara wenye pikipiki wenye bendera za ccm akiwemo Dani Makanga kaimu DC. Mkutano ukaanza DC akaanza kuongea bila kufanya utambulisho wa wageni Rasmussen bali aliwatambulisha makatibu wa ccm wilaya na mkoa, Josephine ngenzabuke mb Viti maalum akaanza kuongea pumba huku akiwashukuru wananchi kwa kumchagua awe mbunge(viti maalum hawachaguliwi) wananchi wakamzomea akashuka kisha mb viti maalum tabora akapandana kuongea kuhamasisha uchangiaji wa katiba. Mwisho makanga akafanya majumuisho akaanza kusoma sheria ya rasimu ya katiba na adhabu za kujadili katiba. Akawaambia wananchi wajadili hiyo sheria. Mwananchi mmoja aliuliza kwa nini muswada wa sheria yenye vitisho hivyo haukuletwa kwa wananchi kabla haijasainiwa na kwa nn ina vitisho kwa wananchi pia kama mkutano huo ulikuwa wa kuhamasisha katiba kwa nini DC alianza kutambulisha makatibu wa ccm kigoma na yule wa kasulu bila ya kutambulisha viongozi wa vyama vingine. Aluminum kibabe na majibu alitoyatoa kwanza walimzuia muuliza swali asiendelee kuuliza kwani atamaliza muda wa kuuliza maswali mengine. Huyu mkuu wa wilaya hana tofauti na hao wabunge wa viti maalum kwani wote ni wa kuwekwa ili wafurahishe wakubwa Baba riz. Wanafuata upepo tu hawana lolote kichwani. Natamani viti maalum vifutwe na DC wote watimuliwe kwani hawana kazi madc kazi yao kuijenga ccm kwa hela zetu

Nakupa tano mkuu.kumbe tulikuwa wote!
 
Mbona hata Chadema nao huweka mikutano ?

Wewe umetumwa au ni magamba, ule haukuwa mkutano wa chama cha siasa ila ulikuwa mkutano wa kuhamasisha uchangiaji wa katiba. Sasa unaropoka chadema wanafanya mkutano. Waliokutuma kawaambie tumekustukia wakipange upya
 
Back
Top Bottom