Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 139
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema Wabunge na mawaziri wa Serikaliya Muungano wanaokejeli Maaumuzi ya Baraza la Mapinduzi juu ya kuliondoa suala la utafutaji mafuta na uchimbaji wa gesi asilia katika mambo ya Muungano wameishiwa na hoja.
Waziri wa Maji, Ujenzi,Nishati na Ardhi, Mansoor Yussuf Himid, Aliliambia Baraza la Wawakilishi wakati akijibu hoja mbali mbali zilizotolewa walipokuwa wakichangia bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wafedha 2009/10.
Waziri Mansour, alisema kauli ya Baraza la Mapinduzi iliyoiwasilisha mbele ya Baraza la Wawakilishi, juu ya maamuzi ya haikuwa yake binafsi na ni ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Wizara yangu inawajibika kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, inayoongozwa na Rais Dk. Amani Abeid Karume na Baraza hili lipo chini yake yeye Rais Karume na wewe Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho ndie unaeliongoza na siwajibiki kwa Wabunge alisema Waziri huyo.
Alisema kwamba Ni hulka ya mwanadamu anapokosa hoja usishangae kwani atatukana na anaweza kutupa mawe sasa na ndio hao wabunge wamekosa hoja anapojuwa amewatendea wenzake dhambi na wizi wa mchana alisisitiza Waziri huyo.
Alisema Baraza la Mapinduzi limeamua kutoa uamuzi huo baada ya kubaini kuwapo kwa ghilba za wizi wa mchana juu ya suala hilo zilizobainishwa na Mshauri elekezi na SMZ haijifurahishi kwani wanachokieleza wabunge hao pamoja Viongozi wa Muungano ni kutokana na kuishiwa kwa hoja juu maamuzi iliyoyachukua serikali.
Akifafanua kauli yake hiyo alisema katika baadhi maelezo ya Mshauri elekezi ambayo yamo ndani ya ripoti yake imeelezea wazi kuwa sheria zilizowekwa kusimamia mafuta na gesi asilia Tanzania, imetungwa ikiwa kama Zanzibar haimo ndani ya vipengele vyake vya sheria hiyo na ndio maana serikali haioni haja ya kuelezea kama suala hilo ni la Muungano.
Baada ya kuona tatizo lipo ndio maana serikali mbili ilizungumzwe na serikali kama zanzibar haipo utaifa uko wapi Alihoji Waziri huyo huku akishangiriwa na wajumbe wenzake.
Himid alisema kwamba sheria ya uundwaji wa Shirika la Kusimamia Mafuta Tanzania (TPDC) ni maoni ya muelekezi ya ambapo ameeleza kwamba halina sura ya Muungano.
Mwelekezi alisema utaratibu tunaoutumia ni wa ajabu na haupo duniani kote na unatumika Tanzania peke yake na akaelekeza kupelekwa katika Mahakma ya Kikatiba sasa tatizo liko wapi Mheshimiwa Spika tayari njia ipo ya kufuatwa Aliuliza Himid.
Nilisikia hadithi moja Nyerere akielezea dhana ya Mungano ambapo alimuita Karume akamwambia waunganishe nchi, lakini siamini kama Mzee Karume, na Mzee Thabit Kombo, waliondosha watawala wawili na kukubali kuletewa watawala wengine mmoja hakuna watawala wengine tunataka kujenga umoja alisema Waziri huyo huku akipumzika.
Baada ya kubainika hayo Mshauri Mwelekezi pia ametowa rai ya kwamba suala hilo serikali zote zielekee katika mahakama ya Kikatiba kwa vile utaratibu wake ulikuwa ni wa ajabu kabisa.
Waziri huyo alifahamisha ndio maana serikaliya Zanzibar iliyabaini hayo mapema tangu wakati wa utawala wa Dk. Salmin Amor, ambaye alitoa amri ya kuzizuia baadhi ya kampuni zilizopewa leseni na serikali ya Muungano kutafuta mafuta hapa Zanzibar.
Hapa Mshauri elekezi alikuja katika Baraza la wawakilishi, akatuambia kwamba sheria zote za mafuta zimetungwa kama Zanzibar haipo na Mamlaka ama taasisi ya kusimamia mafuta haipo wanalazimisha hii ni dhambi kubwa Mheshimiwa Spika wanayowatendea wenzao dhambi na ni wizi wa mchana kweupe kabisa alisema kwa hasira Waziri huyo.
Himid alisema Mshauri Mwelekezi alisema tatizo lipo na ndio maana alisema mlizungumze na ndio hatua hiyo ya Wajumbe wa Baraza hilo ilikuja baada ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini Tanzania bara Adam Kigoma Malima kuliambia Bunge kwamba msimamo wa SMZ kupitiaBaraza lake la Mapinduzi kuliondoa suala la mafuta katika kero za Muungano ni kujifurahisha jambo ambalo baraza hilo lilieleza ni kitendo cha dharau.
Kauli hiyo ya Malima pia iliungwa na mkono na Mbunge wa Same, Samueli Sita ambaye aliliambia Bunge hiyo kwamba hatua hiyoitailazimu SMZ kuamuliwa na Bunge mambo ambayo yalisababisha kutolewa matamshi mbali mbali ya wajumbe wa baraza la Wawakilishi.
Waziri huyo alifahamisha ni vyema kwamba Wabunge kutambua kuwa hakuna watawala wawili wanoweza kumtawala mtawala mmoja na kuzingatia kwamba Muungano uliounganisha Zanzibar na Tanganyika umefanywa kutokana na kujenga umoja wa nchi mbili hizo ili kutafuta mustakabali bora wa maelewano.
Wazanzibari wamefuta utaifa wao iliwafaidike na Muungano lakini sio kwa utaratibu wa sasa uliopo wanakejeli leo tunatafuta suluhu na njia muafaka tuna ambiwa tunajifurahisha Muheshimiwa Spika Baraza la Mapinduzi, ndio limeshaamua alisema Waziri huyo hukuakiwa anashangiriwa na wajumbe wa Baraza hilo.
Akiendelea alisema kazi ambayo hivi sasa Wizara hiyo inakusuda kuifanya ni kuona inamalizia kutayarisha sera ya kusimamia mafuta na gesi asilia, pamoja na kuandaa sheria ambayo inatarajiwa kuwasilishwa katikakikao cha mwezi Oktoba mwaka huu.
SOURCE: ZANZIBAR YETU BLOG.