Wabunge si Wafanyakazi wa kawaida hivyo wasilinganishe Mishahara

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,605
8,744
Viongozi wa bunge wanaosema kwamba si wabunge tu wenye mishahara mikubwa bali wafanyakazi wengine wa serikali na kampuni kama NSSF na TANAPA wana mishahara na marupurupu makubwa wanakosea.

1. Wafanyakazi wengine wa serikali wamechaguliwa kama watendaji wa kazi. Wanaweza kufukuzwa kazi wakati wowote bila mahakama wala sababu yeyote. Mbunge hawezi kufukuzwa kazi na bosi wake kwa utendaji kwasababu bosi wake ni wananchi waliomchagua
2. Kazi za serikalini hazina mkataba zaidi ya kiwango cha miaka ya kustaafu. Kama mtu amepata kazi nyingine pengine yenye maslahi zaidi anaweza kuondoka wakati wowote. Wabunge wana mkataba na wananchi wa miaka mitano hivyo kama kuna mtu anagombea ubunge anatakiwa kujua ni mshahara gani na marupurupu gani atapata kwa miaka mitano na sio kujipandishia mishahara kiholela.
3.NSSF na Tanapa ni kampuni zenye vipato na zinaajiri wataalamu kwa mikataba ya malipo fuluni na marupurupu fulani. Mtu unaweza kwenda kufanya kazi kwenye kampuni kwasababu ya maslahi lakini huwezi kuenda kuwakilisha wananchi wako masikini kwa sababu ya maslahi yako binafsi. Unaweza kuwa mbunge lakini usiwe na uwezo wa kupata nafasi ya kazi NSSF au Tanapa kutokana na sababu nyingi kama uzoefu wa kazi na elimu.
4. Ubunge ni kazi ya kujitolea hivyo kama umeenda kugombea ubunge kwasababu ya maslahi ni kosa. Kazi za serikali zinahitaji wataalamu mfano kama wewe ni Engineer umepata kazi wizara ya ujenzi unaweza kuamua kufanya kazi pate au kwenye kampuni za nje kutokana na nani analipa zaidi hivyo kwasababu ya ushindani wizara ni lazima ilipe vizuri ili ipate ma Engineer. Ubunge ni tofauti kama hujaridhika na pesa na mafao basi usigombee ubunge na nenda katafute kazi nyingine.
Bunge halina kipato chochote zaidi ya kutumia pesa za watu. Bunge lina kazi moja tu ya kutunga sheria kitu ambacho tumeona ni kwamba sheria nyingi ni mbaya na ni za kifisadi kutoka bungeni. Hakuna kitengo kingine cha serikali kinaweza kukaa chini na kujipandishia mishahara kiholela baada ya kuchaguliwa.
 
Back
Top Bottom