Huelewi maana ya Caucuss.
Caucuss ni hiyari ya mtu , siyo lazima na haxziundwi kisheria.
kwa maneno mengine ni kukaa chemba kabla ya kuja na uamuzi wa pamoja. Ila naona uelewa wako upo mbali kidogo.
Wanaweza wakawa hawana guts, ila uwezo wanao.
Naomba uangalie maana ya caucuss, ni dhahiri kabisa huelewi maana yake.
Wabunge wa CCM kupitia vikao vyao nje na ndani ya Bunge wanao uwezo wa kuwalazimisha Mawaziri wao wajiuzulu. Kinachokosekana hapa ni ujasiri wa kufanya maamuzi!
No hawana uwezo huo. Ibara ya 55 inaweka wazi ni nani anateua mawaziri. Lakini pia Ibara ya 58 ya katiba inaweka wazi pia kazi ya uwaziri itafanywa na mtu kwa ridhaa ya Rais. Maana yake ni kwamba hakuna mamlaka ingine ambayo inaweza kupinga ridhaa ya rais. Hii ni katiba yetu ambayo inamfanya rais kuwa mungu mtu. Ndiyo maana ninasema kuwa wabunge wa CCM na bunge hawana uwezo wa kuondoa mawaziri kwa kuwataka wajiuzulu kwani si kazi yao. Kazi yao wao ni ile inayofanywa na Zitto ya kukusanya sahihi na baadae kura 51% ya kura za kutokuwa na imani na waziri mkuu au 70% kutokuwa na imani na rais. Wabunge wa CCM wafuate katika waache kitchen parliament (caucus). Katiba inawapatia more than kumg'oa ngeleja, wanaweza kumg'oa pinda. Hapo ndipo kwenye urefu wa rungu lao tena wakiwa bungeni siyo kwenye vikao vya jikoni.
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kutoa taarifa kwamba; mimi na Bunge hili halina mamlaka ya Mkurugenzi wa Shirika, Katibu Mkuu wa Wizara au Mkurugenzi wa Halmashauri. Mawaziri ambao wametajwa kwa njia moja au nyingine kutokuwajibika ipasavyo na kuliingizia hasara taifa wamekuwa wagumu sana kuwajibika, wanampa kazi Rais ya kuwafukuza.
Lakini sisi hatuwezi kuwaazimia hapa ila sisi tuna mamlaka na mtu mmoja tu humu ndani ya Bunge; na naomba mnisikilize kwa makini sana. Tuna mamlaka na mtu mmoja tu, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, bila kumwajibisha Waziri Mkuu hawa Mawaziri waliotajwa hawatatoka na wasipotoka madudu haya yatarudia. Kwa hiyo Mbunge yoyote mwenye uchungu na ubadhirifu, Mbunge yoyote ambaye anakereka na watoto kwenye Jimbo lake kukaa chini, Mbunge yoyote anayekereka na madawa kuharibiwa na MSD na MSD kushindwa kupeleka madawa kwenye vijiji vyetu, nampa taarifa kwamba kuanzia kesho tunakusanya sahihi za Wabunge 70, ili siku ya Jumatatu tutoe hoja hapa Bungeni ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, na kipindi hiki tunakitoa Mawaziri wote ambao wapo implicated kwenye taarifa hizi waweze kuona ama wao, au wamtoe rehani Waziri Mkuu. (Makofi)
Kama wanashindwa kuzungunza kwa sauti kuu bungeni ni kitu gani kinachowafanya waweze kuzungunza kwa sauti kuu wakiwa huko caucus? Why someone can sit "with someone in a room yesterday and told him to his face that he has messed and must go for the good of the country" lakini anashindwa kufanya hivyo bungeni? Kweli hiyo tunaweza kuita ni "Courage" kama January Makamba anavyodai?
Kama nilivyoeleza katika post yangu hapo juu,BUNGENI wana hatari ya kupoteza serikali na wanahisi,kwa usahihi kabisa,kuwa, itakuwa sababu ya kukataliwa na wananchi mwaka 2015. Ndio maana ,mara zote, hawaoni kama Bunge ni mahali muafaka kufanyia siasa(misuguano ya kihoja)..Hoja hii inapata nguvu tunaporejea ukweli kuwa baadhi ya wapiganaji dhidi ya ufisadi mfano Selelii ,Shelukindo hawakurudi bungeni mwaka 2010.Kadhalika,Spika Sita hakurudi katika nafasi yake kwa mizengwe ya Kamati kuu ya CCM.Hawajaweza kujenga utamaduni wa kisiasa unaotambua umuhimu na nafasi ya tofauti za mawazo..kwa muda mrefu wameendesha siasa za zidumu fikra za mwenyekiti.
Kwa sasa tuna FILIKUNJOMBE.Kwa kweli itakuwa ngumu kwake kurudi bungeni mwaka 2015 maana ni dhahiri wakuu wa chama hawafurahii misimamo yake.
Nimebaini eneo linaloleta 'utata'.
Wapo ndugu zetu wanadhani tunazungumzia nani anamteua nani?kwamba wateule wa Rais hawawezi kuondolewa katika nafasi zao na wabunge.Hii si sahihi kimantiki hata kidogo tukikubaliana na mtiririko huu hapa chini:
1.Rais anachaguliwa na wananchi wa Tanzania,na anawajibika kwao.
2.Wabunge wanachaguliwa na wananchi wa Tanzania.
3.Rais huchagua MAWAZIRI kutoka wabunge wa Tanzania,na kuwa MAWAZIRI wanajibika kwa wananchi kupitia kwa RAIS.
4.Wananchi wa Tanzania ndio msingi wa utawala,mamlaka na uhalali wa serikali YOYOTE ya KIDEMOKRASIA.
