Wabunge: Kwanini Kodi ya Maji ni Muhimu Kupunguzwa au Kufutwa

Za10 mwanasayansi kanithibitishia kuwa maji ya bomba yaliyochemshwa ni safi na salama kuliko hayo ya chupa - walifanya utafiti kwenye maabara chuo kinachoheshimika SASA huo 'mnyororo wa thamani' unaouongelea una faida gani au ni geresha ya kutuibia?

PS. Pia maplastiki yana athari kwa afya na mazingira!
 
Mkuu hawa wahuni washaanza kuyaachia maji kwa wafanyabiashara. Serikali inataka kuwasamehe kodi ili system iwe kama unataka maji kanunue.

Tusikubali hili.... siyo halali. Mwisho wake wataanza kumiliki sehemu za mito na vyanzo vyetu vya maji na kuanza kutuchaji.

Hapana bwana. Maji ya chupa au kwenye majagi ni vitu vya kawaida tu. Na wafanyabiashara sio neno baya na sio wanyonyaji.

Hivi kwani computer hazina ushuru? Hivi ushuru wa computer na maji ya chupa upi muhimu?
 
Hayo ndiyo matatizo yenu.
Mimi nilipo, huwa watanzania wengi wanadhani ni the most capitalist country (US).
Ila ukijaribu kuangalia, Tanzania is more capitalist than US. Hebu kula nondo hapo chini.

Huwezi kuwa capitalist bila kuwa na capital. Tanzania tunataka kuwa capitalist na kufuata liberal western democracy wakati hatuna misingi ya vitu hivyo.
 
Za10 mwanasayansi kanithibitishia kuwa maji ya bomba yaliyochemshwa ni safi na salama kuliko hayo ya chupa - walifanya utafiti kwenye maabara chuo kinachoheshimika SASA huo 'mnyororo wa thamani' unaouongelea una faida gani au ni geresha ya kutuibia?

PS. Pia maplastiki yana athari kwa afya na mazingira!

Kuna mambo mengi ya kuchukua. Unapochemsha maji unatumia energy. The total energy ya kila mtu kujichemshia maji, tayari mnapata viwanda. Hivyo cost zingine hakuzichukua.

Huyo mwanasayansi mwenye alifanya utafiti akiwa na water bottle pembeni.
 
Hapana bwana. Maji ya chupa au kwenye majagi ni vitu vya kawaida tu. Na wafanyabiashara sio neno baya na sio wanyonyaji.

Hivi kwani computer hazina ushuru? Hivi ushuru wa computer na maji ya chupa upi muhimu?
Ushuru wa computer siyo muhimu kama wa maji.
Ushuru kazi yake siyo kulipatia taifa fedha tu... bali hutumuka kudiscourage vitu kama ulevi, uvutaji sigara, kamari, uharibifu wa mazingira, unyonyaji wa maliasili , imports etc... pia hutumika kulinda viwanda na wafanyakazi wetu.

On the other hand ushuru hautakiwi kudiscourage intellectual property i.e uvumbuzi. Kwa mfano majiko ya gesi asilia, solar panels, computers, cell phones, hybrid cars na mazao ya nyumbani.

Think deep, be independent and most of all have mercy on our people mayn!... the've had enough!
 
Kuna mmoja humu JF signature yake ni "Drink beer, save water".

Utengenezaji wa beer unatumia maji mengi sana. Na mtu kama huyo anaangalia beer kama final product. Lakini akiangalia process ya utengenezaji wa beer, atajua kuwa sio sahihi.
 
Huwezi kuwa capitalist bila kuwa na capital. Tanzania tunataka kuwa capitalist na kufuata liberal western democracy wakati hatuna misingi ya vitu hivyo.
That what you think..... brah, you are wrong. Hebu soma quote hii kutoka kwa mchumi aliyeheshimika wa Scotland.

"Labour was the first price, the original purchase - money that was paid for all things. It was not by gold or by silver, but by labour, that all wealth of the world was originally purchased. "
Adam Smith

Read more: Adam Smith Quotes - BrainyQuote
 
Ushuru wa computer siyo muhimu kama wa maji.
Ushuru kazi yake siyo kulipatia taifa fedha tu... bali hutumuka kudiscourage vitu kama ulevi, uvutaji sigara, kamari, uharibifu wa mazingira, unyonyaji wa maliasili , imports etc... pia hutumika kulinda viwanda na wafanyakazi wetu.

On the other hand ushuru hautakiwi kudiscourage intellectual property i.e uvumbuzi. Kwa mfano majiko ya gesi asilia, solar panels, computers, cell phones, hybrid cars na mazao ya nyumbani.

Think deep, be independent and most of all have mercy on our people mayn!... the've had enough!

Kutokuwa na ushuru wa Tanzania kumefanya nchi iwe jalala la macomputer mabovu na sioni innovation yoyote. Na toxic zinazotokana na macomputer mabovu zinafanya wanaume wawe impotent.

