Wabunge wa CCM kuonesha kutokuwa na imani na serikali lazima kuwe na matokeo

ukweli nikwamba kuna nguvu kubwa nyuma ya haya yote, ni kama tsunami ndani ya bahari na tunalioliongelea sisi ni athari zake na sio chanzo! hebu turudi nyuma na kutafakari haya yametokea wapi? kwanini CAG and Katibu mkuu wafanye maamuzi hayo aliyoyafanya kwani ni dhahiri kuwa wanajua wanachokifanya!!! pia waziri mkuu hakukurupuka, naye pia alijua anachokifanya!

wakuu, hivi ni vita vya mafahali wawili... i see this to be deeper than what we have managed to ponder so far!
 
wABUnge wa ccm na serikali yao lao moja ni full usaniii hakuna jipya hiyo tume ni blah blha blah tuuuu
 
Pinda huyu asingekuwa Ziro Mtanzania angesha tangaza kujiuzuru lkn kwa kuwa ni Ziro atakuja nampya Ijumaa analihutubia Bunge kuahirisha sasa sijui atakuja na nini mpya kwa watz.
 
Mi binafsi nawashangaa sana wale wanaosema Pinda ajiuzulu, wakati Pinda mwenyewe alisema hana madaraka ya kumuwajibisha Jairo, sasa wenye maamuzi wameshafanya nyie mnakimbilia kumdandia Pinda, na hili muvu la Jairo nilishalishitukia tangu siku ile Pinda anasema hana mamlaka ya kumwajibisha Jairo kwa sababu sikuona mtu mwingine mwenye unafuu wa kumwajibisha mwenzie kwa sababu wote ni walewale na yaliyofanyika ndiyo mi niliyoyategemea na nimeshangaa kuwaona wengine wakishangaa haya maamuzi
 
Pinda hatakiwi kujiuzuru kwa sababu hajatoa maamuzi yoyote yaliyopingwa.

Asilimia kubwa ya wachangiaji wanataka kutuaminisha kwamba Pinda alisema angekuwa na authority angemfukuza Jairo.

Ili kumaliza ubishi ninanuku alichotamka:

{..kwa jinsi hili lilivyokaa huwezi kulitetea. Ningependa nije hapa niseme ni nini maamuzi yangu. Lakini nikaambiwa kuwa hili ni juu ya uwezo wangu..}

Nani anajua kwamba maamuzi ya Pinda ilikuwa kumfukuza Jairo na si kufanya uchunguzi.

Mbona hata bunge litaunda kamati si ya kuunda tuhuma za kumfukuza Jairo bali kamati ya kulitafiti hili na kuleta mapendekezo.

Fikirini kabla ya kupayuka.
 
Pinda hatakiwi kujiuzuru kwa sababu hajatoa maamuzi yoyote yaliyopingwa.
Asilimia kubwa ya wachangiaji wanataka kutuaminisha kwamba Pinda alisema angekuwa na authority angemfukuza Jairo.
Ili kumaliza ubishi ninanuku alichotamka:

{..kwa jinsi hili lilivyokaa huwezi kulitetea. Ningependa nije hapa niseme ni nini maamuzi yangu. Lakini nikaambiwa kuwa hili ni juu ya uwezo wangu..}
Nani anajua kwamba maamuzi ya Pinda ilikuwa kumfukuza Jairo na si kufanya uchunguzi.
Mbona hata bunge litaunda kamati si ya kuunda tuhuma za kumfukuza Jairo bali kamati ya kulitafiti hili na kuleta mapendekezo
Nadhani si maamuzi yaliyopingwa kama unavyoeleza, kujiuzulu ni pmoja na mtazamo tofauti wa mambo, dhana tofauti au misimamo tofauti. Unaposema hakuna mahali alipopingwa una ji limt katika kutumia dhana nzima kwa kuchagua neno moja.

Tunachokiona sas hivi tulishakiona na kukipigia kelele kuwa huwezi kufanya uchunguzi halali kwa watu walio na uhusiano wa karibu tukasahuri iundwe tume huru ili tupate ukweli sio kuunda tuhuma. Leo bunge limeamua kuunda tume jambo linaloonekana kama kuunda tuhuma.
Hapa ndipo tatizo lilipo. CAG amchunguze PS anayewajibika kwa CPS anayewajibika kwa President! ukiachilia mbali natural justice inayotuonyesha mahusiano ya mamlaka hizi, tunafamu Jairo/Luhanjo/Kikwete ni marafiki wa kikazi na nje ya kazi. Tutegemee nini wakichunguzana!!

Kwanini Pinda ajiuzulu! Yeye ni kiongozi wa shughuli za serikali bungeni. Anashauriwa na AG, Mwanasheria wa bunge, na kupata ushirikiano wa uongozi wa bunge kwa kiwango anchohitaji. Kiongozi wa serikali bungeni anajua taratibu zote za bajeti kama waziri wa zamani, mwanasheria, na PM. Inapofikia mahali akasema 'hii huwezi kuitetea' alishajirisha kuwa kuna jambo ambalo si sawa kwabisa.

Aliposema anasubiri Rais atue ili amweleze ni ushahidi kuwa hili jambo lilikuwa ni kubwa na zito.
Luhanjo amesafisha Jairo na wala hakuna anayehoji hilo kwasababu lilitakiwa lihojiwe kabla ya uchunguzi wa (nguchiro, nyani na tumbili)
Nashukuru nafsi yangu hainisuti hata kidogo kwasababu niliandika hapa Jf kuhusu suala hili na utata wa uchunguzi.

Kinachotusukuma tuamini Pinda anapaswa kujiuzulu si kwa makosa yoyote aliyofanya bali kutokana na majibu ya Katibu mkuu kiongozi yanayomdhalilisha na kuondoa credibility yake kwa umma.

1. Katibu mkuu anasema Jairo hana kosa! Waziri mkuu na kiongozi wa serikali bungeni Mh Pinda hakujua kuwa hilo si kosa, hakujua kuwa utaratibu wa kugawa fedha ni wa kawaida akiwa PM. Akatoa kauli iliyoonyesha kuwa kulitakiwa uchunguzi halali 'hii huwezi kuitetea', lakini Katibu mkuu kiongozi ameweza kuitetea kwa uchunguzi wake ambao ulizuia vyombo vingine isipokuwa CAG. Je, huo ndio ulikuwa mtazamo na dhana ya Mh Pinda?

2. Kiongozi wa shughuli za serikali kuambiwa hadharani hakuna taratibu zilizokiukwa na katibu mkuu kiongozi ni kumdhalilisha Pinda.
Sisi wananchi sasa tunajua kuwa Mheshimiwa Pinda hajui analolifanya kama kiongozi wa serikali bungeni na pengine kauli nyingi anazotoa kama kiongozi huwa zina uwalakini, na kwa mantiki hiyo inabidi sasa tumsikilize Katibu mkuu kiongozi zaidi. Heshima ya Pinda iko wapi?

3. Alipoomba wabunge watulie wakati anashughulikia kwa ushirikiano na Rais, hakusema kama Pinda bali kama PM, msaadizi wa kushoto mwa Rais!
Kauli yake inapoyeyushwa kienyeji namna hiyo katika uchunguzi usiokuwa halali na wa haki ni kumdhalilisha sana Pinda.
Leo ataongea nini bungeni tumwamini? ushahidi ni jinsi alivyotumia cheo chake cha Uwaziri mkuu kumzushia Jairo ndani ya Bunge!!!!!!!

4. Anatakiwa sasa asimame mbele ya bunge, amuombe radhi Jairo na aombe radhi Umma. Kama anaamini hiyo ni sawa basi aendelee kufanya hivyo ili kulinda masilahi yake ya U-PM na unga kwa ujumla hata kama ni kwa dhalili.
Kama hakubaliani na hayo ikiwa ni pamoja na uchunguzi na taarifa ya Ikulu, hapo hakuna chaguo ila KUJIUZULU.
 
Mwanakijiji hapana na ndio!

Ni wajibu wa wabunge wa Chama Tawala Kuitete chama kwa yale mambo pekee ambayo ni Ilani ya Chama na mipango mema ya chama hasa yanayofuata katiba ya chama hicho, siyo kwa matendo na mienendo mibovu ya wanachama wenzao au viongozi wa chama chao, inapofikia hapo lazima wabunge wasimame upande wa wananchni siyo chama.
 
Nadhani si maamuzi yaliyopingwa kama unavyoeleza, kujiuzulu ni pmoja na mtazamo tofauti wa mambo, dhana tofauti au misimamo tofauti. Unaposema hakuna mahali alipopingwa una ji limt katika kutumia dhana nzima kwa kuchagua neno moja.

Tunachokiona sas hivi tulishakiona na kukipigia kelele kuwa huwezi kufanya uchunguzi halali kwa watu walio na uhusiano wa karibu tukasahuri iundwe tume huru ili tupate ukweli sio kuunda tuhuma. Leo bunge limeamua kuunda tume jambo linaloonekana kama kuunda tuhuma.
Hapa ndipo tatizo lilipo. CAG amchunguze PS anayewajibika kwa CPS anayewajibika kwa President! ukiachilia mbali natural justice inayotuonyesha mahusiano ya mamlaka hizi, tunafamu Jairo/Luhanjo/Kikwete ni marafiki wa kikazi na nje ya kazi. Tutegemee nini wakichunguzana!!