Kwa hiyo,basi,
Kwa kuwa Rais,anawajibika kwa wananchi wa Tanzania,na kwa kwa kuwa wananchi wa Tanzania huiwajibisha serikali yao kupitia wawakilishi wao ambao ni wabunge,kwa kuuliza maswali bungeni,kujadili bajeti ya serikali, ama hata kuleta hoja binafsi bungeni,na kwa kuwa MAWAZIRI 3 walipata kujiuzulu nayadhifa zao mwaka 2008,na kuwa vile vile wamepata kumtia misukouko bwana David JAIRO mwaka 2011, kwa sababu za uwajibikaji,na kwa kuwa maamuzi hayo hayakubatilishwa hadi leo,na yanaweza kuchukuliwa kama rejea, basi uamuzi huo utumike tena katika hoja hii,kwa wawakilishi wa wananchi kuchukua hatua za uwajibikaji dhidi ya mawaziri ambao wanamwakilisha rais,na ambao pia kwa kawaida huchaguliwa na wanachi majimboni, kwa makosa ya uzembe na ubadhirifu.
Which you simply mean that badala ya wabunge wa CCM kutaka mawaziri wafukuzwe kwa kupitia vikao vya Caucus vya CCM wafanye hivyo kwa kupitia chombo cha uwakilishi cha wananchi ambacho ni bunge. Wananchi wanawakilishwa kupitia bunge na sio caucus ya CCM.
Waziri anaweza kujiuzulu anytime, for any reason.Which you simply mean that badala ya wabunge wa CCM kutaka mawaziri wafukuzwe kwa kupitia vikao vya Caucus vya CCM wafanye hivyo kwa kupitia chombo cha uwakilishi cha wananchi ambacho ni bunge. Wananchi wanawakilishwa kupitia bunge na sio caucus ya CCM.
Waziri anaweza kujiuzulu anytime, for any reason.
Anaweza kufukuzwa uwaziri na wabunge au rais.
Tunapozungumzia wabunge, wao pia ni wananchi raia wqa Tanzania.
Kama mawaziri wasingetaka kujiuzulu, halafu babu mmoja mchawi akawaloga wakajiuzulu, the end result is the same and justifiable.Hakuna sheria inayozuia.
Taarifa zinasema kumekuwa na mazungumzo baina ya Rais Kikwete na Pinda yaliyolenga kunusuru serikali yao lakini wametofautiana kuhusu hatua inayopaswa kuchukuliwa dhidi ya mawaziri waliotakiwa kujiuzulu.
Msimamo wa Pinda inadaiwa kuwa anataka mawaziri wanaokabiliwa na tuhuma waondoke ili kuleta uwajibikaji serikalini, lakini Rais Kikwete amesema mawaziri hao waachwe waendelee na kazi zao, kwa kuwa suala hili ni la upepo tu, liachwe litapita.
Habari zinasema Rais Kikwete na Pinda walitofautiana juu ya hatua dhidi ya mawaziri hao, hivyo kuwafanya baadhi ya mawaziri kutamba mitaani kuwa hawang'oki madarakani kwa sababu tayari bosi wao ameonyesha kutounga mkono tuhuma hizo.
Habari hizi zinasema pia kwamba Pinda amekuwa hafurahishwi na msimamo wa ‘bosi' wake, hasa katika kushindwa kutoa uamuzi mgumu.
Baadhi ya wabunge wameweka wazi kuwa kama Rais Kikwete ataamua kuwalinda na kuwatetea mawaziri wake basi watawaondoa kwa mkakati tofauti utakaomlazimisha rais kukubaliana na hoja za wabunge.
Source: Gazeti la Tanzania Daima
Waziri anaweza kujiuzulu anytime, for any reason.
Anaweza kufukuzwa uwaziri na wabunge au rais.
Tunapozungumzia wabunge, wao pia ni wananchi raia wqa Tanzania.
Kama mawaziri wasingetaka kujiuzulu, halafu babu mmoja mchawi akawaloga wakajiuzulu, the end result is the same and justifiable.Hakuna sheria inayozuia.
EMT, hawa jamaa hata ukiwaelewesha usiku kucha hawataweza kuelewa unachosema. Caucus ya CCM si mbadala wa Bunge, na hakina uwezo wala ubavu wa kumlazimisha waziri ajiuzulu labda aamue mwenyewe. Na hata akiamua hivyo bado Raisi kama anamhitaji anaweza kumkatalia kama alivyowahi kumkatalia Dr. Idris Rashid wa TANESCO huko nyuma. Bunge pekee ndilo lenye uwezo wa kupiga kura ya kutokuwa na imani kwa ama Waziri Mkuu au Raisi ndani ya kikao rasmi cha bunge na siyo uchochoroni eti kwenye caucus ya CCM.Kwa maana hiyo unakubali kuwa "caucus" ya CCM haina uwezo wa kumfukuza waziri?
Au una maana gani unaposema kuwa waziri anaweza "kufukuzwa uwaziri na wabunge"?
Wabunge kwa maana ya wabunge wa bunge la Jamhuri au wabunge wa CCM kupitia "caucus" ya CCM?
Vipi rais akikataa kuitikia wito wao wa kuwafukuza kazi hao wabunge? Wako tayari kula matapishi yao?
kobello, unaishi katika nchi ya kusadikika siyo Tanzania and very soon you will come back to earth only a little wiser!The logic behind ni kuwavua madaraka mawaziri ambao ni wana-CCM wenzao kistaarabu. Wasiopotaka, basi baraza la mawaziri lote litaondoka!!! CCM ina majority, so only CCM caucus can do this!!!.... trust me, they can do it. Hata rais anaweza kuondolewa na wabunge wa CCM wakiamua kwa pamoja.
Nipe hicho kifungu please?