Wabunge wa CCM, mawaziri wanaopotosha maudhui ya michango ya kambi ya ushindani kichefuchefu!

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,619
2,567
Ndugu wanaJF, nadhani hata nyinyi mmekuwa mkikerwa na baadhi ya wabunge wa CCM na mawaziri wanaodhani wao tu ndio wanaofuata sheria na wafuasi wa vyama vingine hawazifuati. Hotuba iliyosomwa na Godbless Lema bungeni hivi karibuni, inapotoshwa makusudi na wabunge wa CCM na mawaziri hadi inatia kichefuchefu. Hotuba inaongelea uhalisia wa Wizara ya Mambo ya Ndani na kilichotakiwa ni kuiboresha wizara hiyo na si kutetea uozo uliom maana huko si kuwasaidia Watanzania wanaonyanyasika kwa kuuawa na jeshi la polisi, kunyanyaswa, kubambikiwa kesi, rushwa nk. Kutaja kasoro hizo kwa nia ya kuliboresha jeshi hilo na idara nyinginezo siyo uchochezi hata kidogo na wala siyo kuvunja sheria. Wanaovunja sheria ni wale wanaokiuka wajibu wao kwa kutumia nguvu zaidi hata mahali ambapo haihitajiki na kusababisha vifo vya raia. Ni aibu! wanaChadema wanaposema wataandamana kwa amani (si kwa kuchukua silaha) ni pale serikali itakaposhindwa kutimiza wajibu wake na si pale ambapo inatekeleza na kwenye hotuba nzima hakuna sehemu wanayosema wanataka vita au watatumia vita kupigania haki hizo. Na maandamano ya amani ni sauti ya wanyonge kudai haki zao. Lakini baadhi ya wabunge wa CCM na mawaziri katika michango yao wamekuwa wakiupotosha umma kama kawaida yao kuwa Chadema wanataka kuleta vita. Tafsiri hii imetoka wapi? Chadema wanasema katika kutetea haki za wananchi, ambazo wanaona zinanvunjwa na watawala na vyombo vya dola, watatumia maandamano ya amani kupeleka ujumbe kwa umma kuhusu uvunjwaji wa hizo haki ili hatimaye wananchi wao wenyewe (people’s power) waweze kuona ni chama gani kinafaa kiwe madarakani na ni kipi kinapaswa kiwapishe wengine uchaguzi ukifika. Kusema hivi si kuhamasisha vita bali ni kuwafanya wananchi waamke na wajue ni chama gani kinatetea maslahi yao. Kama kuna vita yoyote itatokea, ni wazi haiwezi kuletwa na chama kisicho na polisi wala jeshi bali chama tawala chenyewe. Na kwa nini serikali ikikosolewa baadhi ya wabunge wa CCM wanatetea? Kusudi lao hasa ni nini? Wanataka nchi iendelee kuporwa kama inavyofanyika sasa hivi? Wanataka polisi na askari magereza waendelee kufanya unyama wanaoufanya kwa raia na wafungwa ‘respectively’ kama ilivyosomwa kwenye hotuba ya Lema? Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani alidai ripoti aliyonukuu Lema ni ya zamani na si ya sasa na hivyo kukana kabisa kama unyanyasaji huo bado upo. Lakini nilisoma ripoti nyingine hivi karibuni (utafiti wake ni June 17-July 17, 2009) ambayo itatoka hivi karibuni (nadhani) kuhusu hali ya wafungwa kwenye magereza yetu nchini ni mbaya sana (bado kuna vitendo vya unyanyasaji na uvunjaji wa haki za binadamu). Mauaji ya raia yanayofanywa na jeshi la polisi kulingana na ripoti ya Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu nayo ni uvunjwaji wa haki za binadamu. Kwa bahati mbaya, baadhi ya watawala wanadhani kuvunja haki za binadamu siyo kuvunja sheria za nchi wakati Tanzania imeridhia Tangazo la Haki za Binadamu na maazimio mbalimbali ya kimataifa na kukubali baadhi ya maazimio hayo yawe sehemu ya sheria za nchi halafu mtu anasimama na kudhani kuvunja haki za binadamu siyo kuvunja sheria za nchi! Ibara ya 8(1) inasema: “Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo - (a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii; (b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi; (c) Serikali itawajibika kwa wananchi;(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.” Kama lengo la seriakli ni ustawi wa wananchi [Ibara 18(1)(b)], je, unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za binadamu usipolalamikiwa na kurekebishwa, ustawi huo wa wananchi utapatikanaje?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom