Wabunge wa CCM mzigo usiobebeka (e.g Hamis Kigwangalla)

wabunge wetu ban wanapoteza hela zetu bure.
maana wao ni copy and peste kutoka kenya na uganda.mi naona hamna haja ya kuwa na bunge.
 
Maji Marefu naye huwa anafuka moshi mpaka najuta kuangalia kipindi cha bunge
Yeye alimng'ang'ania zaidi Babu wa Loliondo na kikombe chake. Alidai yeye ni zaidi ya huyo Babu na amezunguka dunia nzima. Akina Wassira wanamwacha pale wanakwenda kwa Babu. Matokeo yake ni usingizi zaidi!
 
mzee Selelii yuko mjini Nzega anakula mitaa tu kila siku.Sijui kama anampango wa kugombea tena
"ni bora kuwa na mbunge aliyeishia form four kuliko Daktari wa kuiba elimu
Selelii, Mpendazoe, MzeeMwanakijiji hawatamsahau Mh Sitta.
 
Selelii, Mpendazoe, MzeeMwanakijiji hawatamsahau Mh Sitta.

Hii statement sioni kama ina ushirikiano,...
umeanza kwa kutaja wabunge,then mwanakijiji ulikua unalenga kusema nini?
kwamba mwanakijiji alikua mbunge pia na sasa sio?

kila mpenda nchi hata sahau uongozi wa sitta bungeni
 
Niko mbele ya Luninga, namsikia Ndugu Tundulisu akichangia juu ya misamaha ya kodi kwa wawekezaji,nikamuelewa vizuri sana juu ya hoja zake.Akasimama mbunge wangu Ndugu H.A Kigwangala(Said Bagaire) akaanza kuwatetea wawakezaji na kuunga mkono hoja kwamba wawekezaji eti wanaleta ujuzi.
Ikumbukwe kuwa huyu mbunge alikuja na sera ya kuandamana(AMKA NZEGA) kwenda mgodini kwa ajili ya mgodi kufungwa kwa vile hauna faida kwa wazawa wa Nzeaga.
1.Kweli ni yule aliyetuambia atakuja kwa ajili ya kuandamana ndiye anayeogea hayo,
2.Kwa kutuacha hewani wana Nzega ni kwamba ametudharau kwa kutudanganya?
3.Je mkutano wake wa mwezi wa 4 jimboni Nzega alikuwa anatupotezea muda wetu?

Kama unakua mbunge, halafu huna falsafa yako kichwani, unaburuzwa na vikao vya bunge kamati ya CCM utaadhirika. Utasahau hata ulichoongea jana. Hata mimi nilimsikiliza nikaona amepoteza nework, hao jamaa waliomchagua wameliwa.
 
hana sababu ya kupima wingi wa sauti za wabunge kwani anaelewa yuko pale kimaslahi zaidi
 
kuna muda wabunge wanachangia misuada mradi wasikike na hata wakiunga mkono wanaelewa wanachounga mkono si sahihi na kile ambacho wananchi wa majimbo yao wanatarajia .. undumilakuwili lazima kwao
 
Back
Top Bottom