Kwanini Pinda ajiuzulu! Yeye ni kiongozi wa shughuli za serikali bungeni. Anashauriwa na AG, Mwanasheria wa bunge, na kupata ushirikiano wa uongozi wa bunge kwa kiwango anchohitaji. Kiongozi wa serikali bungeni anajua taratibu zote za bajeti kama waziri wa zamani, mwanasheria, na PM. Inapofikia mahali akasema 'hii huwezi kuitetea' alishajirisha kuwa kuna jambo ambalo si sawa kwabisa.

Aliposema anasubiri Rais atue ili amweleze ni ushahidi kuwa hili jambo lilikuwa ni kubwa na zito.
Luhanjo amesafisha Jairo na wala hakuna anayehoji hilo kwasababu lilitakiwa lihojiwe kabla ya uchunguzi wa (nguchiro, nyani na tumbili)
Nashukuru nafsi yangu hainisuti hata kidogo kwasababu niliandika hapa Jf kuhusu suala hili na utata wa uchunguzi.

Kinachotusukuma tuamini Pinda anapaswa kujiuzulu si kwa makosa yoyote aliyofanya bali kutokana na majibu ya Katibu mkuu kiongozi yanayomdhalilisha na kuondoa credibility yake kwa umma.

1. Katibu mkuu anasema Jairo hana kosa! Waziri mkuu na kiongozi wa serikali bungeni Mh Pinda hakujua kuwa hilo si kosa, hakujua kuwa utaratibu wa kugawa fedha ni wa kawaida akiwa PM. Akatoa kauli iliyoonyesha kuwa kulitakiwa uchunguzi halali 'hii huwezi kuitetea', lakini Katibu mkuu kiongozi ameweza kuitetea kwa uchunguzi wake ambao ulizuia vyombo vingine isipokuwa CAG. Je, huo ndio ulikuwa mtazamo na dhana ya Mh Pinda?

2. Kiongozi wa shughuli za serikali kuambiwa hadharani hakuna taratibu zilizokiukwa na katibu mkuu kiongozi ni kumdhalilisha Pinda.
Sisi wananchi sasa tunajua kuwa Mheshimiwa Pinda hajui analolifanya kama kiongozi wa serikali bungeni na pengine kauli nyingi anazotoa kama kiongozi huwa zina uwalakini, na kwa mantiki hiyo inabidi sasa tumsikilize Katibu mkuu kiongozi zaidi. Heshima ya Pinda iko wapi?

3. Alipoomba wabunge watulie wakati anashughulikia kwa ushirikiano na Rais, hakusema kama Pinda bali kama PM, msaadizi wa kushoto mwa Rais!
Kauli yake inapoyeyushwa kienyeji namna hiyo katika uchunguzi usiokuwa halali na wa haki ni kumdahalilisha sana Pinda.
Leo ataongea nini bungeni tumwamini? ushahidi ni jinsi alivyotumia cheo chake cha Uwaziri mkuu kumzushia Jairo ndani ya Bunge!!!!!!!

4. Anatakiwa sasa asimame mbele ya bunge, amuombe radhi Jairo na aombe radhi Umma. Kama anaamini hiyo ni sawa basi aendelee kufanya hivyo ili kulinda masilahi yake ya U-PM na unga kwa ujumla hata kama ni kwa dhalili.
Kama hakubaliani na hayo ikiwa ni pamoja na uchunguzi na taarifa ya Ikulu, hapo hakuna chagou ila KUJIUZULU.

I like common sense... you are a great thinker. Keep it up...
 
Hivi ni nani alimuagiza CAG kufanya uchunguzi wa sakata la Jairo?
Kama kumbu kumbu zangu zipo sahihi ni Katibu mkuu Kiongozi. Alitoa ufafanuzi kuwa amemwagiza CAG afanye uchunguzi na baada hapo ikidhihirika kuna tuhuma atawasilina na Jairo kumjulisha tuhuma halafu hatua zitafuata.

Alipotoa taarifa jana ni ushahdi wa yeye kupokea taarifa ya CAG na kuifanyia kazi, hakuna chombo kingine kilichotoa taarifa.
 
Nadhani si maamuzi yaliyopingwa kama unavyoeleza, kujiuzulu ni pmoja na mtazamo tofauti wa mambo, dhana tofauti au misimamo tofauti. Unaposema hakuna mahali alipopingwa una ji limt katika kutumia dhana nzima kwa kuchagua neno moja.

Tunachokiona sas hivi tulishakiona na kukipigia kelele kuwa huwezi kufanya uchunguzi halali kwa watu walio na uhusiano wa karibu tukasahuri iundwe tume huru ili tupate ukweli sio kuunda tuhuma. Leo bunge limeamua kuunda tume jambo linaloonekana kama kuunda tuhuma.
Hapa ndipo tatizo lilipo. CAG amchunguze PS anayewajibika kwa CPS anayewajibika kwa President! ukiachilia mbali natural justice inayotuonyesha mahusiano ya mamlaka hizi, tunafamu Jairo/Luhanjo/Kikwete ni marafiki wa kikazi na nje ya kazi. Tutegemee nini wakichunguzana!!

