Wabunge wa CCm waliotia sahihi maisha yao hatarini.

Wabunge waoga wanataka kuwatisha wabunge mashujaa mazuzu kweli kweli. Hivi mbunge kama Kangi Lugora unamtishia kufa wakati kwao hadi wanawake wanahudhuria mikutano ya siasa wakiwa na mapanga. Usimtishe Lugora kwa hilo, yeye kaamua kuwa shujaa basi haina mjadala.
 
wakijiengua wakagombea majimbo yao kupitia upinzani wanachukua jimbo wala wasihofu
 
Hao wabunge warudi majimboni kwao wakawasemee hao viongozi wao wa chama kwa wananchi tena ikiwezekana wawataje mpaka majina
 
(Nimejaribu kuiharisi habari hii ili isomeke kwa mtiririko mzuri, tunashukuru aliyetulletea. Mtoa mada au Mod wanaweza kuiweka hii ili watu waisome vizuri. Thanks)

BAADHI ya wabunge wa Chama cha Mapinduzi, walioshiriki kusaini hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa nia ya kushinikiza kujiuzulu kwa mawaziri wanaotuhumiwa kufuja mabilioni ya fedha, wametishiwa maisha. Habari za kuaminika zilizothibitishwa na mmoja wa wabunge hao, zimesema kuwa wabunge wawili kati ya wanne wa chama hicho wamelazimika kuukimbia mji wa Dodoma na kujificha kwa muda kusikojulikana. Wabunge hao (majina yao tunayo) waliondoka mjini Dodoma mara baada ya kupewa taarifa na watu wao wa karibu kuwa walikuwa wakisakwa kwa vile baadhi ya wakubwa ndani ya CCM walikuwa wamechukizwa na kitendo hicho.

Akizungumza na Tanzania Daima, mmoja wa wabunge waliokimbia na kujificha, amedai kuwa alilazimika kufanya hivyo baada ya kushauriwa sana na rafiki zake, ingawa awali aligoma kuondoka akisema angekuwa tayari kukabiliana na lolote hata kufa kwa vile anaamini hajafanya kosa lolote la kuhatarisha amani ya nchi. “Ni kweli niko nje ya Dodoma, nimefanya hivi baada ya kuwepo kwa hisia hizo, maana naziita hivyo kwa sababu binafsi siogopi kutishwa,” alisema mbunge huyo.

Kwa upande wake, Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe (CCM) ambaye ni mmoja wa wabunge wa chama hicho waliotia saini hoja hiyo, alikiri kupigiwa simu za shutuma na lawama kwa madai ya kukisaliti chama na kuunga mkono hoja ya wapinzani ya kutaka kuwawajibisha mawaziri wanaoitumikia serikali ya chama hicho. Filikunjombe alisema ingawa hajapata vitisho rasmi, lakini alijua hatua hiyo ingemgharimu. Alisema kuwa hajutii hatua hiyo kwa sababu ndiyo mahali pekee pa kusemea na kwamba kama asipoyasema yeye machungu ya Watanzania, hajui nani atayasema. Mbunge huyo machachali na asiye na woga aliongeza kuwa ni wajibu wake kukisadia chama chake kwa moyo mnyoofu na kuwasilisha kilio cha Watanzania na cha wananchi wa Ludewa.

Alizidi kumshambulia Waziri wa Kilimo na Chakula, Jumanne Maghembe, kwa kuzembea na kupeleka mbolea ya kupandia jimboni kwake Ludewa mwezi Machi badala ya mwezi Oktoba, tena ikiwa feki. “Katika hali ya hovyo kiasi hiki, walitaka nicheke na kutetea upuuzi eti kwa sababu nalinda chama? Nimechaguliwa na watu kuwalinda na kuwaletea maendeleo sio umaskini. Kibaya wamewakopa hata mawakala. Badala ya kunisaidia na kuwawajibisha waliofanya uzembe huu eti nalaumiwa mimi,” alisema.