Kenya wanalipa ushuru na wako mbali.
 
Well, we can always review it and restrict the importation of used computers as well as used cars and other products....
But philosophically, you are wrong on water tax.
 
Hakuna mtaji. Kuna ujangiri tu.

"If money, according to Augier, 'comes into the world with a congenital blood-stain on one cheek,' capital comes dripping from head to foot, from every pore, with blood and dirt" - Mtunzi wa MTAJI
 
That what you think..... brah, you are wrong. Hebu soma quote hii kutoka kwa mchumi aliyeheshimika wa Scotland.

"Labour was the first price, the original purchase - money that was paid for all things. It was not by gold or by silver, but by labour, that all wealth of the world was originally purchased. "
Adam Smith

Read more: Adam Smith Quotes - BrainyQuote

Tena hapa pembeni nina volume yake Wealth of Nations. Moja ya kazi yake ni division of labour. Na anakwambia kuwa katika nchi zilizo-advance, labour hiko very speciliazed. Na katika nchi zetu labour, specialization ni duni.

Kwa mfano ukienda UDSM, professor ana banda la kuku. Na hapo hapo anafundisha. Ukienda Osterbay, Waziri ana banda la ng'ombe, mbunge na mwekezaji. Matokeo hakuna ufanisi.
 
Well, we can always review it and restrict the importation of used computers as well as used cars and other products....
But philosophically, you are wrong on water tax.

Ninaweza ku-prove kuwa tax Tanzania ni mzigo wa maendeleo ya nchi. Sio ya chupa za maji tu.
 
"If money, according to Augier, 'comes into the world with a congenital blood-stain on one cheek,' capital comes dripping from head to foot, from every pore, with blood and dirt" - Mtunzi wa MTAJI

Ukweli wa mambo I love capitalism. Lakini kwa Tanzania naona hakuna moral grounds for it.
 
Ndugu wananchi !Kwa miaka mingi sana serikali ya Tanzania inatumia kodi ya vinywaji kuongeza mapato ya serikali. Katika kipindi cha Nyerere na cha Mwinyi, walipaji wakubwa wa kodi walikuwa ni viwanda vya vinywaji, hususa bia. Ukweli wa mambo utamaduni huu wa kutegemea kodi ya vinywaji hususa maji hauna faida kwa serikali na kwa jamii kwa sababu zifuatazo:-

Maji ni kitu muhimu kwa maisha ya binadamu. Unywaji wa maji masafi unapunguza magonjwa mbalimbali. Na kuwepo kwa kodi katika bidhaa hiyo kunasababisha maji ya chupa kuwa kitu cha anasa na hivyo kutumiwa na wale wenye uwezo. Hii ni fikra mbovu. Kinachotakiwa ni kuwa kabla mtanzania hajanunua vocha ya simu, awe na uwezo wa chupa ya maji.

Ni kweli punguzo la kodi litawasaidia wafanya biashara wa maji ya chupa. Lakini ni nani amesema kuwa watu wa kawaida hawatafaidika. Punguzo la kodi litafanya watu wengi kunywa maji safi. Na ongezeko la idadi litafanya ongezeko la uzalishaji ambalo litaongeza nafasi za kazi. Hivyo sioni sababu za kimsingi za kutopunguza au kuongoa kabisa kodi kwenye maji.

Wabunge mnapokuwa bungeni au kwenye magari yenu ya kifahari mna chupa za maji. Na ikitokea mtu kaiba chupa zako, hamkubali kuomba maji kwenye nyumba za wanyonge. Sasa kwanini kitu chenye manufaa kwa afya yenu mnakifanya kiwe adimu kwa walala hoi?

Mwishoni kodi ya maji haina faida kwa taifa. Hii ni kwa sababu, wanyonge wanaposhindwa kunywa maji safi au kujenga tabia ya kunywa maji safi, wanakunywa maji ambao yanawapa magonjwa. Na magonjwa yatokanayo na maji machafu yanatibiwa na mapato ya kodi. Hivyo serikali haipati faida yoyote hile.

Ni muhimu kwa watanzania kuelewa kuwa sio kila kodi ni muhimu kwa wananchi.Ndugu wabunge, wananchi, na wale wenye kufikiri kuwa kila kodi ni muhimu kwa taifa naomba wafikiri kuwa kodi ya chupa ya maji ni sawa na kodi kwenye kondomu. Unapoweka kodi kwenye kondomu, unafanya iwe na bei mbaya na kufanya masikini waache kutumia.Hivyo basi ningependelea kuwa chupa za maji zisiwe na kodi, au ikiwezekana serikali itoe ruzuku ili kila mtanzania awe na uwezo wa kunywa maji safi.

Wenu

Z10

Niambie tu ni kitu gani kilishawahi kupunguziwa kodi ukauona unafuu. Angalia shule binafsi zimeunguziwa kodi lakini hebu ona ada zake. Kwa tanzania hakuna unafuu wa kodi unaomnufaisha mtanzania.
 
Back
Top Bottom