Kwanini Pinda ajiuzulu! Yeye ni kiongozi wa shughuli za serikali bungeni. Anashauriwa na AG, Mwanasheria wa bunge, na kupata ushirikiano wa uongozi wa bunge kwa kiwango anchohitaji. Kiongozi wa serikali bungeni anajua taratibu zote za bajeti kama waziri wa zamani, mwanasheria, na PM. Inapofikia mahali akasema 'hii huwezi kuitetea' alishajirisha kuwa kuna jambo ambalo si sawa kwabisa.

Aliposema anasubiri Rais atue ili amweleze ni ushahidi kuwa hili jambo lilikuwa ni kubwa na zito.
Luhanjo amesafisha Jairo na wala hakuna anayehoji hilo kwasababu lilitakiwa lihojiwe kabla ya uchunguzi wa (nguchiro, nyani na tumbili)
Nashukuru nafsi yangu hainisuti hata kidogo kwasababu niliandika hapa Jf kuhusu suala hili na utata wa uchunguzi.

Kinachotusukuma tuamini Pinda anapaswa kujiuzulu si kwa makosa yoyote aliyofanya bali kutokana na majibu ya Katibu mkuu kiongozi yanayomdhalilisha na kuondoa credibility yake kwa umma.

1. Katibu mkuu anasema Jairo hana kosa! Waziri mkuu na kiongozi wa serikali bungeni Mh Pinda hakujua kuwa hilo si kosa, hakujua kuwa utaratibu wa kugawa fedha ni wa kawaida akiwa PM. Akatoa kauli iliyoonyesha kuwa kulitakiwa uchunguzi halali 'hii huwezi kuitetea', lakini Katibu mkuu kiongozi ameweza kuitetea kwa uchunguzi wake ambao ulizuia vyombo vingine isipokuwa CAG. Je, huo ndio ulikuwa mtazamo na dhana ya Mh Pinda?

2. Kiongozi wa shughuli za serikali kuambiwa hadharani hakuna taratibu zilizokiukwa na katibu mkuu kiongozi ni kumdhalilisha Pinda.
Sisi wananchi sasa tunajua kuwa Mheshimiwa Pinda hajui analolifanya kama kiongozi wa serikali bungeni na pengine kauli nyingi anazotoa kama kiongozi huwa zina uwalakini, na kwa mantiki hiyo inabidi sasa tumsikilize Katibu mkuu kiongozi zaidi. Heshima ya Pinda iko wapi?

3. Alipoomba wabunge watulie wakati anashughulikia kwa ushirikiano na Rais, hakusema kama Pinda bali kama PM, msaadizi wa kushoto mwa Rais!
Kauli yake inapoyeyushwa kienyeji namna hiyo katika uchunguzi usiokuwa halali na wa haki ni kumdhalilisha sana Pinda.
Leo ataongea nini bungeni tumwamini? ushahidi ni jinsi alivyotumia cheo chake cha Uwaziri mkuu kumzushia Jairo ndani ya Bunge!!!!!!!

4. Anatakiwa sasa asimame mbele ya bunge, amuombe radhi Jairo na aombe radhi Umma. Kama anaamini hiyo ni sawa basi aendelee kufanya hivyo ili kulinda masilahi yake ya U-PM na unga kwa ujumla hata kama ni kwa dhalili.
Kama hakubaliani na hayo ikiwa ni pamoja na uchunguzi na taarifa ya Ikulu, hapo hakuna chaguo ila KUJIUZULU.

Mkuu Nguruvi naenda kukubaliana na wewe. Lakini naona ni vizuri mamba tumwite mamba na sio kenge. Na kuwa Mamba kuwe kuwa mamba tusitumie lugha kugeresha watu na kumuita kenge.

Ukainza kuangalia kwa undani utaona kuwa kwanza ni kosa kwa rais kusema subirini nitakuja kuamua suala la Jairo. Kwanini? Ina maana hatuna mechanism ya kushughulikia mambo kamna rais hayupo, na suala hilo lilikuwa kwenye madaraka ya rais? Si siri kuwa Jairo ni best friend wa JK, na unajua jinsi JK alivyo when it comes to deal with marafiki. Dito aliua alimwambia aendelee kumwomba mungu, na hakusema akamatwe mara moja. Na kwa jairo inaonekana ni kitu kile kile.

Ni vizuri tukubaliane kuwa kuna institutional corruption ambayo ni kama imebarikiwa na kulindwa.Wizara kutumia pesa (whether kwa jina la pesa ya mawasiliano au posho) kuwapatia watu ndani ya bunge wapitishe bajeti, kwa tafsiri yeyote ile iko within the definition of corruption.

