Wabunge wa CCm waliotia sahihi maisha yao hatarini.

cha maana hapa Lugola amesema yaliyoko moyoni mwake na kizuri zaidi amemuanika hadharani katibu wake jinsi alivyo wa hovyo kusimamia mambo ya kitaifa.

kikubwa hapa ni ujumbe.
 
Ndio tunajua chama kinakufa lakini Mukama kama kiongozi lazima aonekane anakisaidia, mbona kuna wengine wamo humo humo wanaonekana?

pole sana mukama hayupo pale kusaidia chama,kazi yake ni kufuga ndevu
magamba ni nooma!
 
Wilson Mukama sio MWANASIASA.

Hilo ndo kosa CCM walifanya. Nahisi JK ameamua kuua CCM hasa baada ya kupita kwenye lile zengwe la CC wakati anagombea urais.

Sio mbaya ngoja tuone na hao magwanda watafanya nini. Kupokezana uongozi ni kitu kizuri kwa kweli
 
Kazi ya Mbunge ni nini? (Kutetea maslahi ya chama na viongozi wake au ......?)
 
Tunamuomba Mkama asifanye nchi kama mali yake aelewe kuwa nchi ni mali ya watanzania wote ndio maana wabunge wanaapa kulinda sheria zote ikiwa ni pamoja na kuisimamia serikali, sasa je kama serikali inafanya vibaya mbunge asiseme akiogopa mkama???? who is mkama in this country, je yeye ndo anahaki ya kuona mali zetu zinaibiwa nasi tunamuachia sio kwa hilo haiwezekani.
 
Ccm ni wauwaji jamani
huyu mbunge na mwenzake walisoma nyakati huyu mkama sio kabisa ana roho ya kusahaulisha watu muwe makini mtashaulika mkatupa wabunge wa gafula chadema oohh
 
Hiyo ni haki yako Mhe Mbunge, na mwambie Mukama akae kimya hana point. Badala ya kuwashughulikia viongozi wabovu anakufuata wewe. Hii ni hatari sana. Kama ni kweli basi, namwogopa kama ukoma.
 
Tuna mwambia Mkama nchi ni wananchi.wananchi wakifa kwa njaa ya ufisadi wanaofanya yeye ataongoza nini?
Naye mwisho wake unafika.
 
CCM wanajidhallsha so ni msimamo wa chama kuwaibia watanzania na wabunge wao wote lazima wausupport!
Pambufu,mliosign you dont have to worry you have somewhere to go kama wakiwasumbua ie CDM.
Mna haki ya kuwatete watanzana ata Mungu atawapa thawabu!
 
Kufuatia wimbi la vitisho linalotolewa na Katibu Mkuu wa CCM,Wilson Mukama kwa wabunge wa chama hicho waliotia saini Waraka wa Zitto wa kutokuwa na imani na Waziri Mkuu,mbunge mmoja amedai kuwa Mukama hawezi kuwatishia nyau.Nikizungumza na mmoja wa Wabunge hao jana jioni,Mbunge huyo alinidokeza kuwa Mukama amechelewa kukarabati chama chake kinachowalea Mawaziri wezi.Mbunge huyo maarufu kwa kipato anayetokea Mkoa wa Baba wa Taifa alinidokeza kuwa Mukama ataishia kuwatisha 'wengine' na hatathubutu kumsogelea yeye.

Mbunge huyo alishangazwa na Mukama kuingilia kisichomuhusu huku yeye(Mukama) akiwa ndiye msimamizi wa sera ya kujivua gamba ya CCM.'Huyu Ndugu yangu sijui amekuwaje tena?!' aliuliza kwa mshangao Mbunge huyo.

Je,Mukama anacheza mdundo anaouelewa?
 
Wasiguse kabisa Nimrod Mkono, ni shughuli nyingine hiyo........ana uwezo wa kuitangaza Musoma Vijijini kama Nchi yake maana anafanya kila kitu mwenyewe..barabara, shulem hospitali, zahanati, ect
 
Nilitarajia Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu kutoa Press Release kukanusha habari hii.
 
walakini kiomgozi nimehamasika bila kukuuliza chanzo cha taarifa japo nakuaminia
Kufuatia wimbi la vitisho linalotolewa na Katibu Mkuu wa CCM,Wilson Mukama kwa wabunge wa chama hicho waliotia saini Waraka wa Zitto wa kutokuwa na imani na Waziri Mkuu,mbunge mmoja amedai kuwa Mukama hawezi kuwatishia nyau.Nikizungumza na mmoja wa Wabunge hao jana jioni,Mbunge huyo alinidokeza kuwa Mukama amechelewa kukarabati chama chake kinachowalea Mawaziri wezi.Mbunge huyo maarufu kwa kipato anayetokea Mkoa wa Baba wa Taifa alinidokeza kuwa Mukama ataishia kuwatisha 'wengine' na hatathubutu kumsogelea yeye.

Mbunge huyo alishangazwa na Mukama kuingilia kisichomuhusu huku yeye(Mukama) akiwa ndiye msimamizi wa sera ya kujivua gamba ya CCM.'Huyu Ndugu yangu sijui amekuwaje tena?!' aliuliza kwa mshangao Mbunge huyo.

Je,Mukama anacheza mdundo anaouelewa?
 
Huyu Mukama! Naona hata wangemuacha Makamba ingekuwa bora, Sijui kaifanyia nini CCM tangu aingie. Hana ubavu wa kumtisha mbunge yeyote, hata wa TLP.
 
Back
Top Bottom