Elections 2010 Wabunge na Joto la Uchaguzi

Ngisibara

JF-Expert Member
Jan 2, 2009
3,301
2,076
Bunge latibuka kwa homa ya uchaguzi,

LITAKUWA LA WIKI TANO, KUVUNJWA JULAI 16



Monday, 07 June 2010
Ramadhan Semtawa

UCHAGUZI mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, umegusa ratiba ya shughuli za Bunge, baada ya mkutano wake wa bajeti unaoanza kesho mjini Dodoma, kutarajiwa kufanyika kwa wiki tano badala ya miezi mitatu kama ilivyozoeleka.Habari za kuaminika zilizopatikana mwishoni mwa juma lililopita kutoka ofisi ndogo ya Bunge jijini Dar es Salaam ,zilisema Bunge litavunjwa Julai 16, ili kupisha maandalizi ya uchaguzi huo.

Spika wa Bunge Samuel Sitta, jana alithibitisha habari hizo na kwamba ratiba hiyo imezingatia kwa kina, mchakato wa uchaguzi mkuu na namna ya kupata serikali mpya.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa Bunge, kutokana na ratiba ya mchakato wa uchaguzi mkuu, lazima mkutano huo wa Bunge uwe mfupi tofauti na miaka ya nyuma.

"Ndiyo, Bunge litavunjwa Julai 16 kwa sababu lengo ni kuendana na ratiba ya mchakato wa kupata wagombea na kisha majina yao yapelekwe Nec (Tume ya Taifa ya Uchaguzi)," alifafanua.

"Hatuwezi kutumia muda mwingi kwa mijadala mirefu wakati tutahitaji utekelezaji wa bajeti kwa kupata serikali mpya...kwasababu mawaziri watapaswa kupatikana ili waweze kusimamia na kutekeleza bajeti ya serikali," alisisitiza.

Kwa kawaida Bunge la bajeti linafanyika kwa kipindi cha kati ya miezi miwili hadi mitatu, kuanzia Juni.

Spika Sitta alipoulizwa iwapo majuma matano yatatosha kushughulikia mijadala ya bajeti , alisisitiza " mijadala ni muhimu, tumepanga vema ratiba lakini ni vema tukafupisha muda kwa ajili ya kupata serikali mpya."

Mchakato wa kura za maoni kwa wabunge CCM unatarajiwa kuanza Julai 19 na baadaye, majina ya washindi na wagombea wengine kutoka vyama vingine, yamepangwa na kuwasilishwa Nec kwa uthibitisho na uhakiki.

CCM tayari pia imetangaza kuanzia Juni 21 itaanza kutoa fomu za urais kwa wagombea wake, huku ratiba ya NEC ikionyesha hadi Agosti 19 majina ya wagombea wa vyama yanapaswa yawe yamewasilishwa kwake.


Tayari vyama vingine ikiwamo CUF vimeshafanya mchakato wa kupata wagombea wake wa uwakilishi na ubunge kwa Zanzibar huku mchakato kwa nafasi za Urais bara na visiwani ukitarajiwa kumalizika leo.

Lakini, tayari mpaka sasa imeonyesha kuwa mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba na katibu wake Maalim Seif wanaonekana kupita bila kupingwa.

Vyama vingine ikiwamo Chadema, NCCR na TLP bado vinaendelea na mchakato wa kupata wagombea wao.

Spika akifafanua zaidi, alisema bunge litajadili vema bajeti ya serikali lakini akaweka bayana kwamba macho na masikio ya Watanzania ni kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba.

"Ni kweli miaka yote tumekuwa tukianza bunge Juni hadi Agosti mwishoni,... lakini safari hii nchi yetu iko kwenye uchaguzi ambao tunapaswa kujipanga vema mapema kwa ajili ya utekelezaji wa taratibu."

Mwaka jana, baadhi ya mijadala kwa baadhi ya wizara zenye mambo mengi ilifanyika kwa takriban siku mbili hadi tatu huku bunge likiwa linafanyika hadi siku za Jumamosi.

Kikatiba, Rais anakuwa sehemu ya bunge linapokaa kama hadhara kuu (National Assembly) na ana mamlaka ya kulivunja wakati wowote au kwa mujibu wa kipindi cha kila baada ya miaka mitano ya bunge.



Mwee! kumbe wiki tano uwaga zinatosha kumaliza Bajeti...Kweli mwaka huu tutaona mengi :mad2:
 
Tatizo sio ukata maana nimesoma mahali makusanyo yamepungua kuliko mategemeo. Na kama mwaka huu itawezekana basi miaka yote wafanye hivyo ili kupunguza gharama za posho kwani zinaongeza matumizi serekalini.
 
Back
Top Bottom