Sidhani kama Shelukindo alidanganya, sidhani kama Pinda alikosea......nadhani kilichopo ni kuwa kauli ya kusema nisubri nakuja kushughulikia, haya ndio matokeo yake. Tanzania kila kitu kinawezekana, kuufanya uongo kuwa ukweli na ukweli kuwa uongo. Nadhani Jairo alifanya baya kwa nia njema kwa serikali, si kwa nia mbaya kwa manifaa binafsi. Kwa uozo uliopo wizarani hata kama mimi ningekuwa Jairo, katioka hali ya kawaida hakuna mtu mwenye akili timamu ambaye angekubali bajeti yake ipitishwe.

Kupokelewa kwa vifijo kwa civil servant anaporudi ofisini si kitu cha kawaida kwa Tanzania, kwa hioyo hapa kuna message fulani tunapata.

Ninachosema ni kuwa tukubali kuwa Pinda hata jiuzulu kwa kuwa hakuna kosa alilofanya, tukubali kuwa mchezo wa Jairo ni rushwa, tukubali kuwa ripoti ya Katibu kiongozi ni disappointment.Tutaongea tu lakini for sure hakuna kitakachofanyika.
 
Kama kumbu kumbu zangu zipo sahihi ni Katibu mkuu Kiongozi. Alitoa ufafanuzi kuwa amemwagiza CAG afanye uchunguzi na baada hapo ikidhihirika kuna tuhuma atawasilina na Jairo kumjulisha tuhuma halafu hatua zitafuata.

Alipotoa taarifa jana ni ushahdi wa yeye kupokea taarifa ya CAG na kuifanyia kazi, hakuna chombo kingine kilichotoa taarifa.
UPDATE:
source: mwananchi
Fidelis Butahe
IKULU imemrejesha kazini Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo baada ya uchunguzi wa tuhuma dhidi yake za kutenga mamilioni ya shilingi kwa ajili ya kuhonga wabunge ili wapitishe bajeti ya wizara hiyo, kubainika kuwa si za kweli. Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo alitangaza uamuzi huo katika mkutano wake na waandishi uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam jana akisema Jairo hana hatia na leo anapaswa kurejea kazini mara moja.

Alisema matokeo ya uchunguzi dhidi yake yamebainisha kwamba hakuwa na hatia hivyo kusema kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Sheria namba 8 ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002 na kanuni zake za mwaka 2003, anamrejesha kazini Jairo... "Ninaamuru David Jairo arejee kazini kuanzia siku ya Jumatano (leo)."

Julai 18, Jairo alituhumiwa na baadhi ya wabunge wakati wakichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwamba amezitaka taasisi, vitengo na idara zilizo chini ya wizara hiyo, zichangie Sh50 milioni kila moja, ili kufanikisha bajeti hiyo.

Tuhuma hizo zilitolewa na Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo na kumfanya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuzitolea maelezo Bungeni akisema akama angekuwa na mamlaka, angelitolea uamuzi lakini akaahidi kulifikisha kwa Rais ambaye alisema ndiye mwenye mamlaka ya uteuzi.

Tuhuma nyingine zilizokuwa zimetolewa na Shellukindo ni za kulipa masurufu ya safari za watumishi walio chini ya wizara hiyo na taasisi zake, ambao tayari walikwishalipwa na wizara na taasisi hizo.

Kutokana na tuhuma hizo Luhanjo alimpa likizo ya malipo katibu huyo na Julai 21 alimwandikia barua Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovic Utouh na kumpa siku 10 kufanya uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo ambao alisema haukuweza kuthibitisha tuhuma hizo.

Luhanjo ambaye katika mkutano huo wa waandishi alikuwa na Utouh alisema: "Kutokana na matokeo haya ya uchunguzi wa awali, mimi kama Mamlaka ya Nidhamu ya Katibu Mkuu Nishati na Madini (Jairo), sitaweza kuendelea na hatua ya pili ya kumpa taarifa ya tuhuma. Pia sitampa Hati ya Mashtaka kwa sababu Jairo hajapatikana na kosa la kinidhamu kwa mujibu wa taarifa za ukaguzi maalumu."

Luhanjo alisema mantiki na shabaha ya uchunguzi wa awali dhidi ya mtumishi wa umma anayetuhumiwa ni matakwa ya kisheria kwa mujibu wa Kanuni ya 36 ya Kanuni za Utumishi wa Umma ya mwaka 2003.

"Lengo la kwanza ni kupata ukweli kuhusu tuhuma zinazohusika, pili ni kutaka kubaini kama mtumishi ametenda kosa la kinidhamu.
Tatu, kama uchunguzi huo utabainisha makosa ya kinidhamu, mamlaka ya nidhamu itampa mtumishi taarifa muhimu ambayo itaambatana na Hati ya Mashitaka," alisema.

Akizungumzia madai ya rushwa, Luhanjo alisema tuhuma hizo zisingeweza kuchunguzwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), kwa kuwa hazihusiani na masuala ya utoaji na upokeaji rushwa.

