Wabunge wa ccm wajijutia.

Mnyaturu

Member
Dec 28, 2011
82
11
Baada ya kulaani na kushindwa kusaini hoja ya zito kabwe ya kutokua na imani na waziri mkuu wakimuogopa mkuu wa nchi kumbe naye rais alikua anafurahia wabunge walivyokuwa wanajadili.wadai wangesaini wangejiongezea umaarufu wa kisiasa kwenye majimbo yao kwa kuonekana wapiganaji.source greatethinker
 
Hawana haja ya kujisikia vibaya...
Walipima hoja ya zito na kuipuuza,sasa hawana chaguo tena,muda umepita,waishi matokeo ya uamuzi wao.
Hata hivyo ,kama wanataka kujiongezea umaarufu kwa wananchi wao bado hawajachelewa ,wajitoe CCM mara moja.
Hii ndiyo njia pekee & uhakika ya kujiongezea umaarufu waliyobakiwa nayo.
 
kigwangala ni mmoja wao,kijana bt anashindwa hata na wazee wakina lugola kusoma alama za nyakati.haya sasa hata mkuu amefurahia na wewe endelea kutetea chama kaka.
 
Jk alimtuma zitto wao walikuwa hawajui; CAG ilipelekwa kwa jk kwnz akataka iende biungeni km ilivyo, tatizo la wabunge wengi wa ccm hawajui kusoma ala;a za nyakati.
 
Na watajuta sana mwaka huu na ikifika 2015 ndio watalia kabisa na kusaga meno
 
Wengi wao ni mazuzu hawajui kinafanywa na mwenyekiti wao.JK sasa hivi ni chadema 90%,yeye ameshasoma alama za nyakati na ndo maana sasa hivi hataki kupingana na CDM by any way!!.JK tunakutakia kila la kheri katika kutimiza harakati uliyoianza.WTZ tuko nyuma yako!! Kill CCM Kill!!!.
 
Unajua wanasema ukimwona samaki anapiga reverse (anaogelea kinyumenyume) basi ujue amekufa. Sasa wabunge wengi wa CCM ndiyo wanatembea reverse kwenda kwa wananchi wao kuelekea mwaka 2015
 
Mimi naamini ni propaganda tu za JK lakini lazima mkwara ulitembea
 
Nawashangaa sana hasa hao vijana,nilichogundua kumbe mfumo hapa ndiyo tatizo,si wazee wala wa ukongwe ndani ya chama bali ni ule ugonjwa unaoitwa(MKNC) Maslahi Na Chama Kwanza.
 
Magamba bwana, hiyo ndiyo shida ya mtu kushindwa kufikiri kwa kutumia akili zako alafu unatarajia mtu mwingine afikiri kwa ajili yako. Hamna kitu hapo
 
Mbona MKNC haiendani na tafsiri ya Maslahi Na Chama Kwanza? Labda ungesema (MNCK)
 
Ni kweli wabunge wengi wa ccm walidhan ni wimbi tu litapita ndio maana wachache walioona mbali walitia sahihi zao.
Na sasa wachache hao wanajivunia uhuru wao kamili ndan ya ccm.
Hata hivyo waliogopa ni uvivu wao tu wa kufikiri kwan hawajachaguliwa na ccm bali ni wananch wanaopaswa kuwaogopa ama kuwatii na sio viongozi wa ccm.
 
Hongera kwa Mh. Deo Filikunjombe, anastahili Salute

Baada ya kulaani na kushindwa kusaini hoja ya zito kabwe ya kutokua na imani na waziri mkuu wakimuogopa mkuu wa nchi kumbe naye rais alikua anafurahia wabunge walivyokuwa wanajadili.wadai wangesaini wangejiongezea umaarufu wa kisiasa kwenye majimbo yao kwa kuonekana wapiganaji.source greatethinker
 
Tatizo lenu nchi nzima na hata humu JF ni kama mmelewa mvinyo wa kudanganywa na siasa zinazotokea nje ya Bunge.

Hivi nani kawaambia kwamba Zitto kaondoa hoja yake kama Slaa mwaka 2007 alivyoondoa BUngeni hoja yake ya EPA.

Hoja ya Zitto ya kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu leo imebakisha siku 4 tuanze kuhesabu ni lini Spika ataitisha Bunge ili kumpigia kura Pinda kwa kutokuwa na imani naye.

Nilikaa kimya humu tangu Kigwangwala alipowadanganya sababu zake za kutosaini hoja ya Zitto kana kwamba kusaini ni jambo la msingi sana wakati hata kama CCM asingesaini hata mmoja, maadam wamefika 20% basi kinachofuata ni kupigiwa kura Bungeni.
Kigwangwalah hatuna haja ya kujua wazo lake kuhusu hoja hii maana hujui moyoni mwake ndiye atakuwa wa kwanza kupiga kura ya NDIYO ya kumuondoa Pinda maana ni siri.

Cha msingi ni kwamba wote tuelewe na tusidanganywe kwamba siku 14 zinakaribia kuisha na hivyo kama sisi ni thinkers basi nafasi yetu ni pale siku 14 za hoja ya Zitto zitakapotimia tuwahinikize Bunge liitishwe. Najua Zitto na wenzake wanalijua zaidi hili.

Kuna thread humu baadhi tuliipuuzia lakini naona inaelekeza kila kitu:

www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/259819-kitanzi-cha-zitto-kinavyomtesa-spika-serikali.html

Kutoipeleka Bungeni hoja ya Zitto maana yake ni uhaini kwani uhaini ni kuvunja katiba kwani Katiba ndiyo inaipeleka hoja ile Bungeni na siyo Makinda, Kikwete, wewe au mimi.
 
Ni kweli wabunge wengi wa ccm walidhan ni wimbi tu litapita ndio maana wachache walioona mbali walitia sahihi zao.
Na sasa wachache hao wanajivunia uhuru wao kamili ndan ya ccm.
Hata hivyo waliogopa ni uvivu wao tu wa kufikiri kwan hawajachaguliwa na ccm bali ni wananch wanaopaswa kuwaogopa ama kuwatii na sio viongozi wa ccm.
Pamoja na ujinga wa hao wabunge kushindwa kusoma alama za kisiasa, lakini na viongozi wa chama chao wanawapiga chenga za kisiasa pia. hakukuwa na dalili kuwa chama kama chama kina msimamo gani katika hili. Mimi nilikuwa Dodoma na kilichokuwa kikionekana ni kutokuwepo kwa msimamo kwa viongozi wa juu wa CCM na serikali. Walikuwa wanayumbishwa kama bendera. Mwanzoni Zitto alipoanzisha hoja ya vote of no confidence, waliona kama masihara, walioona hoja inaanza kuwa na mashiko, ndio wakaanza kuhangaika na wakaja na suluhisho la zima moto.
 
Sasa ule mkwara wa Mukama kwa wabunge walio saini uko wapi kama Bosi wake mwenyewe karidhia? Kweli sasa hivi CCM inaendeshwa kama club ya Kangara kule kijijini kwetu. Mwenyekiti ana kauli zake, anakuja Mukama naye analonga kikwao bado mzee wa Mipasho (Nape) naye ana wimbo wake. Bora hata kusikiliza Mdumange maana una mpangilio maridadi.
 
Wajanja tanzania wako wawili tu.
1.Jk
2.Zitto
wengìne nì kupelekeshwa 2.Hoja ya wazri mkuu kujiuzuru ulikúwa mkakati wa kumwongezea zitto umaarufu kwa ajili ya 2015 jk analifahamu hlo
 
Back
Top Bottom