Lugola apigiwa simu ya vitisho Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola, alipigiwa simu juzi saa saba za usiku na kiongozi mmojam wa juu wa CCM akimtaka ajiandae kwa mapambano kwa kile kilichoelezwa kuwa amekisaliti chama. Akithibitisha tukio hilo, Lugola alisema kuwa kiongozi huyo mzito (jina tunalo) ambaye ni bingwa wa kufoka na kutukana vyombo vya habari vinavyomkosoa, alimwita mbunge huyo mnafiki, mzandiki na kwamba kwa hatua yake ya kusaini hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu atambue kuwa ametangaza vita. “Ni kweli nilipigiwa simu na.. (anamtaja) na kuanza kunifokea na kunitukana. Nilishindwa kuamini kama kiongozi mzito kama yeye anaweza kuniambia maneno hayo. Nami nilimwambia kwa kuwa sina kosa na nimetumia haki yangu, afanye lolote analoweza.” Mbunge huyo alisema pamoja na kuambiwa kuwa leo kigogo huyo wa CCM atafika Dodoma kumshughulikia na wale wote tuliotia saini, haogopi lolote na yuko tayari kukabiliana nam magumu kwa ajili ya maslahi ya Watanzania. Hata wakiniua, sitaogopa naamini katika ukweli na ni kilio cha wengi. Lakini wengi wananiunga mkono, na wamenipigia simu na wanakubali kuwa wako nyuma yangu.

Alisema maisha ya Watanzania ni mabaya, shuleni hakuna walimu wala madawati, hospitali ziko taabani kwa kukosa dawa huku madaktari wakililia maslahi, na kila wakati serikali imekuwa ikidai haina fedha kumbe, zipo na zinaliwa na wajanja. “Hakuna cha kunitisha katika hali kama hii. Wanaonitisha ndiyo wasioitakia mema CCM na Watanzania na hao lazima tuwashughulikie mchana kweupe. Na katika hili, lazima wote bila kujali wao ni nani lazima wajiuzulu bila kusubiri eti wajipime na kutafakari,” alisema Lugola.
 
huyu nadhani wa mikoani,magazeti yanachelewa kufika. kwake yeye hii breaking news!mwacheni jamani ni mtu wetu huyo.
 
kafanya vizuri maana tu wengi wavivu wa kusoma na kukumbuka pia, tumpongezi kwa hilo japo ni copying and paste
 
Hao ni ccm ni mafia-esque mob. Ndio maana wanaamini katika vitisho, uuaji na dhuluma. ccm hawana traits za civil political party so wenye kutishwa should take it seriously.
 
"Wanaonitisha .................lazima tuwashughulikie mchana kweupe. Na katika hili, lazima wote bila kujali wao ni nani lazima wajiuzulu bila kusubiri eti wajipime na kutafakari,” alisema
Lugola.
[/QUOTE]

Ahsante baba!. Usiogope, Mungu atakulinda tu maana moyo wako ni mweupe na dhamira yako ni safi. Hakuna wa kukudhuru maana sasa mwisho wa wenye meno umefika, waondoke tubaki wenye mioyo tujenge nchi yetu. Tumechoka!.

Baba ahsante sana.
 
ITS JUST A MATTER OF TIME........Watanzania wameamasika kwa kiasi kikikubwa wabunge Majasiri wote kutoka CCM walioamua kuwajali wananchi na kuwakacha wazandiki(Magamba) Ni waakikishie tu hata kama watafanya hayo ambayo wao wanafikiri kuwa ndiyo suluhisho kwako moja najua ikiwa ni kuwanyima nafasi ya kugombea tena na hata kuwanyang`anya kadi za unachama kama wanauthubutu huo. Watakuwa wabunge kupitia chama kingine na siyo lazima CCM.
 