"Kila chombo kina nafasi yake… kama mtu akiona katika ripoti kuna mianya ya rushwa suala hili linaweza kufika Takukuru, Polisi na hata Mahakamani," alisema Luhanjo.

Alisema ni kawaida kwa idara zilizo chini ya wizara husika kuchanga fedha kwa ajili ya kusaidia kufanikisha kitu fulani, huku akisita kuzungumzia kuchafuliwa kwa jina la Jairo akidai suala hilo ni la binafsi na ndiye anayepaswa kulizungumzia.

"Jairo kuomba taasisi zilizo chini ya wizara ya nishati kumwezesha kufanikisha bajeti ya wizara ni jambo la kawaida, kwa kuwa bajeti hiyo pia huzihusisha taasisi zilizopo chini ya wizara husika," alisema Luhanjo.
 
Mkuu Nguruvi naenda kukubaliana na wewe. Lakini naona ni vizuri mamba tumwite mamba na sio kenge. Na kuwa Mamba kuwe kuwa mamba tusitumie lugha kugeresha watu na kumuita kenge.
Ukainza kuangalia kwa undani utaona kuwa kwanza ni kosa kwa rais kusema subirini nitakuja kuamua suala la Jairo. Kwanini? Ina maana hatuna mechanism ya kushughulikia mambo kamna rais hayupo, na suala hilo lilikuwa kwenye madaraka ya rais? Si siri kuwa Jairo ni best friend wa JK, na unajua jinsi JK alivyo when it comes to deal with marafiki. Dito aliua alimwambia aendelee kumwomba mungu, na hakusema akamatwe mara moja. Na kwa jairo inaonekana ni kitu kile kile.
Ni vizuri tukubaliane kuwa kuna institutional corruption ambayo ni kama imebarikiwa na kulindwa.Wizara kutumia pesa (whether kwa jina la pesa ya mawasiliano au posho) kuwapatia watu ndani ya bunge wapitishe bajeti, kwa tafsiri yeyote ile iko within the definition of corruption.
Sidhani kama Shelukindo alidanganya, sidhani kama Pinda alikosea......nadhani kilichopo ni kuwa kauli ya kusema nisubri nakuja kushughulikia, haya ndio matokeo yake. Tanzania kila kitu kinawezekana, kuufanya uongo kuwa ukweli na ukweli kuwa uongo. Nadhani Jairo alifanya baya kwa nia njema kwa serikali, si kwa nia mbaya kwa manifaa binafsi. Kwa uozo uliopo wizarani hata kama mimi ningekuwa Jairo, katioka hali ya kawaida hakuna mtu mwenye akili timamu ambaye angekubali bajeti yake ipitishwe.
Kupokelewa kwa vifijo kwa civil servant anaporudi ofisini si kitu cha kawaida kwa Tanzania, kwa hioyo hapa kuna message fulani tunapata.
Ninachosema ni kuwa tukubali kuwa Pinda hata jiuzulu kwa kuwa hakuna kosa alilofanya, tukubali kuwa mchezo wa Jairo ni rushwa, tukubali kuwa ripoti ya Katibu kiongozi ni disappointment.Tutaongea tu lakini for sure hakuna kitakachofanyika.
Mkuu Bongolander, nakubalina nawe kuwa Mh Shelukindo hakutoa taarifa ya uongo na wala hakufanya kosa kutoa taarifa.
Nilichomaanisha ni kuwa alifanya mapema mno na kuondoa ushahidi.

Mathalani ,kama angesubiri zikagawiwa au kukawa na mtego mzuri ingalijulikana nani amepata nini, na hapo tungekuwa na mahali pa kuanzia kwa maswali haya, ni kwa nini na za nini, iweje kwa abc na sio a-z.

Kuhusu Pinda kama umesoma vema sijasema ana kosa la kumfanya ajiuzulu, ila kutokana na mgongano wa taarifa ni wazi kuwa credibility yake imekuwa compromised sana. Kwa kiongozi mkubwa kama yeye ni dhalili na angefikiria kujiuzulu kwasbababu anasimamia asichokiamini kwa maelezo hata kama yanakinzana na imani yake.

Ndio maana katika hoja yangu namba 4 nimesema anayo nafasi pia ya kuendelea na Uwaziri mkuu hata kama ni kwa dhalili.
 
Sasa naomba mtu anisaidie; kama Luhanjo (katibu mkuu kiongozi) ndiye aliyemuagiza CAG kufanya uchunguzi na kumtaka ampatie taarifa akimaliza ili ajue la kufanya na tena Luhanjo amekuwa mtu wa kwanza kumsimamisha kiongozi mkubwa kazi kupisha uchunguzi - Ballali hakusimamishwa, Mgonja hakusimamishwa n.k na CAG amekuja na kutoa taarifa kwa Luhanjo na Luhanjo akajiridhisha kuwa hakuna tatizo - kwanini basi Wabunge wanataka wao wapewe taarifa ambayo wao hawakuigaza? Ni kitu kinawafanya wabunge waamini kuwa wao ndio walitakiwa wapewe taarifa kwanza kabla ya aliyeagiza uchunguzi?

Kama aliyeagiza uchunguzi ameshaona hakuna makosa, na wabuneg wakapitia ripoti hiyo hiyo na kuona kuwa kulikuwa na makosa nani amwajibishe Jairo? Je haitakuwa the case of "double jeopardy" of sort? Kwamba umeshaonekana huna hatia, iweje ushtakiwe tena kwa kosa lile lile?

Labda nikumbushie; Kamati ya Zitto ya POAC ilimwagiza CAG huyo huyo kufanya uchunguzi wa sakata la ujenzi wa majengo ya BoT ya magavana na alipomaliza aliipatia kamati hiyo ripoti yake na kamati ikatuhakikishia na CAG mwenyewe kwamba hakukuwa na ukiukwaji wowote ule wa sheria au matumizi mabaya ya fedha. Ripoti ile haikutakiwa kuja kusomwa bungeni au kujadiliwa na ilihusu fedha nyingi kuliko hizi za Jairo.

Swali: Kwanini kama kuna kuchezeana akili hapa?

Bunge halina sababu, haki wala mamlaka ya kuingilia huu uchunguzi tena au kumshuku Katibu Mkuu kiongozi. Naogopa kwaamba Bunge linataka au likikubaliwa litakuwa linaingilia kazi ya kila mtu kwa kisingizio cha "tunaisimamia serikali". I oppose with an utmost opposition Kamati Teule kuchunguza sakata ambalo limemalizwa katika mhimili mwingine.

Hilo la Bunge kudharirishwa ni dogo mno kiasi cha kunishangaza kwanini watu wamelifanya kuwa kubwa kuliko. Hivi limekuwa Bunge la mkoloni ambalo mtanzania hawezi kusema ni la kichekesho na akaendelea na shughuli zake?
 
@mwanakijiji

tatizo kabla ya zoezi ili kufika hapo jairo alishatoa kauli ya kuwadhalilisha bunge na wabunge kuwa waigizaji wa comedy , sasa kurudi kwake kumelifedheesha bunge na kulionyesha ni kihisia zaidi

wanaounga mkono waseme ndio...ndiooooooooooooooooo wasiounga mkono waseme sio.....siyoooooooooooooooo nadhani wanaounga wameshinda
 
Pinda hawezi kujiuzulu na Bunge la chama chake likabakua . Akijiuzulu LAZIMA Kikwete avunje na bunge ili wote waanze upya.

MM

1. Asante kwa makala nzuri na elimishi kama zilivyo makala zako nyingi.
2.pinda akijiuzulu lazima Kikwete avunje bunge? Mbona alipojiuzulu Lowasa bunge halikuvunjwa na baraza liliundwa kutoka bunge lile lile. Tofauti ni ipi? Naomba kuelimishwa.
 
Sasa naomba mtu anisaidie; kama Luhanjo (katibu mkuu kiongozi) ndiye aliyemuagiza CAG kufanya uchunguzi na kumtaka ampatie taarifa akimaliza ili ajue la kufanya na tena Luhanjo amekuwa mtu wa kwanza kumsimamisha kiongozi mkubwa kazi kupisha uchunguzi - Ballali hakusimamishwa, Mgonja hakusimamishwa n.k na CAG amekuja na kutoa taarifa kwa Luhanjo na Luhanjo akajiridhisha kuwa hakuna tatizo - kwanini basi Wabunge wanataka wao wapewe taarifa ambayo wao hawakuigaza? Ni kitu kinawafanya wabunge waamini kuwa wao ndio walitakiwa wapewe taarifa kwanza kabla ya aliyeagiza uchunguzi?

Kama aliyeagiza uchunguzi ameshaona hakuna makosa, na wabuneg wakapitia ripoti hiyo hiyo na kuona kuwa kulikuwa na makosa nani amwajibishe Jairo? Je haitakuwa the case of "double jeopardy" of sort? Kwamba umeshaonekana huna hatia, iweje ushtakiwe tena kwa kosa lile lile?

Labda nikumbushie; Kamati ya Zitto ya POAC ilimwagiza CAG huyo huyo kufanya uchunguzi wa sakata la ujenzi wa majengo ya BoT ya magavana na alipomaliza aliipatia kamati hiyo ripoti yake na kamati ikatuhakikishia na CAG mwenyewe kwamba hakukuwa na ukiukwaji wowote ule wa sheria au matumizi mabaya ya fedha. Ripoti ile haikutakiwa kuja kusomwa bungeni au kujadiliwa na ilihusu fedha nyingi kuliko hizi za Jairo.