Kanji Lugola wa Mwibara alidai jana kwamba usiku wa kuamkia Jumapili, siku moja baada ya kusaini hati kwa Zito Kabwe alipokea simu kutoka kwa Mukama akimtolea maneno makali kutokana na hatua yake hiyo. “Alizungumza maneno mengi ya vitisho kwa mfululizo bila hata kunipa nafasi ya kujieleza, akasema, ‘nakuja huko wewe na huyo mwenzako mliosaini mtanitambua,’ kuona hivyo tukaondoka Dodoma usiku huohuo,” Lugola alieleza.

Nami nilimwambia kwa kuwa sina kosa na nimetumia haki yangu, afanye lolote analoweza.”“Hata
wakiniua, sitaogopa naamini katika ukweli na ni kilio cha wengi.
Lakini wengi wananiunga mkono, na wamenipigia simu na wanakubali kuwa wako nyuma yangu.

Alisema walisafiri hadi Dar es Salaam na kwamba walihudhuria kikao cha Bunge cha Jumatatu iliyopita wakitokea mafichoni.Alipotakiwa kuthibitisha madai hayo Mukama alisema: “Siwezi kutoa habari kwa simu.”

Alipopigiwa tena na kuombwa afuatwe ofisini alisema, “Kwa leo haitawezekana maana niko njiani natokea Dodoma sasa hivi nimefika Gairo, kama unaweza njoo kesho.”


Chanzo: Tanzania Daima na Mwananchi
 
Hatari, nadhani kama huwa hao akina Mukama wanaenda chooni basi wafahamu sasa ni wakati wa uharo maana hayo mabadiliko na uelewa wa wananchi sasa ni 100% hakuna anayeweza kuyazuia! Nadhani sasa ni wakati wa wabunge wa CCM wapime, maana hata wakienda CDM wanashinda tu uchaguzi, tena CDM hakuna zengwe. Mi namshauri mtu kama Deo ahamie CDM kwani bado ni kijana mno kuishi na mafisadi.
 
ccm labda ya kwenye makaratasi (maana siijui vizuri), hii ya watu inatia shaka sana!
 
Mukama ameishiwa baada ya kushindwa hata kupambana na kivuli cha Yusuf Makamba. Inashangaza ule ujasiri aliokuwa nao wakati akiwa Mkuu wa jiji umeyeyukia wapi.
 
Naomba niulize kwa vitisho kama hivyo mbunge hawezi kufungua mashtaka? Kidhibiti ni simu hiyo wakaprint tu. naomba nieleweshe. Hata Rais akashitakiwe kwa wananchi ili aondoke wananchi sio wakinfa. Tume hoka na huu $$$$@@@.
 
Kama hatafungua mashtaka, then ntajua ni yaleyale ya magamba, perepete nyingi, kazi kiduchu
 
Magamba bana! Hapo angekua ametishiwa na kiongozi wa CDM kesi ingekua mahakamani tayari lakini kwa sababu ni mwenzao wanaogopa sijui wanalindana..
What a shame!!
 
Mbona hawamtishi Filikunjombe au Mkono? Labda wanaona hapo ni mdebwedo lakini piga ua garagaza kama mbunge atamnyooshea Mukama ni wazi Mkama ataufyata mkia.
 
Hivi hii nchi imerogwaa!!? Haina wa kukemea, watu wanauana wanatishiana maisha, hakuna kinachoendelea!!?
 
Mukama ameishiwa baada ya kushindwa hata kupambana na kivuli cha Yusuf Makamba. Inashangaza ule ujasiri aliokuwa nao wakati akiwa Mkuu wa jiji umeyeyukia wapi.

Mukama ndiye anae iangamiza ccm,bora Mzee Makamba alikuwa ana pambana kisawasawa na Dr.SLAA.ULIKUWA UNAMSIKIA MAKAMBA LEO YUKO ZIARANI HUKU NA KULE,LAKINI MZUZU WA KAMBALE NI ZOBA.
 
Back
Top Bottom