Swali: Kwanini kama kuna kuchezeana akili hapa?

Bunge halina sababu, haki wala mamlaka ya kuingilia huu uchunguzi tena au kumshuku Katibu Mkuu kiongozi. Naogopa kwaamba Bunge linataka au likikubaliwa litakuwa linaingilia kazi ya kila mtu kwa kisingizio cha "tunaisimamia serikali". I oppose with an utmost opposition Kamati Teule kuchunguza sakata ambalo limemalizwa katika mhimili mwingine.

Hilo la Bunge kudharirishwa ni dogo mno kiasi cha kunishangaza kwanini watu wamelifanya kuwa kubwa kuliko. Hivi limekuwa Bunge la mkoloni ambalo mtanzania hawezi kusema ni la kichekesho na akaendelea na shughuli zake?
Katika mwendelezo wa Balali, Mgonga na kamati ya Zitto kuhusu BoT, niongezee kuwa suala la EPA ni Luhanjo huyo huyo aliunda kamati ya Mwanasheria mkuu(AG), Mkuu wa jeshi la polisi (IGP) na mkuu wa PCCB kufanya uchunguzi na kumpelekea. Hadi leo hakuna anayejua matokeo yake na wala si bunge limewahi kuhoji taarifa.

Kama nimekuelewa unachosema hapa ni kuwa Bunge lilikasimu madaraka yanayohusu suala lake kwa mhimili mwingine na kwa kufanya hivyo lilikuwa tayari kwa matokeo ya aina yoyote.Ni kinyume cha tartibu kukasimu madaraka halafu kuhoji matokeo yake!!
Tatizo ni kuwa walipoambiwa suala hilo lipo juu ya mamlaka ya waziri mkuu wakasahau kuwa waziri mkuu ni sehemu na sio bunge. Kwahiyo walitakiwa wao walifanyie kazi na si kukasimu madaraka na ndicho kinawasumbua. Zaidi ya hapo ni kuwa kwanini kuna double standards kwa baadhi ya masuala ya kitaifa?

Wabunge wetu hawajifunzi kutokana na yaliyopita. Richmond ilifanyiwa usanii huu na kusafishwa na Takukuru, ndipo wabunge walipoomba kuundwa kamati ya Shelukindo(Mr) ambayo iliridhika kuwa upo walakini na kisha kuundwa kamati ya Mwakyembe iliyokuja na taarifa tunayoijua.
Nadhani wanataka kutumia muundo huo. Wasichokijua ni kuwa matokeo yakiwa tofauti hakuna wa kumwajibisha Jairo. Hakuna kwasababu hata taarifa ya Richomnd ilipopelekwa kwa Rais wahusika waliachwa kustaafu tena kwa mafao. Sijui hili la Jairo litakuwa na mtazamo gani tofauti.

Kwa mtazamo huo sidhani bunge litakuwa na nguvu baada ya kupoteza fursa ya awali(missed opportunity) na pengine hili liwe somo lingine kuwa bunge ni chombo chenye uwezo na madaraka pekee na kitendo cha kukasimu madaraka kinalidhalilisha lenyewe kabla ya kdhalilishwa.

Hata hivyo ninabaki kuamini kuwa hadhi ya waziri mkuu na credility yake vimeharibika, ndiyo maana bila makosa ya moja kwamoja ningemsihi ajiuzulu. Ajiuzulu kwasababu kuambiwa hili suala ni taratibu za kawaida ni kumfanya hajui taratibu anazopaswa kusimamia kama kiongozi wa serikali bungeni licha ya kuzungukwa na wataalam wa kisiasa na kisheria lukuki.

Katibu mkuu anapomfundisha kazi waziri mkuu inafikirisha.
Ajiuzulu kwasababu aliposema'hili huwezi kulitetea' nina uhakika alijua anasema nini. Je sasa baada ya shule ya Luhanjo ameelewa somo! na je anaweza kutetea kile alichosema hawezi kukitetea?
Ajiuzulu kwasababu hakuwa na uwezo wa kutoa majibu ya 'taratibu za kawaida' kwa bunge, na hukuweza kusimamia uchunguzi wa tukio, lakini anapaswa amwombe radhi Jairo. Kama ni mchezo wa mpira wa chandimu Pinda amewekwa 'mtu kati'.
 
Always great thnker great thought..nimewapata wanajamvi...mimi nadhani hapa kuna vacant of leadership...kama kwenye vyumba vyamajadiliano awajatoka na msimamo mmoja nadhani hpo akuna cha serikali imara...namatokeo yakutokua na serikali imara ni public conflitation ya watawala wtu...
Lazima sinema hii iwe na matokeo yake, na nadhani pia wabunge wa magamba wawe ready kubeba responsibiliites zao za mahamuzi...
 
Back
Top Bottom